|
Na. 054 Jumatano Juni 28 - Julai 4, 2000 |
|
|
|
|
|
Matonya wahi, pesa zinatoka sasa! Na Abu Halima Sa Changwa. WASOMAJI wangu wengi walianza kunilaumu nikikutana nao mitaani, kwamba nimeingia mitini, na wengine walitaka kujua kama nimeishiwa na mipasho au ndo nimeshanunuliwa. Sijaingia mitini, sijanunuliwa, bali nilikuwa katika harakati za kutafuta vya kupasha. Ni kwamba sijaandika katika wiki mbili zilizopita. Wiki ya kwanza nilikwenda kumpokea Amani Karume na kufuatilia mambo yalivyokwenda baada ya hapo. Mapokezi yake yalikuwa ni makubwa mno Dar es Salaam na Zanzibar, ingawaje kwa upande wa Pemba hakukuwa na ule mfumuko wa watu kama ilivyokuwa sehemu nyingine. Wiki iliyofuata nikawa tena kwenye heka heka za kumpokea Ngangari, ilimradi nijaribu tu kulinganisha na yale mapokezi ya Amani Karume. Mapokezi yake naye yalikuwa ni makubwa mno, Dar es Salaam, Unguja na hata kule Pemba. Nadhani mapokezi haya ndiyo yaliyompa Maalim Seif ile nguvu ya kusema kwamba Yeye ni Tyson na Karume ni Matumla. Nilikusanya mengi katika mapokezi yote mawili, ila ya muhimu zaidi ni maelezo ya mazungumzo kati ya ndugu wawili niliowakuta kule visiwani, wakibishana bila ya ugomvi kuhusu vyama vyao. Hawa ni ndugu tumbo moja. Mmoja alikuwa ni Hassan (CCM), mwingine Makame(CUF). Mazungumzo yao niliyanasa kwenye kinasa sauti, yalikuwa kama yafuatavyo: HASSAN: Nyie CUF mna nini, midevu tu? MAKAME: Kwani nyie mna nini, vipara tu na vitambi? HASSAN: Nyinyi mtakoma safari hii. Kampeni zetu hamziwezi, si umeuona mchuma, lile gari lenye choo ndani? MAKAME: Khe! Weye ndio hata hutumii akili. Kwa nini wakanunua gari ina choo ndani, si wanajua kule vijijini wananchi hawana vyoo kwa jinsi maendeleo yalivyokuwa nyuma, kwa hiyo wameamua kujenga choo kwenye gari ili wakienda kwenye kampeni wasipate tabu. Sasa ni akili gani hiyo, unaowaongoza vyoo hawana, weye mwenyewe uana choo chumbani, una choo ofisini, sasa mpaka kwenye gari pia una choo. Hata mjini, stendi hakuna choo, watu wanakojoa hovyo tu. HASSAN: Wacha we, bwana. Kila kitu ni mipango tu. Wa nyuma ndio wameharibu, we huoni Rais ana huruma namna hii. Kamkuta maskini akampa laki tano hapo hapo. Nani amewahi kufanya hivyo? Au husomi magazeti weye? MAKAME: Kwenda, kama ana huruma, kwanini sikuzote hatusikii kuwapa maskini pesa? Mbona Matonya alipofukuzwa na Makamba hakumzuia ampe angalau laki moja tu. Kipofu wa watu, hana kitu, kaja mjini kuomba wanamtimua, badala ya kumpa makazi, chakula na malazi. Leo wamepanga mtu, wampe pesa, ili watoke kwenye TV na magazeti kwamba wanajali masikini. Kwa nini hilo lifanyike wakati huu wa Kampeni? HASSAN: Sasa weye huelewi kwamba jema ni jema tu hata kama limechelewa? Labda nikatishe mazungumzo yao, maana watamaliza nafasi na ya ziada itahitajika na hali haipo. La maana ni hii pointi ya mwisho ya Hassan, kwamba hata kama Rais amechelewa kuwapa pesa maskini, jema ni jema tu, hata kama limechelewa. Mimi naogeza jema ni jema tu hata kama lafanyika wakati wa kampeni. La maana ni kuwashtua wale watu ambao bado hawajapata taarifa ili wawahi wakati huduma hiyo bado inatolewa, maana ndio kwanza imeanza, na kabla haijesha. Kumbe Rais anawagaia pesa maskini, kwa hiyo tutamsaidia kumweleza maskini wako wapi, lakini kwanza tupige mbiu kwa Matonya, Mkuu wao, kwa kumwambia kwa njia yoyote ile, kwa redio, runinga, magazeti kama hivi, kwa sauti moja: "Maaatooonyaaa, Wahi huku. Fuatilia misafara. Wakati ndio huu, zinatoka! Tena kuanzia laki tano!! Wahi, Wahi!!! |
YALIYOMO
Tahariri
Kishindo cha CUF chaitikisa Dar Mamia warudisha kadi za CCM Kilwa Chama cha Mugabe chupuchupu Zimbabwe Wasikilizeni wananchi wasemavyo toka kwenye meli mbovu mkabala na Posta ya zamani CCM yakasirishwa kwa kuswaliwa Mtume (S.A.W.) Wanaomzomea Bilal waambiwa Oktoba watakula jeuri yao CCM wapoteza viti 18196; CUF yaongoza kuvinyakua Ushauri Nasaha
MAKALA
MIPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MUANDISHI
MAKALA
Lishe
RIWAYA
Pupe, Mziray wamlia ‘dip’ Shungu - |
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza
hapa
Au
Andika barua kwa: nasaha1420@yahoo.com
|
|
|
|