|
Na. 045 Jumatano Aprili 26 - Mei 2, 2000 |
|
|
|
|
|
Sheikh mwingine ahojiwa Mwanza Na Mwandishi Wetu Mwanza POLISI mjini Mwanza ilimkamata na kumhoji kiongozi wa dini ya Kiislamu,Sheikh Adailla Abdulkadir kwa madai ya kuzungumzia siasa kwenye mihadhara ya dini. Sheikh huyo ambaye ni Imamu wa msikiti wa AL-Asays uliopo Makongoro mjini hapa, alikamatwa saa mbili ya usiku Ijumaa iliyopita akidaiwa kuruhusu kuandaliwa kwa kongamano ambalo lingezungumzia masuala ya "kuchanganya dini na siasa "kwenye msikiti wake. Imamu huyo alikamatwa na kuhojiwa katika kituo cha polisi cha Kati kwa masaa kadhaa. Akielezea juu ya kukamatwa kwake, Sheikh Abdulkadir alisema kuwa aliwaeleza Polisi kwamba yeye kama kiongozi wa msikiti ambayo ni nyumba ya Mwenyezi Mungu, asingeweza kuwazuia waumini wake waliomchagua kuitumia nyumba hiyo kuzungumza chochote kinachoruhusiwa na dini. Alisema kuwa siasa ni sehemu ya dini na haviwezikutenganishwa, kwani kuzungumzia siasa ni sawa na kuzungumzia dini. Imamu Abdurkadir aliachiwa bila masharti yoyote baada ya mahojiano. Wiki iliyopita polisi walimkamata mhadhiri maarufu mjini hapa ustaadh Ilunga Hassan Kapungu kwa madai hayo ya kuchanganya dini na siasa kwenye mihadhara ya waislamu. Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi wa mkoa kuzungumzia kadhia hiyo hazikufanikiwa. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Serikali iache udini, kuwagawa wananchi - Sheikh Mbukuzi Wakati
Kanisa Katoliki likitoa miongozo ya kisiasa:
Hakuna maendeleo bila Demokrasia - Lipumba MPASHO NASAHA
HABARI
‘Suala la kuirekebisha jamii lisiachwe mikononi mwa Serikali pekee’ Jiandikisheni na pigeni kura -Balozi Tanzania
kufutiwa madeni:
Ushauri Nasaha
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Lishe
RIWAYA
|
|
|
|
|