|
|
|
KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA, UTANGULIZI MISINGI YA KATIBA Kwa kuwa sisi Wananchi wa Shirikisho wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki udugu na amani; Na kwa kuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasi ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumisha na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu: Kwa hiyo, basi, Katiba hii Imetungwa na wananchi, kwa kura ya maoni
Kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha
kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasi.
SURA YA KWANZA SHIRIKISHO
SEHEMU YA KWANZA SHIRIKISHO Kutangaza Shirikisho 1. Tanzania ni nchi moja na ni Shirikisho. Eneo la Jamhuri la Shirikisho 2.(1) Eneo la Shirikisho ni eneo lote la Tanganyika na eneo la Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzanyika na Zanzibar inaimiliki chini ya Sheria za Kimataifa. Bunge 2. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Shirikisho au Serikali ya Zanzibar, au Serikali ya Tanganyika, Waziri Mkuu wa Serikali ya Zanzibar na wa Serikali ya Tanganyika wanaweza kugawa maeneo yao katika mikoa, wilaya baada ya kupat amaoni ya wananchi, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge la Tanganyika au Bunge la Zanzibar. Bunge Na kwamba maamuzi ya kugawa nchi katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo yatakayofanywa na Waziri Mkuu anayehusika kama ilivyoelezwa katika Ibara hii, itakuwa ni lazima yafikishwe katika Bunge la Tanganyika au Bunge la Zanzibar kwa jinsi itakavyokuwa kwa uthibitisho. Tangazo la nchi yenye mfumo wa vyama vingi 3. (1) Jamhuri ya Shirikisho ni nchi ya kidemokrasia yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. 2. Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa Tanzania yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanganyika na sheria zilizotungwa na vyombo husika kwa ajili hiyo. Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi 4.(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Shirikisho zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo vitatu vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo vitatu vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki, na pia vyombo vitatu vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma. (2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya Shirikisho, na Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar na vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Mahakama ya Rufaa ya Shirikisho, Idara ya Mahakama ya Tanganyika na Zanzibar na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga Sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge la Shirikisho, Mabunge ya Tanganyika na Zanzibar. (3)Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Shirikisho, na Serikali ya Zanzibar, na Serikali ya Tanganyika, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Shirikisho kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza iliyoko mwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na mambo yasiyo ya Shirikisho, ambayo ni mambo mengine yote ambayo hayakutajwa katika nyongeza hiyo na ambayo yametajwa katika Nyongeza ya pili katika Katiba hii. (4) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti yaliyomo katika Katiba hii, (5) Bunge na Mahakama vitakuwa ni vyobo huru katika utendaji wa kazi zake na Serikali ya Shirikisho itawajibika kuchukua hatua zote za lazima kuhakikisha kwamba Bunge na Mahakama zinafanya kazi zake kwa ufanisi na malengo yaliyokusudiwa na Katiba hii.
SEHEMU YA PILI MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI Ufafanuzi 5. Katika sehemu hii ya sura hii, isipokuwa kama maelezo yahitaji vinginevyo, neno "Serikali" maana yake ni pamoja na Serikali ya Shirikisho, na Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar, Serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote. Matumizi ya masharti ya Sehemu ya Pili 6. (1) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), Serikali vyombo vyake vyote na watu wote au mamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa kuzingatia, kutilia maanani na kutekeleza masharti yote ya sheemu hii ya Sura hii. Serikali na watu 7.(1) Shirikisho la Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasi na haki ya kijamii, na kwa hiyo (a) Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali zitapata madaraka na mamlaka zake zote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii. (b) Lengo kuu la Serikali zote litakuwa ni ustawi wa wananchi; (c) Serikali zitawajibika kwa wananchi; na (d) Wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali zao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii. (2) Muundo wa Serikali ya Shirikisho na Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar, au wa chochote kati ya vyombo vyake na uendeshaji wa shughuli zake, utatekelezwa kwa kuzingatia umoja wa Shirikisho na haja ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa. 8. Lengo la Katiba hii ni kudumisha udugu na amani katika Shirikisho. Kwa hiyo, Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha- (a) kwamba utu na haki zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa; (b) kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa; (c) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufa aya wananchi wote kwa jumla. (d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa; (e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake; (f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu na makubaliano ya kudumisha Haki za Binadamu ya Umoja wa nchi Huru za Afrika na yale ya Umoja wa Mataifa; (g) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila ya kujali rangi, kabila , dini au hali ya mtu; (h) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaoondolewa nchini; (I) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi. (j) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia. Wajibu wa kufanya kazi, kupata elimu na nyinginezo 9.(1) Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa wajibu wamtu kufanya kazi haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi.Bila kuathiri haki hizo, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake. (2) Kila mtu anao wajibu wa kujielimisha, na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake. (3) Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo.
SEHEMU YA TATU HAKI NA WAJIBU MUHIMU Haki ya Usawa Usawa wa binadamu 10 (1) Binadamu wote wana asili moja huzaliwa huru na wote ni sawa. (2) kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake Usawa mbele ya Sheria 11.(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria. (2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Shirikisho au inayotumika nchini kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake. (3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na mahakama na vyombo vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na Sheria au kwa mujibu wa sheria. (4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi. (5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, jinsia, kabila , pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanyiwa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima. (6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia msiingi kwamba- (a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi na mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika; na kwamba shauri hilo litasikilizwa bila kuchelewa; (b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo; (c) ni marufuku kwa mtu kukamatwa na kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chochote ambacho alipokitenda hakikuwa ni kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwa adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa; (d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi na uendeshaji wamambo ya jinai na katika shughuli nyingine ambazo mtu anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; (e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha. Haki ya kuishi
Haki ya kuwa hai 12. Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake. Haki ya Uhuru wa watu binafsi 13. (1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru (2) kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang’anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu- (a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria inayohusu upelelezi wa makosa ya jinai au (b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai. Haki ya faragha na ya usalama wa mtu 14. (1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi. (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii , Bunge la shirikisho na Mabunge ya Tanganyika na Zanzibar itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama wa nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii. Uhuru wa mtu kwenda atakako 15. (1) Kila raia wa Shirikisho anayo haki ya kwenda kokote katika Shirikisho na kuishi katika sehemu yoyote , kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Shirikisho. Itaendelea toleo lijalo...
|
Serikali yaipongeza Africa Muslim
Agency
Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba
1998:
Athari ya milipuko Dar, Nairobi: Waliokufa
wafikia 258
Wakuu wa mashule waache ubaguzi
ABU AMEENA: Mwana harakati aliyesilimisha wanajeshi 3000 wa Marekani -2 Kisiwa cha Karafuu chageuzwa cha ulevi Twalaban wadhibiti Afghanistan yote Madina yachapisha kitabu cha rejea MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA Maoni: Nyerere kasema kweli Ujamaa
na Ukristo vimeshindwa
Kina Ngatara na wenzake ndio urithi
tulioachiwa na Wakoloni
HOJA BINAFSI: Suala la Mwembechai,
serikali imeumbuka
Kupigwa mabomu misikitini: Waislamu
tumejifunza nini?
MAONI: Hoja za kutofautisha Yesu
na Issa ni udhaifu na ni uzushi mtupu!
Utangazeni Uislamu kwa nguvu
zote – Sheikh Jongo
Salafiya wataka wanawake
wawe macho na vyombo vya habari
Waumini Misufini Morogoro
waazimia kujenga Msikiti
Serikali yatakiwa kuondoa
askari Mwembechai
|