NASAHA
Na. 045 Jumatano Aprili 26 - Mei 2, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Habari za Kimataifa 
 
 

Russia yakiri kuuliwa kwa wanajeshi wake na Wachechen 

MOSCOW

RUSSIA imekiri kwamba wapiganaji wa Kiislamu wa Chechnya wamefanya shambulio kubwa katika vikosi vyake vya majeshi Jumapili, Aprili 23 mwaka huu. Hata hivyo, Russia imekanusha madai ya wapiganaji hao wa Kiislamu waliosema wamewaua wanajeshi 80 wa Russia, wakati ukweli wenyewe (kwa mujibu wa Russia) ni wanajeshi 15 tu waliouliwa.

Ikulu ya Russia imesema kati ya wapiganaji 50 mpaka 60 wakiongozwa na Ibn-Ul-Khattab waliwashambulia wanajeshi wa Russia karibu na kijiji cha Serzhen-Yurt, kusini mwa Jamhuri ya Kiislamu. 

Waziri wa Ulinzi wa Russia, Bw. Igor Sergeyev alisema, wanajeshi 15 wa Russia waliuliwa katika shambulio hilo. Kauli hiyo ya Bw. Igor inasahihisha kauli ya awali ya Russia iliyosema wanajeshi wake waliokufa ni 5 na 8 walijeruhiwa. 

Shambulio la Jumapili iliyopita la Wachechen dhidi ya Warusi ni la tano katika kipindi cha miezi 2 iliyopita. Wapiganaji wa Kiislamu wa Chechnya wakishirikiana na ndugu zao kutoka mataifa mbalimbali duniani, ni hodari kwa vita ya msituni. 

Vikosi hivyo vya Russia vilishambuliwa kwa kushitukizwa na wapiganaji wa Kiislamu, licha ya ulinzi mkali uliokuwepo wa Helkopta za Russia. 


Iran na Saudia kushirikiana

Jeddah, Saudi Arabia

MAWAZIRI wa Ulinzi wa nchi hizi mbili katika mazungumzo hapo juzi usiku wameazimia kukuza ushirikiano wa kijeshi katika nyanja ya usalama.

Waziri wa Ulinzi wa Iran, Bwana Ally Shamkhan yuko katika ziara ya nchi za Falme za Kiarabu na Saudi Arabia. 

Katika mazungumzo yao, wakuu hao wa Ulinzi wamesema kuwa, azma yao ni kuona kuwa mataifa haya yanaondoa mivutano na migogoro ya chini kwa chini. 

Wameongeza kuwa, mataifa yao yana sura ya Kiislamu hivyo wanadhima na wajibu mkubwa katika ulimwengu wa kuwa mfano bora katika kuutekeleza Uislamu. 

Pia wamekuwa kuwa pamoja na malengo yao ya kushirikiana kama dola kuu za Kiislamu na zenye ushawishi mkubwa katika mwenendo wa Kiislamu ulimwenguni watachukua hadhari dhidi ya kijicho cha adui yao aliye makini kukwaza mafanikio hayo. 

Saudi Arabia na Iran ni nchi zilizopo katika bara la Asia ambazo zinakadiriwa kuwa na Waislamu zaidi ya asilimia 98 kulinganisha na dini nyingine zilizopo huko. 

Iran ambayo hujulikana kama Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuanzia mnamo miaka ya sabini baada ya kuupindua utawala wa kifalme wa mfalme Shah. 

Saudi Arabia ambayo inatawaliwa Kifalme haijatangaza kama ni dola ya Kiislamu japokuwa yenyewe imekuwa ikidhania hivyo. 

Utawala wa Kiislamu ni ule ambao mkuu wake ana wadhifa wa "Khalifa" ambaye huingia madarakani kwa kupendekezwa na kuchaguliwa na wananchi. 

Kushirikiana kwa mataifa haya kutaondoa mikanganyiko miongoni mwa mataifa mengine ya Kiislamu ambayo yalikuwa yakikumbwa na misimamo tofauti pindi Saudia na Iran zinapotofautiana katika fatwa mbalimbali. 


Wapinzani wawili wauawa Zimbabwe 

HARARE

WANACHAMA wawili wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe wamedaiwa kuuawa huku wakulima wa Kizungu wakikutana kuombeleza kifo cha mwenzao aliyeuliwa na wafuasi wa serikali.

Chama cha upinzani nchini Zimbabwe, Movement For Democratic Change (MDC) kimesema kwamba, wafuasi wake wawili wameuliwa na wafuasi wa chama cha Rais Mugabe. 

Msemaji wa MDC, Bw. Nomore Sibanda amesema kuwa mtu mmoja alipigwa hadi kufa katika eneo la Shamva, kiasi cha kilometa 50 kaskazini-mashariki mwa Harare, Jumatatu na mwingine aliuliwa katika jiji hilo la Harare. 

Wiki iliyopita, mkulima wa Kizungu Bw. David Stevens aliteswa na hatimaye kupigwa risasi na mpiganiaji uhuru wa zamani. 

Kiongozi wa chama cha Movement For Democratic Change (MDC) Bw. Morgan Tsangirai amesema vurugu za kisiasa ndiyo gharama ya mabadiliko ya kimokrasia. 

"Vitisho vitaendelea. MDC inajua misukosuko itakayoipata haitaadhiri kampeni zetu. Mahali popote pale duniani, mtu akisimama dhidi ya dhulma, kitakachotokea ni fujo. Tutaendelea na mapambano", alisema kiongozi huyo wa MDC ambaye ni tishio kwa serikari ya Rais Mugabe. 


Museveni aondoa vikosi 

Kampala, UGANDA

SERIKALI ya Uganda imeondoa askari wake huko Jamhuri ya Congo Kinshasa.

Akitangaza uamuzi huo hapo jana, Waziri wa Ulinzi wa Uganda Bwana Steven Kavuma amesema kuwa, "tumeondoa vikosi vyetu huko kutokana na mafanikio tuliyopata dhidi ya wapinzani waserikali ya Uganda". 

Hata hivyo, Waziri huyo ameongeza kuwa, wataondoa vikosi viwili na baadhi ya askari wataendelea kubaki huko ili kuhakikisha usalama zaidi wa Uganda. 

Uganda ilipeleka vikosi vyake huko mashariki mwa Congo Kinshasa kwa kile ilichodai kuwa ni kuwasaka waasi wa Uganda waliokuwa wakiendesha mapigano kutokea upande huo. 


Nchi changa kulindwa 

Pretoria, AFRIKA KUSINI

RAIS Thabo Mbeki na Jiang Zemin wa China wametoa mwito wa kuzilinda nchi changa katika maendeleo dhidi ya ubeberu wenye sura ya kutandawaa (globalisation).

Rais wa China Bwana Zemin yuko katika ziara nchini Afrika ya Kusini. 

Katika mazungumzo yao yaliyochukua masaa mawili hapo jana walisema kuwa, japokuwa Uchina na Afrika Kusini ziko mbali kijiografia lakini kutokana na urafiki wao zimeungana zipo zikaribiana sana. 

Wakiyataja malengo ya nchi hizi mbili hapo siku za usoni ni kupigania maslahi ya nchi changa ili zitie mitaji yao katika nchi za viwanda. 

Wameeleza kuwa watapigania mfumo mpya wa uchumi kwa kuongoza nchi changa zisitawaliwe. 

Rais Zemin ni kiongozi wa kwanza wa China kuitembelea Afrikaya Kusini, alipowasili alikagua gwaride la heshima na kupigiwa mizinga 21. 

Nchi hizi zilirudisha uhusiano wa kibalozi mnamo mwaka 1998. 

Naye Mbeki amesema kuwa nchi yake inaunga mkono Uchina ipewe uanachama wa Shirika la Biashara ulimwenguni (WITO). 

Viongozi hao wamesisitiza mwito wao wa kuendeleza sera za uzinduzi kwa Afrika kwa kuhakikisha Afrika inaondokana na machafuko, umaskini na ukimwi. 

Hii leo, Rais wa China anatarajiwa kwenda mjini Cape Town ili kuona makumbusho ya Taifa. Moja ya makumbusho ambayo yalikuwa ni jela alimotumikia Bwana Nelson Mandela katika harakati za kuwatetea wazalendo wa Afrika ya Kusini. 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Acheni  kuwacheza shere Waislamu, ondoeni udini

Serikali iache udini, kuwagawa wananchi - Sheikh  Mbukuzi

Wakati Kanisa Katoliki  likitoa miongozo ya kisiasa:
Sheikh mwingine ahojiwa Mwanza

Hakuna maendeleo bila Demokrasia -  Lipumba

MPASHO NASAHA
KAMCHEZO  AU?

HABARI
Sheikh Jongo asababisha mtafaruku mbele ya Al-Haji Mwinyi

‘Suala la kuirekebisha jamii lisiachwe mikononi mwa Serikali pekee’

Jiandikisheni na pigeni kura -Balozi

Tanzania kufutiwa madeni:
Wananchi hawatarajii nafuu yoyote

Ushauri Nasaha
Vyombo vya habari na vijana  - 2

MAKALA
Sababu ‘1000’ kwanini tunataka CCM ing’oke madarakani - 4

Kalamu ya Mwandishi
Muungano watimiza miaka 36 kwa migogoro

MAKALA
Chama cha Mapinduzi na sera za maendeleo (1)

Lishe
Jinsi ya kutunza virutubisho wakati wa maandalizi ya vyakula

Habari za Kimataifa

RIWAYA
Maisha mema ya akhera

MASHAIRI

MICHEZO

  • Raoul Shungu apigwa ‘Dafrao’ 
  • Yanga wamfurusha Waziri Mudhihir uwanjani
  • Simba wampongeza Msajili wa Vyama

  •  

     


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita