NASAHA
Na. 054 Jumatano Juni 28 - Julai 4, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
HABARI ZA KIMATAIFA 

Polisi jela kwa mauaji ya Waislamu 

Calcuta, India

MAAFISA watano wa polisi nchini India hivi karibuni wamehukumiwa kifungo cha maisha na faini kwa kumuua Muislamu mwanaume na mkewe huko Calcuta kwa kile kilichodaiwa kuingia katika Uislamu.

Hakimu wa awamu nyingine wa Calcuta, Bwana Sukumar Chakraborty aliwahukumu maofsa hao baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya siri na uvurugaji wa ushahidi. 

Chimbuko la tuhuma limetokana na uchunguzi ulioongozwa na idara kuu ya uchunguzi ambao umewezesha mamlaka ya mahakama kutoa uamuzi wa kuwa, maofisa hao walimuua Lachimi Singh na mkewe Penuka kwa sababu ya kurejea katika dini ya Kiislamu. 

Lachimi alikuwa ofisa wa polisi huko Punjab na alibadilisha jina na kuitwa Bashir Ahmed. Penuka alibadili jina na kuitwa Sakina. Wote walipigwa risasi jioni ya mwezi Mei 17, 1993 katika eneo la mafunzo ya kulenga shabaha. 

Jopo la majaji liliamini kuwa maofisa waliitupa miili hiyo na kujitahidi kuficha makosa. Hadi sasa haijapatikana hata mwili mmoja . 

Mateso kwa wanaoacha dini nyingine na kurejea katika Uislamu nchini India ni suala la kawaida, nchi inayodai kuwa haina dini na ina demokrasia. 

Katika matukio mengi Waislamu hao hulazimika kuhamia miji mingine kwa ajili ya uhuru na usalama wao. 

Miaka michache iliyopita, Mhindi mmoja tajiri na maarufu alirejea katika dini yake ya asili (Uislamu) huko Ghaziabad Uttarparadesh. Wahindu wakamzulia na kumfungulia mashtaka ya uongo ya mauaji. Aliwekwa mahabusu na mwishowe alifutiwa kesi baada ya kusikilizwa. 

Ukweli kuwa haki iliyotolewa kwa matukio yote mawili, India inahtiaji kusonga mbele kwa maili kadhaa. 

Serikali imeshindwa kutoa haki sawa miongoni mwa wananchi. Matarajio ya sasa ni kufanya jitihada ili kuanzisha demokrasia kwa wote. Hii itafanya wananchi wa India wote waweze kujihisi kushiriki katika muundo wa dola nchini. 


Rais wa Kazakhstan kutawala maisha

Astome, Kazakhstan

BUNGE la Kazakhstan lilipitisha uamuzi wa kura nyingi jana wa kumpa Rais Nursultan Nazarbayev mamlaka ya uwezo wa kuwa na nguvu za kisiasa katika uhai wake wote.

Sheria hiyo inampa Nazarbayev uwezo wa kuwa na uwezo wa kuwashauri Marais wote watakaokuja, kuwa na sauti serikalini, katika Bunge na hata kwa wananchi wa Khazakhstan hata baada ya kustaafu, inamruhusu kutoa ushauri katika masuala nyeti yanayohusu mambo ya ndani na nje ya nchi. 

Kwa wapinzani wake, nguvu mpya aliyopewa inathibitisha tuhuma kwamba Nazarbayev, ambaye anaongoza nchi hiyo tajiri kwa mafuta tangu ilipopata uhuru wake toka Moscow mwaka 1991 ana nia ya kuiongoza Kazakhastan kwa maisha yake yote. 

"Muacheni Nazarbayev awe Rais wa maisha", alisema Serikbolsyn ambaye ni mpinzani mkubwa wa utawala na pia kiongozi wa chama cha kikomunisti cha KCP kuliambia bunge. 

Sheria mpya inamhakikishia nafasi ya kudumu katika Baraza la Ulinzi na pia uongozi wa Bunge. Ana uwezo wa kujiunga na Baraza la Katiba akitaka, ingawa wasaidizi wake waliweza kumfanya kuwa mjumbe wa maisha wa Seneti. 

Nazarbayev amechagua kujiweka mbali na sheria hiyo iliyopitishwa, na kusema kwamba alisoma kwa mara ya kwanza katika gazeti la Urusi alipotembelea Moscow. 

Lakini wengi wanasema kwamba sheria hiyo ya bunge inayo baraka na uthibitisho wa kiongozi huyo wa zamani wa kikomunisti na rekodi yake ya kufanya makubaliano na wabunge kwa ahadi ya upendeleo fulani. 

Bunge dogo lijulikanalo kama Nazhilis (Majlis) na Bunge kuu la Seneti yalikutana kwa masaa mawili na kuingiza mabadiliko 87 katika muswada uliokuwepo tangu mwisho wa wiki jana, ingawa majadiliano yalikuwa makali na matokeo yake kutokuwa na shaka yoyote. 

Katika wajumbe 77 wa Mazhilis, 59 walipopiga kura kuunga mkono marekebisho, matano walipinga na watatu hawakupiga kura. Katika viti 37 vya Seneti, 36 waliunga mkono na mmoja ikaharibika. 

"Muswada huu siyo sheria, lakini itakuwa hivyo ikisainiwa na Rais", alisema Askhat Daulbayev, Mwenyekiti wa kamati iliyochaguliwa kuandaa muswada huo. 

"Hakuna jambo lolote maana linaloweza kutokea bila kuidhinishwa na Rais", Pyort Svvik, kiongozi wa chama cha Azamat alisema. 

Wakati huo huo, Saparmurat Niyazov, Rais wa nchi jirani ya Tunemenistan, tayari ameshatajwa kuwa Rais wa maisha wa nchi hiyo tajiri wa gesi. 

Nchi za magharibi zinayatazama maendeleo haya kama hatua ya makusudi ya kujenga udikteta wa viongozi wa Asia ya kati, eneo muhimu linalounganisha Russia, China, Iran na Afghanistan na wakati huo huo ikitamba kuwa na rasilimali nyingi. 

Sheria hii kwa upande wa Kazakhstan ilipendekezwa na chama kiitwacho Civilian Party ambacho viongozi wake ni wamiliki wa viwanda na kikasisitiza kuungwa kwake mkono na wajumbe wa Bunge. 

Wapinzani wanasema sheria hii ilichochewa na ukweli kwamba Nazarbayev alitarajiwa kufikisha miaka 60, tarehe 6 mwezi ujao. 

Nazarbayev mwenyewe alisema wiki iliyopita kwamba hakutaka kupewa zawadi wala pongezi na maofisa wa serikali, lakini amri hii huenda ikapuuziwa katika nchi kama hii ambapo nafasi ya kumuona Rais na wasaidizi wake huonekana kama ufunguo wa mafanikio. 


Mkutano wa OIC wafunguliwa 

Kuala Lumpar, Malaysia

WAZIRI Mkuu wa Malaysia Bwana Mahathir Mohamed amefungua mkutano wa Mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya nchi za Kiislamu (OIC).

Mkutano huo wa siku nne ulifunguliwa jana na Waziri Mkuu huyo kwa kutoa tahadhari ya kujilinda dhidi ya mataifa ya kibeberu. 

Amewataka Waislamu kukumbatia elimu ya sayansi ya kileo, hususan katika enzi hii ya habari. 

Ametahadharisha kuwa mataifa ya magharibi yana lengo la kuongoza na kutawala shughuli zote za mabenki na viwanda hatimaye kurudisha ukoloni. 

"Uporaji wa magharibi una lengo la kutufikisha tuwe hatuna usemi na dhaifu", alisema. 

Aliongeza kuwa, "Uislamu umetoa maagizo ya kutafuta elimu, kwani ndiyo mhimili wa kutotawaliwa". 

Naye Mwenyekiti wa OIC kuhusu suala la amani mashariki ya kati alisema kuwa Israel inadhalilisha watu na mwenendo mzima wa amani eneo hilo. 

Na alitoa mwito wa kuendeleza mapambano dhidi ya Israel hadi iachie ardhi inazozikalia kwa mabavu. 

Akigusia suala la Russia kuivamia Chechnya alieleza kuwa huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu unaotakiwa kukomeshwa mara moja. 

Katibu Mkuu wa umoja huo amezitaka Iraq na Kuwait kumaliza chuki ya chini chini baina yao kwa kurudishiana mateka wa kivita, iliyotokea mwanzoni mwa miaka ya tisini. 

Pia ameitaka India kumaliza mgogoro kati yake na jimbo la Kashmir kwa kuruhusu kura ya maoni ifanyike ili wananchi wa Kashmir watoe maoni yao hatimaye kujitawala. 

India imekuwa ikiikalia kwa mabavu Kashmir huku ikidai kuwa yenyewe ni nchi ya demokrasia. 

Huku akionesha kukerwa na vikwazo dhidi ya Iraq, alieleza kuwa vitendo inavyofanyiwa Iraq havihalaliki na mbaya zaidi ni uvamizi wa mara kwa mara wa madege ya Marekani kwa kisingizio cha kulinda maeneo ya usalama. 

Katika moja ya vikwazo ilivyowekewa Iraq ni kutorusha ndege zake katika ardhi yake ambayo imetengwa kuwa ukanda wa amani. 

Vikwazo hivyo hadi hivi sasa vimegharimu maisha ya Wairaq mamilioni wamefariki. 

Na alilaani kitendo cha Israel kuhujumu makazi ya Palestina na ardhi ya Lebanon na Syria na kutoa mwito wa kuongeza nguvu hadi ushindi dhidi ya Israel kama ambavyo hivi karibuni Hizbullah walivyowasambaratisha katika ardhi waliyoikalia zaidi ya miaka ishirini. 

Umoja huo wenye wanachama 56, ikiwa ni mchanganyiko wa nchi zenye serikali ya Kiislamu na zisizo na serikali ya Kiislamu. 

Nchi ambazo hujiunga na umoja huo hunufaika na miradi ya kiuchumi isiyo na riba au mlengo wa kuzitawala nchi maskini. 

Mkutano huo wa Mawaziri utapitia maazimio matatu juu ya utekelezaji wake. 

Maazimio hayo ni suala la Israel kutibua amani na usalama eneo la Mashariki ya kati, uvamizi wa Russia huko Chechnya na Kashmir kukaliwa kimabavu na India. 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Serikali isikilize kilio cha wapinzani na Waislamu

Kishindo cha CUF chaitikisa Dar

Mamia  warudisha kadi za CCM Kilwa

Chama cha Mugabe chupuchupu Zimbabwe

Wasikilizeni wananchi wasemavyo toka kwenye meli mbovu mkabala na Posta ya zamani

CCM yakasirishwa kwa kuswaliwa Mtume (S.A.W.)

Wanaomzomea Bilal waambiwa Oktoba watakula jeuri yao

CCM wapoteza viti 18196; CUF yaongoza kuvinyakua

Tambwe huyoo anakuja!

Ushauri Nasaha
Unapomdharau mama yako mbele ya rafiki yako...

MAKALA
Uchaguzi wa Zimbabwe: Vita kati ya mabeberu na wapinga Ukoloni mamboleo

MIPASHO NASAHA
Matonya wahi, pesa zinatoka sasa!

MAKALA
Vijembe kwa viongozi wa vyama vya upinzani, huduma kwa wananchi ziro

KALAMU YA MUANDISHI
Ukongwe hausaidii kubaki madarakani

MAKALA
Kuchanganya siasa na ushirikina

Habari za Kimataifa

Lishe
Faida za vyakula vya nyuzi nyuzi

RIWAYA
Dunia ndivyo ilivyo - 4

Barua

MASHAIRI

TANGAZO

MICHEZO

  • Mpambano wa watani wa jadi: U-CCM umeiponza Yanga wasema Simba
  • Wanamichezo wamshtukia Mkapa
  • Mabosi DRFA kujulikana leo

  • Pupe, Mziray wamlia ‘dip’ Shungu
    -



     
     

       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com


    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita