|
|
|
Ndugu Mhariri KWA kweli nimekaa nikitafakari na kalamu yangu mkononi juu ya "Ucha-Mungu" ule tuliokuwa tukifundishwa na Waadhamu kuwa ndiyo kigezo cha kuwapata Wacha Mungu wanaofaa kutuongoza, lakini baada ya kutazama kwa jicho la yakini nimeibuka na maswali yanayonitatiza. Mara tu baada ya wachapakazi wacha Mungu kupewa usukani kwa kuapishwa na kuahidi kufuata Katiba na uongozi wa sheria huku wakiwa wameshika vitabu vitakatifu mikononi mwao, vijana wakatumwa kuvamia ghala la ngano na kuiteketeza kabisa bila ya kujali kauli ya mahakama kwa madai tu yasiyothibitishwa, ukihoji, "Hii ni awamu ya ukweli na uwazi" Jamani! Ni ucha Mungu gani huu? Awamu hii serikali haikukarabatiwa, bali imeundwa, makusanyo ya kodi yanasimamiwa ipasavyo ,watu wanahimizwa na mafanikio ya ukusanyaji hutangazwa, lakini huduma za afya taabu, umeme kwa shida, maji ndio usiseme. Hivi ni uchamungu gani huu wa kukusanya kodi kwa makini bila ya kuboresha huduma za jamii. Haya, na sasa serikali inabidi kupunguza gharama za uendeshaji, punguza punguza ya watumishi serikalini ikashamiri, ubinafshaji juu, wanasema ajira itaongozeka, kazi akawa kwa waliopunguzwa kupata mafao yao. Hivi ni uchamungu gani huu? Paroko katoa tamko, misamaha ikaombwa na ahadi za kuwashughulikia Waislamu zikatolewa, Mkuu wa Mkoa akapata kazi, kamata kamata ya Waislamu ikaanza nyumba hadi nyumba. Kosa lao nini? Wamesema Yesu si Mungu, hakufa msalabani na Mungu ni mmoja wala hana mtoto. Piga yule! Mwongeze ! Muislamu anadondoka chini na damu inafukiwa kwa mchanga kosa lake nini? "Wacha Mungu" wakaendelea kwa kupongezana baada ya kufanya mauaji kana kwamba haikutosha, wakavunja Msikiti na kushambulia akina mama wa Kiislamu kwa mabomu pamoja na kuwadhalilisha. Kosa lao nini? Huku ndio kufuata na kulinda katiba mlikoahidi wakati mkila kiapo? Huu ndio uongozi wa sheria uliotuahidi? Au Ukweli na Uwazi maana yake ni kuwaua Waislamu na kuwadhalilisha akina mama wa Kiislamu hadharani? Akisema Paroko, amani na utulivu wa nchi huhatarishwa na Waislamu wakasakwa na kuuawa kama panya au mende wanafanya uharibifu, bunduki na risasi vitatumiwa, Paroko katulia anasubiri kuwapongeza "Wacha Mungu" wake kwa kuwapa mkate "Baba kazi uliotutuma tumeimaliza". Akisema Ponda kuwa wauaji pamoja na wale waliowadhalilisha akina mama wa Kiislamu wakamatwe inakuwa nongwa, anaanza kusakwa na familia yake kupekuliwa kila siku, Waislamu wa mtaani kwake wanaviziwa wakati wa sala ya alfajiri hukamatwa na kuhojiwa kutwa nzima kuhusu Ponda. Kwani Ponda kosa lake nini? Oh anahatarisha amani! Paroko je? Hivi ni
ucha Mungu gani huu.
