|
Na. 054 Jumatano Juni 28 - Julai 4, 2000 |
|
|
|
|
|
Faida za vyakula vya nyuzi nyuzi CHAMOS, H.J KULA vyakula mchanganyiko ni moja kati ya kanuni muhimu za lishe bora. Vyakula vya nyuzinyuzi ni mchanganyiko wa vyakula mbalimbali vya wanga ambavyo haviyeyushi kama vyakula vingine. Nyuzinyuzi hizi huwepo kwenye gamba la nje la seli. (cell walls). Nyuzinyuzi hizi hupatikana katika vyakula ambavyo havijapitia kiwandani au utayarishaji kama kukoboa, kusaga (n.k.) ambavyo ni nafaka , mizizi, kundekunde, matunda, mbegu za mafuta na mboga za majani. Kuna aina mbalimbali za nyuzinyuzi ambazo zimegawanyika katika makundi mawili. Zinazoyeyuka na zisizoyeyuka. Vyakaula vya mimea vinaweza kuwa na aina zote mbili au mojawapo. Kwa mfano kundekunde na matunda zina nyuzinyuzi zinazoyeyuka. Nafaka zingine huwa na nyuzinyuzi zisizoyeyuka. Pia kuna wanga ambao hauyeyushwi unapofika kwenye utumbo mpana. Hii huwa inaifanya kazi kama za nyuzinyuzi. Mwili hauwezi kuyeyesha nyuzinyuzi au kufyonza kama ambavyo hufanya kwa vyakula vingine. Nyuzinyuzi hubakia katika utumbo na hata baadaye hata kama makapi. Zile zinazoyeyuka hufyonzwa na mwili . Nyuzinyuzi ni irutubisho muhimu kwa sababu zifuatazo: Nyuzinyuzi hupunguza kasi ya uyeyushaji wa chakula kuanzia mdomoni hadi tumboni. Vyakula ambavyo vihavijakobolewa au kupitia viwandani huwa hizi nyuzinyuzi ambazo hubakia mdomoni au tumboni kwa muda mrefu. Hivyo humfanya mtu asisikienjaa haraka. Hii husababishwa na ugumu wa kuzitafuna na kuzisagasaga nozi za vya vyakula hivi (cell walls) tofauti na vyakula vilivyokobolewa na kupitia viwandani huwa rahisi kutafunwa kusagwa na hata kuyeyushwa. Nyuzinyuzi husaidia chakula kufyonzwa taratibu. Nyuzinyuzi zikiloana hubeba maji na kusababisha chakula kuwa kizito tumboni. Hii husababisha ufyonzwaji wa virutubisho kuwa wataratibu. Ni vizuri kwa mwili kufyonza virutubisho pole pole na kwa ufanisi kuliko haraka haraka kama chakula kinavyokuja. Nyuzinyuzi husaidia chakula kuwa kingi. Hii huwasaidia sana watu wanene na wenye uzito mkubwa kupunguza kula.Kwani huon achakula kingi hali ni nyuzinyuzitu. Lakini hii ni hasara kwa watoto wadogo kwani watakula chakula kingi cha kuongeza nguvu tu badala ya kula vyakula mchanganyiko. Kwani hushiba haraka. Nyuzinyuzi husaidia kinyesi kuwa laini na kingi. Hii ni faida kuu mojawapo ya nyuzinyuzi. Kutokana na tabia ya nyuzinyuzi kufyonza maji, hutoka na kinyesi kupitia utumbo mpana. Kinyesi kikiwa laini na kingi hutoka kwa wepesi na kuzuia "constipation" matatizo ya kupata choo. Hii pia husaidia utumbo kubaki na afya wakati wote na hata kuzuia magonjwa mbalimbali ya utumbo kama sarakani, vidonda n.k. Nyuzinyuzi husaidia hulowesha wadudu wowote wanaolowana na kuwatoa nje na kinyesi, hii huzidi kuuacha utumbo msafi na kuukinga na magonjwa. Vile vile nyuzi nyuzi husaidia kupunguza kiasi kolesteroni katika damu ambayo husababisha magonjwa ya moyo. Kwa upande mwingine, nyuzinyuzi huzuia ufyonzwaji wa madini ya chuma na mengineyo. Kwa hivyo tunashauri wajawazito na watoto wadogo ambao wanaweza wakapata "anemia" upungufu wa damu wanashauriwa wasile sana. Na kwa vyakula vya watoto, nyuzinyuzi zipunguzwe, kwani watashiba haraka na kuelekea wasile vyakula vingine vyenye virutubisho mbalimbali. Vyanzo muhimu vya nyuzinyuzi ni kama karoti, matunda aina zote, nkabeji, mboga za majani maharage na jamii yake, mahindi mabichi, unga wa mahindi usiokobolewa sana, viazi n.k. Hasa hasa utapata 'fibre" kwenye vyakula asilia. |
YALIYOMO
Tahariri
Kishindo cha CUF chaitikisa Dar Mamia warudisha kadi za CCM Kilwa Chama cha Mugabe chupuchupu Zimbabwe Wasikilizeni wananchi wasemavyo toka kwenye meli mbovu mkabala na Posta ya zamani CCM yakasirishwa kwa kuswaliwa Mtume (S.A.W.) Wanaomzomea Bilal waambiwa Oktoba watakula jeuri yao CCM wapoteza viti 18196; CUF yaongoza kuvinyakua Ushauri Nasaha
MAKALA
MIPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MUANDISHI
MAKALA
Lishe
RIWAYA
Pupe, Mziray wamlia ‘dip’ Shungu - |
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza
hapa
Au
Andika barua kwa: nasaha1420@yahoo.com
|
|
|
|