|
Na. 045 Jumatano Aprili 26 - Mei 2, 2000 |
|
|
|
|
|
Sheikh Jongo asababisha mtafaruku mbele ya Al-Haji Mwinyi Na Mwandishi Wetu SHEREHE za mwaka mpya wa kiislamu 1421 zilizofanyika Aprili 14 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja, zilitawaliwa na vurugu kutokana na Waislamu wachache waliohudhuria sherehe hiyo kutofurahishwa na kitendo cha waandalizi wa shughuli hiyo kumpa nafasi Imam wa Msikiti wa Manyema, Sheikh Hamid Jongo ya kusimama na kuzungumza na Waislamu. Sheikh Jongo amekuwa akituhumiwa na Waislam kuwa ni mtu anayetumika dhidi yao na watu wasiowatakia mema Waislamu. Miongoni mwa lawama hizo ni kitendo cha viongozi wa msikiti wa Manyema kuwaita Polisi kuwakamata Waislamu waliongia katika msikiti huo baada ya kufanya maandamano ya kulaani kauli za Wabunge za kupinga Hijab mashuleni. Na katika tukio la Mwembechai Sheikh Jongo alitoa hotuba za kushutumu Waislamu waliokuwa mstari wa mbele kutetea na kulaani mauaji yaliyofanywa na polisi.Kutokana na taswira hizo Jongo alipoanza kuzungumza wengine walianza kuzomea, wengine kulalamika na baadhi yao kuondoka. Shutuma hizo za waislamu zimeelekezwa kwa masheikh wengine wa Bakwata kuwa wamekuwa wakiwatumikia viongozi wa serikali katika masuala yasiyopendeza kwa waislamu.Miongoni mwao ni Sheikh Suleiman Kilemile ambaye alisikika katika semina moja akiwalaumu waislamu kuwa ni watu wa jazba na wenye chuki dhidi ya wakristo. Waislamu wamelaumu kauli hizo na kusema kuwa suala ni serikali kuwadhulumu waislamu na sio chuki kati ya waislamu na wakristo. Awali akitoa nasaha zake Al-haj Alli Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo aliwataka waislamu watumie kalenda za kiislamu katika mawasiliano yao yote na kuwaasa waepukane na tabia za kufuata tamaduni za kigeni katika shughuli zao mbalimbali. Alitoa mfano kwa kusema kuwa wakristo hufanya 'send-off' kuwaaga maharusi na kuwa Waislamu nao wameiga jambo hilo,kitu ambacho ni kinyume na mafundisho ya kiislamu. Katika sherehe hizo Sheikh Suleiman Kilemele alitoa mada inayohusu Hijra. Na Imam wa Msikiti wa Kitumbini Sheikh Juneid alisoma dua ya kufunga sherehe hizo.
Na Kenneth Simboya -Iringa TAASISI ya kidini ijulianayo kama Dhinureyn Islamic Foundation yenye makao yake makuu mkoani Iringa imesisitza azma yake ya kuijenga jamii ya Watanzania kiroho na Kimwili. Akiongea na Mwandishi wa habari hizi jana Ofisini kwake Wilolesi Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sheikh Said Abri alisema kwamba Taasisi hiyo inasikitishwa sana na jinsi maadili katika jamii ya Watanzania yanavyozidi kumomonyoka na hivyo kuzidisha vitendo viovu katika jamii. Sheikh Said alisema kwamba suala la kuirekebisha jamii ya Watanzania haliwezi kuachwa mikononi mwa Serikali peke yake, ni swala ambalo madhehebu ya dini yanatakiwa kulishughulikia ipasavyo. "Kazi ya dini yoyote ile ni kuwajenga waumini wake kiroho na kimwili ili wakubalike hapa duniani na peponi", alisema Sheikh Said. Kwa mujibu wa Sheikh Said ili kuijenga jamii kiroho, Dhinureyn Islamic Foundation inajenga Misikiti kwa ajili ya watu kupata mahali pa kumwabudi Mungu. "Lakini pia katika karne hii ya sayansi na teknolojia suala la elimu kwa waumini lazima lipewe kipaumbele", alisema Sheikh Said na kuongeza kuwa ndio maana Dhinureyn wamejenga chuo hapa mjini Iringa kijulikanacho kama Dar-Al-Ulium (Nyumba ya elimu) pia wanatarajia kujenga sekondari na chuo kikuu hapa Iringa. Pamoja na shughuli za nyingine Dhinureyn mkoani Iringa wanatoa huduma za kiafya, ushauri katika maswala ya kilimo, kutoa misaada wakati wa maafa na kusomesha watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia karo bila kujali dini.
Na Y. Kijukuu VIJANA nchini wenye umri wa miaka 18 au zaidi wametakiwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais, utakaofanyika mwezi Oktoba, mwaka huu. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa 'Islamic Club', Balozi Abbas Sykes, Aprili 23, mwaka huu katika mahafali ya kuwaaga kidato cha sita yaliyofanyika katika sekondari ya Tambaza, jijini. "Uchaguzi ni haki yenu ya kikatiba, kwa hiyo lazima vijana mjiandikishe na wakati ukifika mjitokeza kupiga kura ili muwachague viongozi waadhirifu, ambao wataweza kuondoa kero mbali mbali zinazowakabili", alisema Balozi Sykes. Mwenyekiti huyo wa Islamic Club alisema, vijana wa Sekondari wamepata elimu ikiwemo inayohusu mambo ya siasa, kwa hiyo lazima waitumie elimu hiyo kuwaelimisha wazazi wao na wananchi wengine kwa ujumla umuhimu wa kupiga kura, ili wajiandikishe na hatimaye kupiga kura wakati utakapofika. Awali katika hafla hiyo wanafunzi wa Kiislamu katika risala yao walieleza matatizo mbalimbali yanayowakabili, zikiwemo nafasi za masomo ya elimu ya juu, kuzuiwa kuvaa hijab katika shule za sekondari zinazomilikiwa na jeshi Dar es Salaam na ukosefu wa ajira. Akijibu risala hiyo, Balozi Sykes alisema taasisi
yake ina mipango kamambe ya kuwashirikisha Waislamu ili wajiletee maendeleo
yao wenyewe badala ya kutegemea misaada. Mipango hiyo ni pamoja na kutoa
elimu ya ufundi kwa vijana wanaomaliza elimu ya msingi na ile ya sekondari.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Serikali iache udini, kuwagawa wananchi - Sheikh Mbukuzi Wakati
Kanisa Katoliki likitoa miongozo ya kisiasa:
Hakuna maendeleo bila Demokrasia - Lipumba MPASHO NASAHA
HABARI
‘Suala la kuirekebisha jamii lisiachwe mikononi mwa Serikali pekee’ Jiandikisheni na pigeni kura -Balozi Tanzania
kufutiwa madeni:
Ushauri Nasaha
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Lishe
RIWAYA
|
|
|
|
|