|
Na. 045 Jumatano Aprili 26 - Mei 2, 2000 |
|
|
|
|
|
Chama cha Mapinduzi na sera za maendeleo (1)
UMASKINI unaweza kuutaja kuwa ni hali duni ya maisha ya wananchi inayosababishwa na ukosefu wa ajira, ukosefu wa uwezo wa kupata mahitaji muhimu kama vile elimu, chakula bora, matibabu kwa urahisi na kwa kiwango cha kuridhisha pamoja na nyumba bora. Ili kupambana na hali hiyo, serikali ya awamu ya kwanza ikatangaza kampeni ya Kitafia iliyoitwa "UHURU NA KAZI" kwa lengo la kusisitiza umhimu wa kazi kwa ajili ya kujiletea maendeleo na heshima ya mtu. Kwa ajili ya kupanua na kuongeza kipato cha wananchi, wakulima na taifa kujitosheleza kwa chakula ikaanzishwa kampeni ya "siasa ni kilimo." Kwa ajili ya kuboresha maisha ya jamii, serikali ikaanzisha kampeni nyingine kwa jina la "Mtu ni Afya." "Elimu kwa wote" (UPE) ni kampeni nyingine iliyoanzishwa kwa lengo la kuongeza idadi ya wanaojua kusoma, hii ilikwenda sambamba na kampeni ya "Elimu ya watu wazima." Hatujakaa vizuri ikaanzishwa kampeni nyingine iliyojulikana kwa jina la "Nyumba bora za kisasa." Kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi wote nchini Tanzania wanakuwa na nyumba bora kwa matumizi yao. Kampeni zote hizi zilianzishwa na vigogo wa chama tawala, bila kuwashirikisha wananchi, wao walitakiwa kutekeleza tu. Katika makala hii, tutatumia vigezoambavyo wataalamu wa elimu ya sayansi ya jamii huvitumia katika kupima mafanikio katika kupambana na umaskini ili tuone kama kampeni hizo zilifanikiwa ama la. Moja ya vigezo unavyotumika ni idadi ya wananchi wanaojua kusoma na kuandika ndani ya nchi. Katika miaka ya 1980 idadi ya wananchi wanaojua kusoma na kuandika ilifikia 90 pasenti na sasa imeshukakwa asilimia 68 pasenti. Jambo linaloashiria ongezeko kubwa la wananchi wasiojua kusoma na kuandika, na kwa hivyo ni ishara pia ya kuongezaka kwa umaskini miongoni mwa jamii. Upatikanaji wa maji safi na ya kutosha kwa wananchi, ni kigezo kingine kinachotumika katika kupima mafanikio ya mapambano dhidi ya umaskini. Kwa wananchi walio wengi hapa nchini upatikanaji wa maji kwa urahisi ni anasa, tunaambiwa na wataalamu kuwa ni pasenti 11 tu ya wananchi ndio wanaopata maji ya bomba majumbani na idadi iliyobaki ya wananchi hupata maji kuanzia umbali wa kati ya kilometa mbili hadi kumi na tano, tena maji ambayo hata usalama wake ni wa katilia mashaka. Ukosefu wa huduma bora za afya ni kigezo kingine cha kudhihirisha kiwango cha umaskini wa wananchi. Wataalamu wa sayansi ya jamii wanaeleza kwamba kulingana na idadi ya watu nchini ambayo inakadiriwa kuwa ni zaidi ya milioni 30, kila hospitali au kituo cha afya kimoja kilichopo nchini huhudumia wastani wa wananchi 7400, kitanda kimoja kwa kila wagonjwa 1000 na daktari mmoja (1) kwa kila wananchi 33, 300 na kwa maana hii Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo bado zinahangaishwa na matibabu ya magonjwa ambayo yamekwisha kutokomezwa katika nchi nyingi duniani. Idadi ya watoto wanao kufa ni 84 kwa kila watoto 1000 ikilinganishwa na vifo vya watoto saba (7) katika kila 1000 wanaozaliwa katika nchi zilizoendelea. Kwa sababu ya umaskini uliokothiri, wananchi wengi hawapati chakula bora na kwa hivyo, utapiamlo nao ni tatizo kubwa hapa nchini, hasa kwa wananchi waishio vijijini ambao hula chakula cha aina moja tu kila uchao. Ukosefu wa ajira ni kielelezo kingine cha umaskini nchini, tunaambiwa kwamba kila mwaka kiasi cha wanafunzi 300,000 humaliza, kufuzu na wengine kuhitimu masomo yao, lakini idadi ya wanaoajiriwa ni 30,000 pekee. Maisha yanakuwa magumu kwa wananchi wengi, lakini vijijini maisha yanakuwa magumu zaidi na kwa hivyo idadi kubwa ya watoto wanaomaliza masomo darasa la saba hulazimika kukimbilia mijini ambako nako pia hakuna ajira na kusababisha ongezeko la idadi ya watoto wa mitaani na wazururaji mijini. Ni kweli kwamba ongezeko la vibaka, wezi, majambazi na wanawake malaya mijini ni ushahidi wa kuporomoka kwa maadili, lakini kwa kiwango kikubwa hali hiyo inasababishwa pia na umaskini uliokithiri miongoni mwa jamii. Na jambo hili ni hatari sana kwa amani na utulivu wa nchi yetu, ukiachilia mbali kuporomoka kwa maadili kunakoendelea kwa kasi ya kutisha. Ushahidi mwingine wa umaskini tulionao ni kiwango kidogo cha kipato cha wananchi walio wengi, makadirio yaliyofanywa mwaka 1995 yalionyesha kuwa kiwango cha chini ambacho mtu angestahili kupata kwa mwezi ni Shs. 73,877/- na hiki ni kiwango ambacho kilikadiriwa kumtosha mtu mmoja tu, achilia mbali mtu mmoja na mkewe na mtoto mmoja. Kwa maana hii zaidi ya pasenti 50 ya wananchi wanaishi kwa kubahatisha. Umaskini katika nchi nyingi barani Afrika husababishwa na uongozi mbaya, kutowajibika, ubinafsi, na ufujaji wa pato la taifa unaofanywa na viongozi walioko madarakani kwa visingizio mbali mbali pamoja na ukosefu wa utashi wa kisiasa wa viongozi hao katika kuboresha maisha ya wananchi walio wengi. Kwa miaka mingi sasa, viongozi wa chama tawala wamekuwa wakisema kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa taifa letu, na jambao hili lilipata pia kusisitizwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mahojiano yake na televisheni ya CNN alipokuwa Atlanta, Georgia huko Marekani tarehe 23 Septemba 1999, aliposema, kimsingi uchumi wa Tanzania umejikita katika kilimo kinachoendeshwa kwa sehemu kubwa na wakulima wadogo wadogo nchini. Sasa kama huu ndio ukweli, serikali ya Chama Cha Mapinduzi ina mikakati gani ili kuboresha hali na kipato cha wananchi ambao zaidi ya pasenti 85 ni wakulima? |
YALIYOMO
TAHARIRI
Serikali iache udini, kuwagawa wananchi - Sheikh Mbukuzi Wakati
Kanisa Katoliki likitoa miongozo ya kisiasa:
Hakuna maendeleo bila Demokrasia - Lipumba MPASHO NASAHA
HABARI
‘Suala la kuirekebisha jamii lisiachwe mikononi mwa Serikali pekee’ Jiandikisheni na pigeni kura -Balozi Tanzania
kufutiwa madeni:
Ushauri Nasaha
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Lishe
RIWAYA
|
|
|
|
|