NASAHA
Na. 045 Jumatano Aprili 26 - Mei 2, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Hakuna maendeleo bila Demokrasia - Lipumba

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi [CUF] Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa maendeleo duni katika nchi za ulimwengu wa tatu yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa demokrasia.

Aliyasema hayo kwenye kipindi cha 'Maoni yetu' kilichotangazwa na sauti ya Ujerumani Jumapili wiki hii. "Demokrasia na maendeleo huenda pamoja", alisema Profesa huyo wa uchumi. 

Katika mjadala huo ambao ulikuwa juu ya kuhusika kwa mfuko wa fedha wa Kimatifa IMF na Benki ya Dunia(WB) na kuanguka kwa uchumi wa nchi za ulimengu wa tatu, Profesa Lipumba alisema kuwa 'lazima tuelekeze lawama zetu kwa viongozi wetu wenyewe na si vinginevyo. Akifafanua alisema kuwa ufujaji wa fedha za umma unaofanywa na viongozi wa nchi za dunia ya tatu ndiyo tatizo kubwa zaidi. 

Alikubali kuwa IMF na Benki ya Dunia wana matatizo lakini lazima tutatue matatizo ya ndani kwanza kabla ya kuyarukia mashirika hayo. 

Kuhusu utawala bora Profesa Lipumba alisema kuwa viongozi wengi wa nchi zinazoendelea hawako makini katika suala la kuandaa mazingira yanayoruhusu kukua kwa uchumi na badala yake hutumia muda mwingi kujiimarisha kisiasa wao binafsi. Amedai kuwa hali hii inasababishwa na ukiritimba wa kisiasa, ambapo vyama vingi vimeng'ang'ania madaraka kwa zaidi ya miaka 50. 

"Vyama vilivyotawala muda mrefu hupoteza uwezo wa kutambua na kutetea matatizo ya watu. Viongozi wake hujipa uhalali wa kutawala na kuwaona wananchi kuwa ni watu wa kutawaliwa tu", alisema Prof. Lipumba. 

Kwa upande wa demokrasia Mwenyekiti huyo wa CUF alidai kuwa nchi nyingi zinazoendelea zinakabiliwa na ukosefu wa demokrasia ya kweli. Hakuna uhuru wa kisiasa, watu hulazimishwa kujiunga na vyama vya siasa kabla ya kuruhusiwa kugombea vyeo vya kisiasa. 

Wakati huo huo, Mwenyekiti huyo wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), amesema kuwa wananchi katika mikoa na wilaya mbalimbali hapa nchini, wamedhamiria kwa dhati kabisa kuleta mabadiliko ya kisiasa kwa kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Urais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. 

Akizungumza na NASAHA mwishoni mwa wiki, akitokea mikoa ya Tabora na Shinyanga, Profesa Lipumba amesema kuwa hali ngumu ya maisha, kukithiri maradhi sambamba na umasikini, kukosekana kwa ajira na kukosekana kwa mawasiliano ya kuaminika, hasa kwa mikoa ya kati na kusini imekuwa ni kichocheo tosha kwa wananchi hao kuona haja ya kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini.

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Acheni  kuwacheza shere Waislamu, ondoeni udini

Serikali iache udini, kuwagawa wananchi - Sheikh  Mbukuzi

Wakati Kanisa Katoliki  likitoa miongozo ya kisiasa:
Sheikh mwingine ahojiwa Mwanza

Hakuna maendeleo bila Demokrasia -  Lipumba

MPASHO NASAHA
KAMCHEZO  AU?

HABARI
Sheikh Jongo asababisha mtafaruku mbele ya Al-Haji Mwinyi

‘Suala la kuirekebisha jamii lisiachwe mikononi mwa Serikali pekee’

Jiandikisheni na pigeni kura -Balozi

Tanzania kufutiwa madeni:
Wananchi hawatarajii nafuu yoyote

Ushauri Nasaha
Vyombo vya habari na vijana  - 2

MAKALA
Sababu ‘1000’ kwanini tunataka CCM ing’oke madarakani - 4

Kalamu ya Mwandishi
Muungano watimiza miaka 36 kwa migogoro

MAKALA
Chama cha Mapinduzi na sera za maendeleo (1)

Lishe
Jinsi ya kutunza virutubisho wakati wa maandalizi ya vyakula

Habari za Kimataifa

RIWAYA
Maisha mema ya akhera

MASHAIRI

MICHEZO

  • Raoul Shungu apigwa ‘Dafrao’ 
  • Yanga wamfurusha Waziri Mudhihir uwanjani
  • Simba wampongeza Msajili wa Vyama

  •  

     


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita