|
|
| Inaendelea kutoka toleo
lililopita...
Abu Ameena: Mwana harakati aliyesilimisha wanajeshi 3000 wa Marekani -2 Nilijiunga na chuo kikuu cha Kiislamu Madina na kupata shahada ya Usuli diin mwaka 1979. Mwaka 1985 nilipata shahada ya pili katika Theolojia ya Kiislamu na mwaka 1994 nikapata Ph.D. Nilifundisha elimu ya Kiislamu na lugha ya Kiarabu katika mashule binafsi mjini Riyadh kwa muda wa miaka 10. Na miaka mitatu baadae nikawa Mhadhiri wa Islamic Studies katika Chuo Kikuu cha Kiislamu Jijini Cotabato nchini Philippines. Wakati huo huo nikiwa mhadhiri katika chuo cha Kimarekani katika falme za Kiarabu. Nilivyo fanya Daawah katika kambi za jeshi la Marekani Ghuba. Wakati wa vita vya Ghuba, nilifanya kazi ya Da’awah miongoni mwa askari wa Marekani kupitia idara ya mambo ya dini ya kikosi cha anga cha jeshi hilo. Askari wa Marekani kama ilivyo kwa watu wa Magharibi walikuwa wakiuelewa vibaya Uislamu. Wanajeshi hao walipewa amri ya kutosogea futi 10 kutoka misikitini. Kinyume na amri hiyo sisi tuliwachukua hadi misikitini. Walivutiwa mno na jinsi mazingira ya ndani ya misikiti yalivyo. Hawakuona humo jambo lolote la kustaajabisha zaidi ya miswala. Wakati walipofika nchini Saudi Arabia walishangazwa kuwaona wanawake wa Kiislamu wakiwa katika vazi la Hijab. Waliwapa jina la utani UBO (Unidentified Black Objects) yaani "maumbile meusi yasiyo tambulika." Lakini kadri walivyoendelea kuzoea mazingira ya Saudi Arabia ndivyo walivyozidi kufunguka macho na fahamu. Walishuhudia ukarimu waliotendewa na mabedui (watu wa jangwani). Mabedui hao walikuwa wakitembelea mahema ya askari hao wa Marekani na kugawa tende na maziwa. Askari hao hawakuuona ukarimu huu Korea, Japan wala mahali pengine popote pale ambako jeshi hilo limekuwa na vituo kwa miongo kadhaa. Kutokana na mazoeano ya miezi kadhaa na vikosi hivyo, baada ya vita kumalizika nilipata fursa ya kwenda Marekani ambako nilifungua ukurasa mpya wa Uislamu katika idara ya ulinzi ya nchi hiyo. Nakisia askari wapatao 3000 wa jeshi la Marekani wamesilimu, wengi wakiwa wamesilimu kipindi kile kile cha vita Ghuba. Niamini nikisema kwamba Saudi Arabia ni mahali pekee duniani ambako askari wa Kimarekani wameshindwa kuacha watoto wa vita", hali kadhalika pamoja na ulevi uliokithiri kwa askari hao, pombe ilinywewa kwa nadra. Nikiwa India Kwa mara ya kwanza nilizuru India mwaka 1991. Hii ilikuwa wakati nafanya utafiti. Nchini India nilikutana na Waislamu wa Jimbo la Kaskazini. Waislamu niliokutana nao walikuwa wamezama kwenye mambo ya ushirikina. Ushirikina ulifanywa sehemu ya ibada. Mara yangu ya pili kutembelea India ilikuwa mwaka jana (1997), safari hii ilinichukua hadi mji wa Karala. Mjini Karala kuna jumuiya za Kiislamu kama Jamaat Islam na Islamic Research Foundation ambazo zinafanya kazi nzuri ya Da’awah. Da’awah ya Jumuiya hizi imelenga vyuo vikuu na wasomi wengine katika taasisi mbali mbali ipo pia Jumuiya ya Tabligh ambayo harakati zake zimeelekea zaidi misikitini. Kwa hali niliyoiona India, ningependa kushauri kwamba ipo haja kwa jumuiya
za Kiislamu kushirikiana.
|
Serikali yaipongeza Africa Muslim
Agency
Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba
1998:
Athari ya milipuko Dar, Nairobi: Waliokufa
wafikia 258
Wakuu wa mashule waache ubaguzi
ABU AMEENA: Mwana harakati aliyesilimisha wanajeshi 3000 wa Marekani -2 Kisiwa cha Karafuu chageuzwa cha ulevi Twalaban wadhibiti Afghanistan yote Madina yachapisha kitabu cha rejea MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA Maoni: Nyerere kasema kweli Ujamaa
na Ukristo vimeshindwa
Kina Ngatara na wenzake ndio urithi
tulioachiwa na Wakoloni
HOJA BINAFSI: Suala la Mwembechai,
serikali imeumbuka
Kupigwa mabomu misikitini: Waislamu
tumejifunza nini?
MAONI: Hoja za kutofautisha Yesu
na Issa ni udhaifu na ni uzushi mtupu!
Utangazeni Uislamu kwa nguvu
zote – Sheikh Jongo
Salafiya wataka wanawake
wawe macho na vyombo vya habari
Waumini Misufini Morogoro
waazimia kujenga Msikiti
Serikali yatakiwa kuondoa
askari Mwembechai
|