AN-NUUR
Na.162 Rabiul Thani 1419, Agosti 14 - 20, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Utangazeni Uislamu kwa nguvu zote – Sheikh Jongo

Na Badru Kimwaga 

WAISLAMU nchini wametakiwa kutoogopa kumtangaza Mtume Muhammad (s.a.w) na kuitangaza dini ya Kiislamu bila woga na pia kutangaza wazi kuwa hakuna dini nyingine zaidi ya Uislamu itakayomuokoa mtu siku ya hukumu. 

Maagizo hayo yametolewa na Imam wa Msikiti wa Manyema, Sheikh Hamid Jongo, alipokuwa akihutubia waumini msikitni hapo wakati wa swala ya Ijumaa, iliyofanyika katika Msikiti huo, Jijini. 

Sheikh Jongo alisema kuwa Waislamu watangaze kwa nguvu na bila woga kuwa hakuna Mtume zaidi ya Muhammad (s.a.w) katika zama hizi, na pia dini ya Kiislamu tu, ndio inayotumbulika kwa Mwenyezi Mungu na kwamba kuacha kutangaza hivyo ni kuenda kinyume na maamrisho ya Mungu. 

Aliongeza kuwa, Waislamu wasiogope kutangaza hivyo kwa sababu, wasiokuwa Waislamu mbona wanatangaza dini zao ambazo mbele ya Mungu ni hasara, iweje wao (Waislamu) waogope. 

"Watu wanashindwa kumtangaza Mtume Muhammad juu ya mazazi yake kwa madai ni bidaa, huku wakisisitiza kuwa zipo dini nyingine, lakini katika mashindano ya urembo, sijui nini ya sura mbaya wao ndio watu wa mbele tena Waislamu, huko sio bidaa ila kutaja Mtume na kutangaza Uislamu ni kosa, wapi tunapokwenda Waislamu, amkeni acheni kutekwa na wasio Waislamu na mkajiona bado Waislamu ilhali mshajivua ", alisema Sheikh Jongo. 

Pia alisisitiza waumini kuwa na uvumilivu baina yao na kuachana na miparaganyiko baina yao kwa madhehebu au itikadi za kisiasa, kwani, ni kwenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu na Mtume. 

Sheikh Jongo aliongeza kuwa Waislamu waamke na wajisaidie wenyewe katika nyanja zao ziwe za kijamii au kiuchumi. 

 
Salafiya wataka wanawake wawe macho na vyombo vya habari
Na Mwandishi Wetu

Wanawake Waislamu Jijini Dares Salaam wametoa wito kwa Waislamu kote nchini kuwa na msimamo madhubuti katika kuibaini dini yao na wasikubali kurubuniwa. 

Aidha wametakiwa kutekeleza barabara kwa vitendo ujumbe wa Mtume (S.T.W.) huku wakiwalea watoto wao kwa kizingatia maadili ya Uislamu. 

Hayo yametolewa kama sehemu ya maazimio mwishoni mwa kongamano la uzawa wa Mtume (s.a.w.) katika msikiti wa Idrisa Ilala Agosti 8. 

Kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na wanawake Waislamu wapatao 500 liliwakumbusha akina mama kwamba salama na heshima yao iko katika kuutekeleza Uislamu katika kila kipengele cha maisha bila ya kuchagua. 

Akitoa mada katika kongamano hilo Ukht Uzale Mwanjie alibainisha kwamba ili Waislamu wafanikiwe katika harakati zao ni lazima wawe na imani madhubuti isiyoyumba; wawe watendaji wa kudumu na wakweli katika kujitoa muhanga na kushikaman pamoja katika hilo. 

Wakati huo huo, wanawake Waislamu wa ‘Salaffiyah" wakishirikiana na DAMUSSA idara ya wanawake walifanya semina hivi karibuni kuwakumbusha akinamama na mabinti wa Kiislamu wajibu wao katika Uislamu. 

Katika semina hiyo iliyofanyika katika Shule ya Kiislamu ya Ubungo. 

Suala la vyombo vya habari na jinsi vinavyotumika kuwadhalilisha wanawake lilijadiliwa kwa undani. 

Ilielezwa kwamba matangazo mengi yanayotolewa ni yenye kumdhalilisha mwanamke na yanayotoa mchango ukubwa kuporomosha maadili ya jamii. 

Pamoja na azimio la kusoma kwa bidii ili baadae kuiongoza na kuisaidia jamii, lilipitishwa pia azimio la kupiga vita maadili mabaya. 
 
 

Waumini Misufini Morogoro waazimia kujenga Msikiti

Na Rajab Rajab, Morogoro 

Waumini wa Kiislamu waishio eneo la Misufini,Chamwino mjini hapa wameamua kujenga Msikiti katika eneo hilo baada ya kukosekana kwa muda mrefu. 

Akiwasilisha taarifa ya kamati ya muda inayoshughulikia suala hilo katika kikao cha Waislamu na eneo hilo Jumapili iliyopita, Katibu wa kamati hiyo, Fadhili R. Mshana amesema kukosekana kwa Msikiti katika eneo hilo kumepelekea vijana wengi kujiingiza katika vitendo viovu kama vile kucheza kamari, kuvuta bangi na wizi, ambapo kungekuwepo Msikiti ingekuwa rahisi kuwaelimisha vijana hao na kukemea vitendo vyao viovu. 

Aliendelea kusema Katibu huyo kuwa kamati yake iliweza kufanya sensa ya Waislamu waishio eneo hilo na kubainika kuwa kuna Waislamu 300 wanawake na wanaume, na kuongeza kuwa eneo hilo halina sehemu ya kufanyia ibada kwa Waislamu lakini madhehebu mengine zipo sehemu hizo. 

Baada ya kutolewa taarifa hiyo, kamati ya muda ambayo ilikuwa inaongozwa na Hassan Amri, A. Mgaya, Mussa Ismaili, Fadhil R. Mshana, Kassim Rashid na Mzee Mohamed Fusi ilivunjwa na kuundwa kamati ya kudumu ambayo itafuatilia suala hilo na mengine kwa kina. 

Kamati hiyo ya kudumu inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Mussa Ismaili Mkwinda, Fadhili R. Mshana (Katibu) na Kassim Rashid (Mweka Hazina). 

Aidha, kikao hicho kilichagua viongozi kina mama ambao watashirikiana na kamati hiyo, waliochaguliwa ni Pili Seburi (Mwenyekiti), Mama Abdallah (Katibu) na Asha Igilo (Mtunza Hazina) Vile vile kamati hiyo itakuwa na wajumbe wake ambao ni Mama Omar pamoja na Maimuna Peter ambapo viongozi huo umeanza kazi mara moja. 

Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na zaidi ya waumini 50, wanaume na wanawake kiliwataka waumini wake washirikiane na viongozi hao katika kutafuta eneo la kujenga Msikiti pamoja na madrasa ya watoto na watu wazima. 
 

Serikali yatakiwa kuondoa askari Mwembechai

Na Badru Kimwaga 

WAUMINI waswalio katika Msikiti wa Mwembechai, wameitaka serikali kuliondoa jeshi la polisi lililovamia msikiti huo kwa muda wa miezi sita sasa. 

Waumini hao kwa nyakati tofauti wiki iliyopita na mwanzoni mwa wiki hii, wamesema kuwa kuwepo kwa askari hao huchangia kuwafanya waumini kutoswali msikitini hapo na pia kukwamisha maendeleo ya elimu ndani ya msikiti huo, kwa vile madarasa yamefungwa kwa woga wa wanafunzi. 

Wakiongea kwa masharti ya kuficha majina yao, waumini hao ambao pia wako walio katika kamati ya msikiti, wamesema kuwa wamechoshwa na ulinzi huo usio na maana bali kuzorotesha msikiti huo ambao ulikuwa maarufu na wenye kudhuriwa na waumini wengi kabla ya polisi kuvamia mwanzoni mwa mwaka huu. 

Mmoja wa wanakamati aliyekataa kutaja jina kwa sababu za kiusalama, amedai kuwa hata wenyewe wadhamini wa msikiti huo wameonyesha kuchoshwa na kuwepo kwa askari hao, ambao hushinda msikitini hapo bila kazi zozote na hasa kufanya msikiti ukose waumini na pia kuzorotesha maendeleo ya kielimu. 

Aliongeza kuwa licha ya kufanyia ukarabati madrasa na maeneo yaliyokuwa yakitolewa elimu kwa akinamama, lakini wameshindwa kuanzisha darasa hizo kutokana na kutokuwa na waumini na vilevile 

Alihoji ni kwa vipi Serikali isiwaondoe askari hao ili kuweza kuurudisha msikiti katika hali yake ya kawaida. 

"Hata watoto wanashindwa kuja msikitini kwa ajili ya askari hao kwa nini serikali isiwaondoe, wanafanya nini maeneo haya na hakuna ukosefu wa amani, msikiti umekuwa mkiwai serikali iwaondoe askari hao, tunaomba walisikie hili....", alisisitiza muumini huyo. 

Hivi karibuni mzee wa msikiti huo,aliwahi kusimama mara baada ya swala na kulalama kuwa waumini hawachangi fedha wapitishapo kikapu, lakini sababu hasa ni uchache wa watu na wengi wakiwa ni wazee wasio na kazi, kwani wengi wamestaafu makazini. 
 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Serikali yaipongeza Africa Muslim Agency 
Na Mwandishi Wetu, Moshi 

Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba 1998: 
Afisa Elimu akiri kutaka orodha ya wanafunzi 
Na Mwandishi Wetu, Morogoro 

Athari ya milipuko Dar, Nairobi: Waliokufa wafikia 258 
Na Mwandishi Wetu 

Wakuu wa mashule waache ubaguzi 
Na Mwandishi Wetu 

ABU AMEENA: Mwana harakati aliyesilimisha wanajeshi 3000 wa Marekani -2 

Kisiwa cha Karafuu chageuzwa cha ulevi 

Twalaban wadhibiti Afghanistan yote 

Madina yachapisha kitabu cha rejea 

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA 

Maoni: Nyerere kasema kweli Ujamaa na Ukristo vimeshindwa 
Na Abdul Gullam 

Kina Ngatara na wenzake ndio urithi tulioachiwa na Wakoloni 
Na J. Hussein 

HOJA BINAFSI: Suala la Mwembechai, serikali imeumbuka 
Na Mwinjilisti Kamara Kusupa 

Kupigwa mabomu misikitini: Waislamu tumejifunza nini? 
Na RAJAB RAJAB

MAONI: Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu na ni uzushi mtupu!
Na Muhibu Said

Utangazeni Uislamu kwa nguvu zote – Sheikh Jongo
Na Badru Kimwaga

Salafiya wataka wanawake wawe macho na vyombo vya habari
Na Mwandishi Wetu

Waumini Misufini Morogoro waazimia kujenga Msikiti
Na Rajab Rajab, Morogoro

Serikali yatakiwa kuondoa askari Mwembechai
Na Badru Kimwaga

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi 

Masomo 

Chakula na Lishe  
 
 

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita