|
|
|
Wengi watuma rambirambi na misaada Vyombo vya habari vyaitaka serikali iache papara Na Mwandishi Wetu Idadi ya watu waliokufa katika milipuko ya mabomu mjini Dar es Salaam na Nairobi imedaiwa kufikia 258 hadi kufikia jana, 248 wakiwa ni waliokufa Nairobi na 10 Dar es Salaam. Waliokufa katika tukio la Dar es Salaam wametajwa kwamba ni Ramadhani Mahundi, Mtendeje Rajabu, Abbas William na Omar Ahmed Nyumbu. Wengine ni Abdallah Mohamed, Dotto Selemani, Abrahman Abdallah; Hassan Siyad na Yusuf Shamte. Maiti moja ilikuwa haijatambuliwa. Msiba huu mkubwa umesababishwa na milipuko miwili mikubwa katika Balozi za marekani jijini Dar es Salaam na Nairobi Ijumaa ya Agosti 7; 1998. Serikali kupitia viongozi wake wa ngazi za juu; imeeleza kushtushwa kwake na tukio hilo na kwamba itafanya kila iwezalo kuwapata watu waliohusika. Aidha watu binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na nchi za nje zimekuwa zikitoa salamu za rambirambi; pole na misaada ya matibabu. Wakati askari wa Israel wamekuwa wakishiriki katika zoezi la kuwaokoa walionasa katika vifusi vya majengo yaliyobomoka mjini Nairobi. Serikali ya Misri imetuma madaktari na tani mbili za madawa. Saudi Arabia nayo imeripotiwa kutuma ndege ya msaada kwa ajili ya waathirika wakati inasemekana kwamba serikali ya Canada imetoa msaada wa shilingi milioni 45. Wakati juhudi za Serikali ya Tanzania ikishirikiana na vyombo vya usalama vya Marekani; ikiendelea na juhudi zake za kuwatafuta wahusika imeripotiwa kwamba Waislamu nchini Kenya wanalalamika kuwa wamekuwa wakinyanyaswa toka kutokea kwa mlipuko huo. Taarifa za vyombo vya habari zimedai kwamba vijana wa Kiislamu na baadhi ya waalimu wa dini wamekuwa wakikamatwa bila maelezo yoyote. Naibu Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu nchini Kenya (SUPKEM) amewataja watu waliokamatwa na polisi kuwa ni Amjad Javed na Mwalim wa Dini Abdulrazak Qare aliyekamatwa huko Isiolo. Mwalimu Abdulrazak ana asili ya Pakistani. Aidha Sheikh Ibrahim amekaririwa alisema kwamba vijana wawili raia wa Kenya wenye asili ya Kiarabu walikamatwa mjini Nairobi na haijulikana wanakoshikiliwa. Nalo Baraza la Ushauri la Waislamu wa Kenya limelaani kitendo cha gazeti la ‘East Africa Standard’ la Jumatano Agosti 12, kuchapisha Katuni ikionyesha Muislamu akiswali kando ya bango lililoandikwa "Kambi ya Ugaidi". Wakati huo huo, baadhi ya vyombo vya habari vimeitaka serikali kuchukua hadhari katika zoezi la kuwasaka waliohusika na mlipuko wa mabomu katika Ubalozi wa Marekani. Vyombo hivyo vimeishauri serikali iacha papara inayoashiria kujitokeza katika usakaji wa watuhumiwa. Ushauri huo umekuja kufuatia kukamatwa kwa watu 14 ambao imedaiwa ni
raia wa nchi za Sudan, Iraq, Somalia na Uturuki. Ambapo masaa machache
baadaye ikaripotiwa kwamba mmoja wa watuhumiwa hao mwenye asili ya Kisomali
ni mfanyakazi wa shirika moja la Umoja wa Mataifa ambaye kituo chake cha
kazi ni mkoa wa Kigoma.
|
Serikali yaipongeza Africa Muslim
Agency
Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba
1998:
Athari ya milipuko Dar, Nairobi: Waliokufa
wafikia 258
Wakuu wa mashule waache ubaguzi
ABU AMEENA: Mwana harakati aliyesilimisha wanajeshi 3000 wa Marekani -2 Kisiwa cha Karafuu chageuzwa cha ulevi Twalaban wadhibiti Afghanistan yote Madina yachapisha kitabu cha rejea MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA Maoni: Nyerere kasema kweli Ujamaa
na Ukristo vimeshindwa
Kina Ngatara na wenzake ndio urithi
tulioachiwa na Wakoloni
HOJA BINAFSI: Suala la Mwembechai,
serikali imeumbuka
Kupigwa mabomu misikitini: Waislamu
tumejifunza nini?
MAONI: Hoja za kutofautisha Yesu
na Issa ni udhaifu na ni uzushi mtupu!
Utangazeni Uislamu kwa nguvu
zote – Sheikh Jongo
Salafiya wataka wanawake
wawe macho na vyombo vya habari
Waumini Misufini Morogoro
waazimia kujenga Msikiti
Serikali yatakiwa kuondoa
askari Mwembechai
|