NASAHA
Na. 045 Jumatano Aprili 26 - Mei 2, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
MPASHO NASAHA

KAMCHEZO  AU? 

Na Abu Halima Sa Changwa

WIKI iliyopita niliwaletea ushauri niliompa mjamaa mmoja anayetaka kugombea ubunge. Nilimwambia kuwa katika kugombea kwake na kuwa kwake mbunge, asichanganye dini na siasa, bali achanganye tu siasa na dini, ili asalimike.

Hivi karibuni kumekuwa na malumbano ya kisiasa kati ya wale wanaoruhusiwa kuchanganya na wanaokatazwa kuchanganya. Mashehe na maaskofu wamekuja juu kukishupalia chama tawala, na chama tawala kimeonyesha kwa njia moja au nyingine kutokuridhishwa na baadhi ya hawa wachanganyaji. 

Hapa panatia wasi wasi. Kwanza kabisa, pamoja na kwamba sina chama, paliponipagawisha ni ile response ya serikali kwa hawa wachanganyaji. Nakumbuka mashehe waliwahi kuchanganya. Wa kwanza ni Sheikh Ponda. (Sijui anaponda nini!). Huyu aliwaita waandishi wa habari, akawaeleza hisia zake kuhusu suala la malalamiko ya Waislamu na masuala mazima ya Mwembechai na madhila ambayo sheikh huyu aliona serikali ya CCM imewafanyia Waislamu. Sheikh Ponda ikabidi aingie mitini, maana alikuwa anatafutwa kama jambazi gani, sijui. Tukasikia mpaka Interpol ingetumika kumkamata. Haya! 

Wa pili ni Sheikh Mbukuzi (naye sijui anabukua nini!). Huyu naye aliongea na waandishi wa habari. Akachanganya. Kesho yake tukakuta magazeti yameandika; "Sheikh msema ovyo mbaroni", yaani Mbukuzi, kawa msema ovyo, kwa mujibu wa mapaparazi wetu. Haya! 

Kadinali Policarp Pengo (Sijui pengo la nini!) alisema hasa, na mapaparazi wakainyaka, kwamba CCM ni kichaka cha wahuni.Lakini bwana huyu ni "muadham", hadi marais hupiga magoti mbele yake, hakuulizwa chochote. Wakamataji watu waliinamisha tu vichwa chini, wakisema tu, makubwa haya! Haya! 

Juzi tu, Askofu Kakobe (sijui ni kadogo kiasi gani!) naye aliongea na waandishi wa habari, akapakaaaza. Akasema kabisa CCM haifaaaai. Lakini yeye hakuachwa tu kama Pengo. Lakini pia hakukurupushwa kama Ponda, wala hakuambiwa msema ovyo na kutiwa ndani kama Mbukuzi. Sana sana wakamataji baada ya kulalamika kidogo kuhusu kauli zake, wakaishia kusema: "Tumemsamehe, maana hajui alitendalo". Haya! 

Mara twasikia wakatoliki tena wametoa kitabu cha kupakaza. Mapaparazi wakatoa habari zake. Khe! Kadinali Pengo kawashupalia, eti wanataka kumgombanisha na serikali. 

Sasa mimi haya mambo yote yananipagawisha sana. Ila yote tisa, kumi najiuliza, hivi hii mipakazo ya "Chama kimeoza, viongozi wahuni, hao hawafai, blah blah blah" ni kweli au ni yale yaleee yaliyoanzwa na Hayati Nyerere? Tulishitukia tu akikishupalia chama; "eeh, wahuni, eeh hatima eeh hawatufai!" Na Kitabu akaandika. Uchaguzi ulipokaribia, yeye yeye tena akamuibua mtu chwaaa kutoka humo humo mlimojaa wahuni, akawaambia watu wasiogope wanaobebwa, akimaanisha bwana Mrema, na kwamba mtu kama anapenda kubebwabebwa kama maiti wamuache abebwe tu wote wakaangua vicheko Kwaaa kwa kwa kwaaaa! Mwishowe akasema: Chagueni huyu. 

Sasa nawauliza hawa watu, hivi mnavyochanganya, mko siriazi au mnatupagawisha tu? Kwa mashehe, uchaguzi uliopita kuna mashehe waliambiwa kuwa waligeuka wakawa madalali, ukali wao wote ukaisha, na watu wao wakabaki wamepagawa hawajui kwa kwenda. Leo mashehe hao wanashtukiwa na kufukuzwa kwa bakora kwenye mikutano ya hadhara. 

Wanaonipagawisha zaidi ni maaskofu. Do you really mean what you say, or you just say what you mean? Isijekuwa kamchezo ni kalekale ka kuwachanganya watu ili mpewe nafasi ya kuulizwa: Sasa tufanyeje? Ili mseme, Chagueni huyu. 

Inawezekana pia mnacheza kamchezo ka kuwachukua watu kisaikolojia. Mkishawachanganya wanawasikiliza sasa muwape solutions. Si ajabu baadaye karibu na uchaguzi tukasikia: "Amin, nawaambieni. Hata Kanisa lilikosea, lakini hatukulikimbia, kwa sababu Papa Yohane Paulo wa Pili aliliombea msamaha. Kwa hiyo nalisema CCM imekosea, nami naiombea radhi kama Papa alivyoliombea radhi Kanisa". Na watu wataitikia: "Aaaamen!" 

Kule kwingine nako twaweza kusikia: "Imeandikwa, msamehe akusamehae. Naliwakemea wakaudhika, lakini wakasema wamenisamehe. Nami leo nawasamehe. Nanyi wasameheni" Na wote wajibu: "Aaaamen!" 

Wasiwasi wa kamchezo haka unakuja tena pale ninapofikiria maaskofu wengine ngangali kama akina Mtikila wakinena tu wanakurupushwa kama akina Ponda, lakini wengine, aah, wanapeta tu. Sijui, lakini nina wasiwasi kwamba kuna kamchezo. Wacha tusubiri. Time will tell
 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Acheni  kuwacheza shere Waislamu, ondoeni udini

Serikali iache udini, kuwagawa wananchi - Sheikh  Mbukuzi

Wakati Kanisa Katoliki  likitoa miongozo ya kisiasa:
Sheikh mwingine ahojiwa Mwanza

Hakuna maendeleo bila Demokrasia -  Lipumba

MPASHO NASAHA
KAMCHEZO  AU?

HABARI
Sheikh Jongo asababisha mtafaruku mbele ya Al-Haji Mwinyi

‘Suala la kuirekebisha jamii lisiachwe mikononi mwa Serikali pekee’

Jiandikisheni na pigeni kura -Balozi

Tanzania kufutiwa madeni:
Wananchi hawatarajii nafuu yoyote

Ushauri Nasaha
Vyombo vya habari na vijana  - 2

MAKALA
Sababu ‘1000’ kwanini tunataka CCM ing’oke madarakani - 4

Kalamu ya Mwandishi
Muungano watimiza miaka 36 kwa migogoro

MAKALA
Chama cha Mapinduzi na sera za maendeleo (1)

Lishe
Jinsi ya kutunza virutubisho wakati wa maandalizi ya vyakula

Habari za Kimataifa

RIWAYA
Maisha mema ya akhera

MASHAIRI

MICHEZO

  • Raoul Shungu apigwa ‘Dafrao’ 
  • Yanga wamfurusha Waziri Mudhihir uwanjani
  • Simba wampongeza Msajili wa Vyama

  •  

     


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita