|
Na. 045 Jumatano Aprili 26 - Mei 2, 2000 |
|
|
|
|
|
Vyombo vya habari na vijana - 2 NA KHADIJA IDD KATIKA wiki iliyopita, tuliangalia jinsi vyombo
vya habari vinavyowaathiri vijana hususan kupitia kwa watu au waigizaji
waliomo katika vyombo hivyo. Tuliona jinsi vijana wanavyojibadilisha na
kujirekebisha kwa kumuuangalia muigizaji fulani wa mchezo wa Televisheni
au tangazo la biashara. Leo basi tuangalie wazazi au walezi wana mchango
gani katika kuwasaidia vijana katika kipindi hiki chenye mtirivyogo wa
mambo.
KABLA ya kuwaruhusu au kuwakataza vijana kutumia chombo fulani cha habari, ni vizuri na muhimu kuwasaidia vijana hao waeleweshwe maadilli ya jamii yao vyema, waelewe kwa mapana yapi yanaruhusiwa na yapi yapi hayaruhusiwi. Katika kufanya hivi, inabidi tuchukue tahadhari ili tupunguze au kuondoa kabisa matumizi ya ukali usio wa lazima, kwani vijana katika kipindi walichonacho cha makuzi hujiona ni wakubwa na wanajua kila kitu. Matumizi ya ukali yataondoa maelewano na masikilizano baina yako na kijana. Badala yake basi, mzazi atumie upole, aheshimu na kujali hisia za kijana na pia ampe heshima inayostahili, katika kumuelimisha kwa nini anakatazwa au kuzuiliwa kufanya kitu fulani. Katika kutumia vyombo vya habari, vijana hukumbana taarifa za aina mbalimbali, zinazowafaa na zisizowafaa. Ni sisi wazazi na walezi wenye jukumu la kuwasaidia kuchambua zinazowafaa. Katika magazeti kwa mfano, vijana hupata taarifa aina mbalimbali na mengine yakiambatanishwa na picha au katuni za 'ajabu.' Kuwakataza vijana kwa kutumia 'marufuku' peke yake na hakutoshi na wala hakusaidii iwapo 'marufuku' hiyo haiambatani na ushauri na maelekezo yaliyotolewa kwa njia nzuri. Sababu za hali hii ziko nyingi, vijana huenda shule, kutembelea jirani, ndugu na marafiki, nao hutembelewa, huenda maeneo mbalimbali. Huko wapitako hawana "marufuku" inayowazuia kufanya watakalo au kusoma watakacho. Ni jambo muhimu sana kwa vijana hawa kuelimishwa ipasavyo juu ya habari wazipatazo ili waweze kutofautisha za kujenga na za kubomoa. Habari za fumanizi, mapenzi na mauaji yaliyojazwa 'kasheshe' kwa hakika yana uongo mwingi kuliko ukweli, na yanaharibu vijana na kuwafanya waisifikirie juu ya hali zao bali wapasue mbavu, kucheka na kuduwaa. Kwa upande wa Televisheni, hali kadhalika tunaona yanayoonyeshwa, kwa hali yake haina tofauti sana. Michezo inayoonyesha (na ndiyo inayobeba sehemu kubwa ya muda) hulenga kuelimisha juu ya jambo fulani. Lakini maadili ya michezo mingine ni kinyume na yale ya jamii yetu. Njia za 'kuelimisha' katika michezo mingi haziendani na njia zetu. Vijana wanapaswa kujua hili na kuweza kutofautisha. Hata hivyo hali inakuwa ngumu kidogo kwani katika TV watu wanaonekana wakitenda na hamna wanavyotenda, tunawasikia wasemapo na tunaona namna wasemavyo hayo yote hutoa taarifa nyingi sana, zilizokusudiwa na zile zisizokusudiwa. Kutokana na hatua yao ya makuzi vijana huanza kuiga na kujipima kwa kumuangalia mtu fulani katika mchezo fulani. Wazazi au walezi wanawajibu wa kujua vijana wao wanaangalia nini na kuwashauri mara tu baada ya kumaliza wanachoangalia. Hata hivyo, iwapo kinachoangaliwa ni kinyume na maadili ni bora kuindolewe kabisa, na badala yake wazazi wawashauri kuangalia picha/michezo mingine inaofaa. Kwa ujumla waelimishwe matumizi mazuri ya video na televisheni. Kuwakataza au kuwaruhusu vyote vinafaida na hasara
zake. Ukiwaruhusu wataangalia vyote na kuiga vyote, ukiwakataza pia watachunguza
unaweka wapi funguo na wataiba, au watakwenda kuangalia kwa jirani au rafiki
zao na huko watapata 'mwalimu bora' wa kuwaelekeza. Haya yote yafanyike
pamoja, wakatazwe kuangalia yaliyo kinyume na maadili na waruhusiwe kuangalia
yanayafaa na wakati huo huo wakipata kushauri na mawaidha kutoka kwa wazazi
na walezi. Ila tukumbuke tu kuwa hawa ni watoto wetu lakini ni 'watu wazima'
pia hivyo tuwaheshimu katika kufanya hivyo.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Serikali iache udini, kuwagawa wananchi - Sheikh Mbukuzi Wakati
Kanisa Katoliki likitoa miongozo ya kisiasa:
Hakuna maendeleo bila Demokrasia - Lipumba MPASHO NASAHA
HABARI
‘Suala la kuirekebisha jamii lisiachwe mikononi mwa Serikali pekee’ Jiandikisheni na pigeni kura -Balozi Tanzania
kufutiwa madeni:
Ushauri Nasaha
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Lishe
RIWAYA
|
|
|
|
|