AN-NUUR
Na.162 Rabiul Thani 1419, Agosti 14 - 20, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 TAHARIRI
S.L.P. 55105, SIMU 181365, DSM
 
Tathmini ya Mchango wa Mashirika ya Dini

Kwa mara nyingine Serikali imetoa pongezi na kuzishukuru taasisi za kidini kwa mchango mkubwa zinazotoa kuboresha huduma za elimu, afya na jamii kwa ujumla. Kama alivyozungumza Afisa Elimu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa akifungua kituo cha Markaz El-Hudaa; huduma hizi ni za thamani kubwa kwa Watanzania na hapana budi kuwashukuru wahisani wahusika. 

Tungependa tuungane na Serikali katika kutambua na kuthamini misaada katika huduma za jamii zinazotolewa na mashirika ya dini na hivyo kuyapa moyo yazidishe juhudi zake. 

Aidha pamoja na kwamba yapo mashirika mengi ya dini yanayofanya shughuli mbalimbali kuwasaidia Waislamu na Watanzania kwa ujumla; tungeyaomba yaige mfano wa Africa Muslim Agency ambayo imelenga katika ile miradi ambayo hasa ndio kilio cha Waislamu. 

Suala la kujenga na kuendesha mashule, mahospitali na miradi mingine mikubwa kama hiyo ni suala linalohitaji nguvu kubwa inajumuisha misaada toka sehemu mabalimbali. 

Umuhimu wa misaada hiyo ya mashirika ya dini unapata nguvu zaidi ikizingatiwa kwamba uwezo wa Serikali yetu kutoa huduma muhimu kwa jamii unazidi kupungua mwaka hadi mwaka. 

Na pengine ni kwakuzingatia ukweli huo Mabaraza ya Kikristo yaliingia mkataba na Serikali ya Tanzania, maarufu kwa ‘Memorandum of Understanding" ambapo misaada ya Kielimu na Afya kwa Tanzania toka kwa Serikali za nchi kama Ujerumani itakuwa ikipitia katika mashirika ya Kikristo. 

Aidha Serikali ya Tanzania inawajibika kuyaombea misaada mashirika hayo ya Kikristo toka nchi za nje. Tunaimani kwamba kwa msimamo huu wa Serikali Mashirika ya Kidini toka nchi mbalimbali za Ulaya; Arabuni, Asia n.k. yataitumia fursa hii kuwahudumia waumini wao na wananchi kwa ujumla ili kuimarisha imani zao na kuboresha maisha yao. 

Kwa upande mwingine tungependa tutoe wito kwa wananchi kwamba wawe ni wenye kuenzi na kutunza miradi na huduma mbalimbali zinazotolewa na mashirika ya dini ili lengo lililokusudiwa liweze kufikiwa. 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Serikali yaipongeza Africa Muslim Agency 
Na Mwandishi Wetu, Moshi 

Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba 1998: 
Afisa Elimu akiri kutaka orodha ya wanafunzi 
Na Mwandishi Wetu, Morogoro 

Athari ya milipuko Dar, Nairobi: Waliokufa wafikia 258 
Na Mwandishi Wetu 

Wakuu wa mashule waache ubaguzi 
Na Mwandishi Wetu 

ABU AMEENA: Mwana harakati aliyesilimisha wanajeshi 3000 wa Marekani -2 

Kisiwa cha Karafuu chageuzwa cha ulevi 

Twalaban wadhibiti Afghanistan yote 

Madina yachapisha kitabu cha rejea 

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA 

Maoni: Nyerere kasema kweli Ujamaa na Ukristo vimeshindwa 
Na Abdul Gullam 

Kina Ngatara na wenzake ndio urithi tulioachiwa na Wakoloni 
Na J. Hussein 

HOJA BINAFSI: Suala la Mwembechai, serikali imeumbuka 
Na Mwinjilisti Kamara Kusupa 

Kupigwa mabomu misikitini: Waislamu tumejifunza nini? 
Na RAJAB RAJAB

MAONI: Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu na ni uzushi mtupu!
Na Muhibu Said

Utangazeni Uislamu kwa nguvu zote – Sheikh Jongo
Na Badru Kimwaga

Salafiya wataka wanawake wawe macho na vyombo vya habari
Na Mwandishi Wetu

Waumini Misufini Morogoro waazimia kujenga Msikiti
Na Rajab Rajab, Morogoro

Serikali yatakiwa kuondoa askari Mwembechai
Na Badru Kimwaga

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi 

Masomo 

Chakula na Lishe  

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita