|
Na. 045 Jumatano Aprili 26 - Mei 2, 2000 |
|
|
|
|
|
Raoul Shungu apigwa 'Dafrao' Na Mwandishi Wetu KOCHA Mkuu wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Raoul Shungu amesisimamishwa kufundisha soka ndani na nje ya nchi na chama cha soka nchini kwa miezi sita kutokana na utovu wa nidhamu. Shungu amekumbwa na dhoruba hiyo kufuatia kitendod chake cha kutaka kumvamia mwamuzi wa mchezo kati ya timu yake na Kariakoo ya Lindi, Andrew Kiloyi kwa madai ya kuiumiza Yanga. Mchezo huo ulikwisha kwa sare ya 2-2. Akithibitisha adhabu hiyo jijini jana, Mwenyekiti wa FAT, Muhidini Ndolanga amesema, adhabu hiyo inandamana na faini ya shilingi laki tano. Kadhalika, FAT imeipipiga faini Klabu ya Yanga yenye thamani ya shilingi laki tano kwa kushindwa kuwadhibiti wafuasi wake waliokuwa na dhamira ya kujeruhi. Vile vile Ndolanga ambaye anadaiwa kuathirika
na vurugu hizo amesema, kuwa adhabu hiyo itajadiliwa kwa kina Ijumaa ijayo
na Kamati ya Utendaji ya FAT ili itoe baraka zake. Hata hivyo Yanga wemepinga
hukumu hiyo.
LIGI KUU TANZANIA BARA
WASHABIKI wanaodhaniwa kuwa wa klabu kongwe nchini Yanga, juzi katika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam walianzisha vurumai zilizopelekea kushambuliwa kwa jukwaa la wageni rasmi alipokuwa ameketi Naibu Waziri wa Serikali ya Awamu ya Tatu na kumfanya atoweke kwa usalama wake. Mudhihir Mudhihir ambaye Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, katika sakata hilo alikuwa pamoja na Mwenyekiti wa chama chama cha soka nchini (FAT), Muhidin Ndolanga na mjumbe wa chama hicho, Twalib Twalib. Mudhihir na Ndolanga licha ya nyadhifa zao pia walikuwepo Uwanjani hapo kushuhudia timu ya nyumbani Kariakoo ya Lindi iliyokuwa ikimenyana na Yanga ya Dar es Saaam zilizofungana 2-2. Kwanza kabisa washabiki hao walitaka 'kumfanyia' mwamuzi Andrew Kiloyi wa Iringa kwa madai ya kuibeba Kariakoo na iliposhindikana wakaamua kuwashughulikia waheshimiwa hao. Katika shughuli hiyo, washabiki walitumia mawe, chupa, vipande vya miti na vibao vya kubadilishia wachezaji huku waheshimiwa wakijifunika viti na kutimka kunako usalama. Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja hali zao. Akizungumza ofisini kwake jijini jana na NASAHA, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Abbas Tarimba alioonyesha kusikitishwa kwake na tukio hilo lililotokea akiwa safarini lakini akasita kuomba radhi kwa niaba ya watu wake. "Sio rahisi kuomba radhi, kwani sina ushahidi kama kweli waliofanya vurugu zile ni washabiki wa Yanga kwa nini wasiwe wa Klabu nyingine yoyote kama Simba ambao wanaweza kufanya hivyo ili kuipaka matope Yanga", amehoji Aidha, baadhi ya washabiki wa soka jijini wamemtaka Mwenyekiti wa FAT Muhidin Ndolanga kumuomba radhi Waziri kutokana na usumbufu alioupata ambao ulisababishwa na udhaifu wa refa aliyepangwa na FAT.
WANACHAMA wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam wamempongeza Msajili wa vyama na vilabu nchini Ronald Thadeo kwa alivyoushughulikia mgogoro wao na kuumaliza kwa amani. Simba ilikuwa katika mgogoro mkubwa wa uongozi uliodumu kwa karibu mwaka mmoja kitu ambacho kilimfanya Msajili aingilie na kuwafungia kuongoza Yusufu Hazali na Khalfani Matumla waliokuwa Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Simba. Anaripoti Mwandishi Wetu. Pia wamemsifu alivyosimamia uchaguzi wao mkuu uliowasimika uongozini Juma Salum mwenyekiti na Katibu Mkuu Kassim Dewaji. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Serikali iache udini, kuwagawa wananchi - Sheikh Mbukuzi Wakati
Kanisa Katoliki likitoa miongozo ya kisiasa:
Hakuna maendeleo bila Demokrasia - Lipumba MPASHO NASAHA
HABARI
‘Suala la kuirekebisha jamii lisiachwe mikononi mwa Serikali pekee’ Jiandikisheni na pigeni kura -Balozi Tanzania
kufutiwa madeni:
Ushauri Nasaha
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Lishe
RIWAYA
v |
|
|
|
|