Idd S. Kikong'ona,
Uislamu shuleni Galanos mashakani Ndugu Mhariri TUTAFURAHI iwapo utatupatia nafasi katika gazeti lako hili kuweza kuelezea masuala ya Uislamu katika shule yetu ya Galanos. Kwa miaka mingi hususan tangu Mkuu wa shule aliyepo hivi sasa kuja hapa, kuna mambo mengi yanayotendeka ambayo yana lengo la kuuzima na kuutokomeza Uislamu kamili hapa shuleni. Mara kwa mara Mkuu wa shule ya Galanos amekuwa akitoa hotuba fupi fupi aidha tuwapo mstarini wakati wa asubuhi au kabla ya kuingia madarasani ama katika mabaraza mbalimbali ya shule akiuponda Uislamu na Waislamu na kutaka kuwatoa au kuwapunguza imani baadhi ya wanafunzi Waislamu waliopo hapa. Kwa mfano, utamsikia akisema "Dini, dini kitu gani? waanzilishi wa dini huko kwao sasa wameacha majengo yao ya (ibada kama magofu kwa kuwa hakuna anayekwenda kuswali). Na huko Uarabuni wengi wanao swali swali ni wale wasio na kazi. Hivi eti unaswali kutwa mara tano unatarajia kazi za maendeleo uzifanye katika muda gani? Yote hii ni ukosefu wa elimu, ukisoma bwana utaona kwamba dini si chochote mbona watu wanakufa tu!" Mnamo mwaka 1995 wakati tulipoanza kupigania suala la kuruhusiwa kuvaa hijabu kama agizo la mstaafu Rais Alhaj Ali Hassan Mwinyi lilivyotutaka, Mkuu huyo alitoa kauli za kebehi na kulidhalilisha vazi hili la heshima, "Kujifunika funika ni ushamba, kwani usipojifunika imani yako inaondoka? Huku kuzubaa zubaa ndiko kunanyima watu wengi maendeleo. Eti mtu anavaa kanzu hayo ni mavazi ya watu wa jangwani shauri ya joto". Pamoja na kwamba kauli hii huitoa kwa pamoja tunapokusanyika, lakini wakati mwingine hata humfuata mtu mmoja mmoja aliyemaliza kidato cha nne mwaka 1996 japokuwa kijana huyu hakubabaishwa na vitisho hivyo. Baada ya shinikizo kali kutoka kwa uongozi wa shule wa Jumuiya na Taasisi mbalimbali mkoani Tanga, hatimaye tulianza kuvaa suruali badala ya kaptula. Lakini kwa upande wa mabinti bado hawaruhusiwi kujifunika vitambaa wawapo darasani. Ratiba ya shule kwa miaka mingi haikuwa na nafasi maalum kwa ajili ya vipindi vya dini isipokuwa vipindi hivi vimewekwa sambamba na wakati ambapo Waislamu wanakwenda kuswali sala ya Ijumaa. Hali hii huwa fundisho tu wale wasio Waislamu kwa kuwa walimu wao wa dini kutoka mitaani hufika kuwafundisha. Sasa kwetu sisi ni yupi ataacha kwenda kusali sala ya Ijumaa abaki shuleni, je, atafundishwa hiyo dini na Mwalimu yupi asiyejuwa umuhimu wa Ijumaa? Kwa kweli hili limepangwa makusudi tusizidi kupata elimu yetu ya dini na kuielewa haki na batili kikamilifu. Hali hii ya kuikosa elimu ya dini pamoja na kuwa na imani dhaifu juu ya Allah (s.w.) ndiyo inayopelekea hata wale walimu ambao kwa majina hujulikana kwamba ni Waislamu wamebaki kimya isipokuwa mwalimu mmoja ambaye naye tunasikia amepewa ukuu wa shule katika shule moja huko Moshi, Mungu amzidishie. Mwaka 1996 waliua nguruwe katika maeneo ya shule ambaye ni miongoni mwa mifugo iliyopo shuleni hapo. Baadhi ya wanafunzi wasiokuwa Waislamu walihudhuria kula haramu hiyo kisha wakachuku mafuta na kurudi nayo mabwenini kwa matumizi ya baadae huku wakijisifu, "Tuone hao wanaosema haramu kama watahama shule". Ukichukulia kwamba wanafunzi shuleni huishi kama ndugu kwa kushirikiana vyombo na vitu vingine hali ambayo iko wazi kwamba Waislamu wangelishwa nguruwe. Suala hili kama sio busara za uongozi wa jumuiya yetu uliokuwa madarakani wakati ule, karibu lingezua mtafaruku mkubwa baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Watu walishapanga mikakati mingi ikiwemo wa kuwapiga wote waliohudhuria katika sehemu aliponyongewa mnyama huyo. Watu walipoozwa na kuombwa waache ghadhabu, wakawasikia viongozi wao na suala hili kupitia kwa mwalimu huyo aliyehamishwa likafikishwa kwa Mkuu wa Shule ili wahusika wachukuliwe hatua. Alichofanya Mkuu huyu ni kutucheza shere kwa kutuonyesha usoni kwamba limemuudhi lakini bila kuchukua hatua yoyote akasema "sheria za shule haziruhusu nguruwe kuchinjwa karibu na majengo ya shule, wanafunzi wanaohudhuria kupata nyama hawaruhusiwi kubeba kitu chochote kujanacho shuleni na haitakiwi kumnyanyasa mwenzako juu ya imani yake. Hivyo kwa suala hili naahidi halitarudiwa tena na nguruwe sasa watachinjwa mbali kabisa chini ya usimamizi mkali na wale wote waliohusika tutawachukulia hatua kali". Hakuna hatua kali iliyochulikuwa mpaka sisi tunamaliza muda wetu shuleni hapo. Lakini kama ni sheria kwanini wasiadhibiwe hali ya kuwa wanafahamika? Mbona wanaotoroka na kwenda nje ya shule husimamishwa masomo kwa muda kisha hurudi makwao? Kwanini wanafunzi Waislamu wanapokwenda kuswali sala ya Ijumaa bila ya kuvaa sare za shule hunyang’anywa nguo waliovaa? Au hawa sio miongoni mwa wana Galanos? Bila shaka huu ni unyanyasaji katika imani. Ni jambo la kumshukuru Allah (s.w.) kwamba kila uongozi wa jumuiya unaokuwa madarakani umejitahjidi kukemea suala la wanafunzi Waislamu kuhudhuria disko kwa kuwa ni kinyume na maadili yetu, lakini uongozi wa shule hasa kupitia kwa mwalimu wa nidhamu na starehe waliodumu mpaka mwaka huu mwanzoni wanajaribu na kufaulu kwa kiasi kikubwa kuwashawishi baadhi yetu kuhudhuria. Kwa sababu hivi sasa disko huwa mchana mashuleni, wamejaribu kuwaandikia wazazi wa mabinti Waislamu kuwaombea ruhusa kwa kuwa mara nyingi masuala haya huwa siku za Jumamosi, lakini maombi hayo hupotoshwa maana ili kupunguza ugumu wa kuruhusiwa. Utakuta badala ya binti kuombewa kuhudhruia disko ombi huwa "Tunakuomba mzazi wa (binti Muislamu) umruhusu mwanao aje shuleni Jumamosi kuna sherehe fupi. Ni muhimu sana kwani kuhudhuria kwake ndio mafanikio". Sasa hapa mzazi anampa ruhusa mwanae kwa kutofahamu undani halisi. Kwa shuleni Galanos ni vigumu kwa wanafunzi wanaosoma pale kutoa malalamiko kama haya au hata ya masuala mengine, kama chakula na afya au michango mbalimbali kwakuwa ikibainika tu utajengewa hoja na maisha yako shuleni kuwa mashakani. Ndio maana nafasi hii tumeichukua sisi tuliosoma pale miaka ya nyuma. Wanafunzi wa zamani,
GAZETI hili limezungumza na Mwalimu Mkuu wa Galanos, amekanusha madai yenu. Amesema shule yake inaheshimu dini zote kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi. Mhariri. Ndugu Mhariri NAOMBA nafasi kidogo ili nami nitoe dukukudu langu kuhusu serikali yetu inavyochukulia uzito tofauti haya masuala ya vurugu za kidini. Baada ya hekaheka chungu nzima zilizowakuta ndugu zetu Waislamu wenzetu, za vifo na kujeruhiwa kwa risasi na mabomu na kuadhiriwa akina mama wenzetu kwa kuvuliwa nguo zote mbele ya watoto wadogo, na wakina baba nao halikadhalika watoto wetu kuumizwa vibaya, kulazwa Muhimbili na pingu miguuni kwa muda mrefu bila hata huruma. Serikali haijali hata kuwafungulia kesi walioua na wale waliowatesa watu kwa miezi kadhaa kisha wanawaambia hawana kosa. Tulidhani Mheshimiwa Waziri Mkuu wakati akifunga Bunge angegusia au angetoa msimamo wa serikali wapi! Kama kawaida ya serikali hii juu ya masuala ya Waislamu. Kukaa kimya, na ilivyokuwa limejitokeza suala la Ubalozi wa Marekani ndiyo ikawa sababu ya kupuuziliwa mbali masuala nyeti yanayogusa mustakbali wa nchi, hili likiwa mojawapo. Kweli huu ni utawala wa haki na sheria? Faraja yangu ni kwamba yupo Hakimu wa Mahakimu. Alaysallah Bi Ahkamil-Haki min. Asha Rashid,
Ndugu Mhariri NAOMBA nafasi niweze kueleza yangu machache niliyonayo kuhusu kongamano lililofanyika katika Msikiti wa ANNUUR Kimara Baruti Julai 7, 1998. Ningependa kuunga mkono na kupongeza yote yaliyozungumzwa na Wahadhiri, isipokuwa kulipatikana kasoro chache zilizojitokeza. Katika moja ya kasoro hizo ni kwamba ni pale niliposikia Mhadhir mmoja akisema kwamba polisi hawausiki na dhulma ya Mwembechai kwa sababu wao walitumwa tu hawana budi kutekeleza amri hiyo. Kwa mantiki hiyo nani afikishwe mahakamani? Kama ni Makamba na Ali Ameir peke yao, je, walishika silaha kuwalenga akina Chuki na Ustadh Saleh? Kama sivyo kwanini washtakiwe peke yao? Napenda kusema kwmba wahusika wote wafikishwe mahakamani kuanzia Ali
Ameir mpaka askari waliolenga shabaha "piga yule! Muongeze!"
Ndugu yenu mpenda haki,
|
Serikali yaipongeza Africa Muslim
Agency
Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba
1998:
Athari ya milipuko Dar, Nairobi: Waliokufa
wafikia 258
Wakuu wa mashule waache ubaguzi
ABU AMEENA: Mwana harakati aliyesilimisha wanajeshi 3000 wa Marekani -2 Kisiwa cha Karafuu chageuzwa cha ulevi Twalaban wadhibiti Afghanistan yote Madina yachapisha kitabu cha rejea MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA Maoni: Nyerere kasema kweli Ujamaa
na Ukristo vimeshindwa
Kina Ngatara na wenzake ndio urithi
tulioachiwa na Wakoloni
HOJA BINAFSI: Suala la Mwembechai,
serikali imeumbuka
Kupigwa mabomu misikitini: Waislamu
tumejifunza nini?
MAONI: Hoja za kutofautisha Yesu
na Issa ni udhaifu na ni uzushi mtupu!
Utangazeni Uislamu kwa nguvu
zote – Sheikh Jongo
Salafiya wataka wanawake
wawe macho na vyombo vya habari
Waumini Misufini Morogoro
waazimia kujenga Msikiti
Serikali yatakiwa kuondoa
askari Mwembechai
|