AN-NUUR
Na.162 Rabiul Thani 1419, Agosti 14 - 20, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 MAONI
Nyerere kasema kweli Ujamaa na Ukristo vimeshindwa
Na Abdul Gullam

Rejea habari zilzochapishwa katika gazeti la Msemakweli toleo nambari 013 la Jumapili Juni 7-13, 1998 yenye kichwa cha habari,"Nyerere adai Ujamaa na Ukristo vimeshindwa" likinukuu mahojiano yaliyofanyika katika kipindi cha maswali na majibu katika television ya CNN. 

Nyerere alisema, "Ujamaa umeshindwa kama vile Ukristo ulivyoshindwa. Ukristo ulianza yapata miaka 2000 iliyopita na kila Jumapili niendapo Kanisani nakuta watu bado wanahubiri. Na kwa kweli sina hakika kama kuna nchi hata moja tunayoweza kuiita taifa la Kikristo." 

Katika toleo hilo mwandishi wa Msemakweli akiripoti maoni ya Wakristo mbalimbali juu ya madai ya Nyerere.Wakristo wengi, wakiwemo Maprofesa na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo,walijitahidi sana kuutetea Ukristo kuwa haujashindwa bali Ujamaa ndio ulioshindwa peke yake. Moja ya sababu zilizotolewa ni kuwa Ujamaa umeshindwa kwa vile umetokana na mawazo ya mtu (Nyerere), wakati ukristo haujashindwa kwa sababu haukuanzishwa na mtu bali na Yesu (ambaye Wakristo wengi hudai ni Mungu aliye hai). 

Nyerere anaitwa baba wa Taifa na ni mtu wa kimataifa na hivyo maneno yake yanakuwa na uzito wa aina yake katika jamii. Sidhani kama Nyerere alitoa madai haya kwa mzaha tu. 

Nyerere ni muasisi wa ujamaa wa Tanzania na amebahatika kushuhudia ukisambaratika mbele ya macho yake, pamoja na juhudi zake za kuhakikisha ujamaa unadumu. Vile vileNyerere ameshuhudia waasisi wa mfumo huu duniani Urusi au Soviet Union ya zamani ikisambaratika bila hata risasi moja kufyatuliwa. 

Sina sababu yoyote ya kutilia mashaka matamshi ya Nyerere ambaye, pamoja na kuwa ni muumini mzuri sana wa kanisa Katoliki, vile vile ametoa mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya Ukristo hapa Tanzania. 

Naamini ametoa matamshi hayo kwa kutumia uzoefu wake wa kitaifa na wa kimataifa katika masuala mbalimbali ya kijamii na kisiasa. Kutokana na uzoefu huu Nyerere yuko katika nafasi nzuri sana ya kuchambua na kuongelea masuala haya. 

Imeleweka wazi kuwa Ujamaa ni mfumo wa maisha ambao uliasisiwa na kina Karl Marx na Lenin, hawa ni binaadamu kama mimi na wewe. 

Je, Ni kweli kuwa Ukristo (Christianity) ulianzishwa na Yesu, Mungu aliye hai? Biblia inatueleza kuwa Ukristo kwa mara ya kwanza ulianza pale Antiokia ambayo iko katika bara la Ulaya (soma Matendo ya mitume 11:26) miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa amekwisha kamilisha kazi aliyotumwa na Baba yake hapa duniani. 

Ikumbukwe hapa kuwa Yesu hakuwahi kufika Antiokia katika maisha yake yote ya hapa duniani. Na aliwakataza kabisa wanafunzi wake kupeleka mafundisho yake nje ya Israel (soma Mathayo: 10:5-6). 

Hakuna hata sehemu moja katika Biblia tunapofahamishwa kuwa Yesu alileta mfumo mpya wa maisha hususan Ukristo. Yesu mwenyewe anatufahamisha kuwa hakuja kutangua mfumo alioukuta uliokuwepo toka wakati wa nabii Musa (ambao sio Ukristo), bali kuutimiliza (Mathayo: 5:17-20). Na kwa Wayahudi peke yao, na wala sio kwa Wazungu au Waafrika au Wahindi au makabila mengine (Gentiles) ya ulimwengu huu (Mathayo 14:21-28). 

Ukristo umeasisiwa na Sauli ambaye ndie Paulo. Katika mazingira ya kutatanisha bila ya kuwepo ushahidi wa kuaminika, Paulo alidai kupewa Utume na Yesu mwenyewe katika Njozi. 

Kwa ajili ya majadiliano haya naomba tukubali kuwa Paulo alikuwa Mtume. Lakini bado hii haimpi hadhi ya Uungu, bado anabaki kuwa binaadamu kama wengine. 

Katika nukta hii tukumbuke kuwa Paulo hakuwahi kukutana na Yesu katika uhai wake. Na ni vema vile vile tukakumbuka kuwa huyu ndio yule Paulo aliyekuwa mstari wa mbele katika kuwatafuta na kuwaua wanafunzi wa Yesu. 

Vile vile tisisahau kuwa huyu ndie Paulo aliyekufa kwa kukatwa kichwa karibu na Roma kati ya mwaka 61B.K. na 68 B.K. Bibilia haituelezi kuwa Paulo baada ya kufa alifufuka na hivyo kuushinda umauti kama inavyodaiwa kwa Yesu, hivyo kupata hadhi ya uungu. 

Inaendelea toleo lijalo...
 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Serikali yaipongeza Africa Muslim Agency 
Na Mwandishi Wetu, Moshi 

Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba 1998: 
Afisa Elimu akiri kutaka orodha ya wanafunzi 
Na Mwandishi Wetu, Morogoro 

Athari ya milipuko Dar, Nairobi: Waliokufa wafikia 258 
Na Mwandishi Wetu 

Wakuu wa mashule waache ubaguzi 
Na Mwandishi Wetu 

ABU AMEENA: Mwana harakati aliyesilimisha wanajeshi 3000 wa Marekani -2 

Kisiwa cha Karafuu chageuzwa cha ulevi 

Twalaban wadhibiti Afghanistan yote 

Madina yachapisha kitabu cha rejea 

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA 

Maoni: Nyerere kasema kweli Ujamaa na Ukristo vimeshindwa 
Na Abdul Gullam 

Kina Ngatara na wenzake ndio urithi tulioachiwa na Wakoloni 
Na J. Hussein 

HOJA BINAFSI: Suala la Mwembechai, serikali imeumbuka 
Na Mwinjilisti Kamara Kusupa 

Kupigwa mabomu misikitini: Waislamu tumejifunza nini? 
Na RAJAB RAJAB

MAONI: Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu na ni uzushi mtupu!
Na Muhibu Said

Utangazeni Uislamu kwa nguvu zote Sheikh Jongo
Na Badru Kimwaga

Salafiya wataka wanawake wawe macho na vyombo vya habari
Na Mwandishi Wetu

Waumini Misufini Morogoro waazimia kujenga Msikiti
Na Rajab Rajab, Morogoro

Serikali yatakiwa kuondoa askari Mwembechai
Na Badru Kimwaga

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi 

Masomo 

Chakula na Lishe  
 
 

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita