|
Na. 054 Jumatano Juni 28 - Julai 4, 2000 |
|
|
|
|
|
Kumbe kazi ya CCM ilikuwa kurudisha maendeleo nyuma Ndugu Mhariri, NAOMBA kwa heshima na taadhima unipe nafasi lau kwa pembeni mwa gazeti lako ili nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu kauli ya Mheshimiwa Mangula, Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha CCM, kuhusu kauli 'chafu' za Profesa Lipumba. Profesa Lipumba alisema eti CCM haijafanya lolote la maendeleo tangu tulipopata uhuru. Tangu Tanganyika kupata uhuru wake mwaka 1961 hadi leo 2000 inakaribia miaka 40. Ili kuchangia, nataka nimfahamishe Profesa Lipumba na wenzake kwa kuorodhesha baadhi ya 'mafanikio' tuliyoyapata chini ya utawala wa TANU/CCM kama ifuatavyo:- Wakati tunapata uhuru kiwango cha elimu nchini petu kilikuwa sawasawa na Kenya na vilevile Uganda. Hali ya shule zetu ingawa zilikuwa chache lakini zilikuwa na madawati na wanafunzi wakigawiwa mahitaji muhimu kama madaftari, vitabu vya rejea, kalamu, vidau vya wino na kadhalika. Kwa kuanzia pale, ilitarajiwa leo hii tungelikuwa mbali. Lakini kinyume chake leo, miaka 40 baada ya uhuru, shule zetu ni kama jela. Wakati tunapata uhuru, hospitali na vituo vya afya vichache vilivyokuwepo viliwahudumia wananchi na waliridhika. Elimu ya afya ilitolewa kwa umma na faida yake ilionekana. Mahospitalini, wagonjwa walitibiwa na kuhudumiwa kwa kuhurumiwa na kubembelezwa. Manesi na madaktari walikuwa kama wazazi kwa watoto wao. Hayo ndiyo mafunzo tuliyorithi kwa watawala wetu. Hali hiyo iliendelea kudidimia hadi sasa ambapo mgonjwa na daktari wanangaliana kama mwizi na polisi. Hivi sasa huduma nafuu lazima inunuliwe kwa fedha. Wakati tunapata uhuru miaka 40 iliyopita, nchi yetu ilikuwa na mashirika machache, mazuri yenye kutenda kazi zake kwa kuwajibika. Tulikuwa na Shrika la Reli, Shirika la Bandari na Shirika la Ndege, mazuri yaliyokuwa yakifanya kazi zake kwa moyo wa huduma. Watu wote waliridhika na huduma zake za uhakika. Yalikuwepo mashirika mengine madogo madogo, viwanda na makampuni. Baada ya miaka kadhaa, utawala ukaanza kutafuna shirika moja baada ya jingine. Huduma zikaanza kudidimia hadi kufa. Mashirika, viwanda na makampuni yaliyokuwa ya umma yakadhoofika na kufa. Wakati idadi ya watu inaongezeka, ajira zinaondoka kwa kasi kubwa sana.Viwanda vinakufa ovyo ovyo tu. Tulikuwa na viwanda kama MWATEX, SUNGURA TEX, KILTEX, MUTEX, KIWANDA CHA CHUMA TANGA, KIWANDA CHA MBOLEA na vinginevyo. Leo havipo tena. Waliokuwa wafanyakazi katika viwanda hivyo leo ni wazururaji. Vijana na wazee wao wote sasa wanaranda mitaani, hawana kazi. Hakuna shirika, hakuna kampuni ya umma. Hakuna ajira. Hiyo inahesabiwa ni hatua ya maendeleo baada ya mika 40 tangu kujitawala. Miaka kumi mara nne ya utawala wa aina moja usiowahudumia wananchi wake, na bado wananchi hao wanalazimishwa kuchagua na kuukubali utawala usiowajali wananchi. Mfanyakazi anazeekea kazini, muda wake unakwisha anastaafu, anadhulumiwa haki zake. Leo hii wafanyakaziwa Jumuia ya Afrika Mashariki fedha zao zinategemea majaliwa ya matokeo ushindi wa uchaguzi ujao. Wenyewe wanakufa kwa njaa na matatizo mengine. Wastaafu viwandani na kila mahali wanalilia mafao yao lakini hawapiti. Huo ndio utawala wa wananchi. Hayo ndiyo matunda ya uhuru baada ya miaka 40. Profesa akisema kuwa nchi inarudi nyuma badala ya kwenda mbele, anaonekana hajui kupima maendeleo. Maendeleo yanapimwa kwa kuangalia viongozi wana nyumba ngapi, magari ya fahari mangapi na watoto wangapi wa vigogo wanaosomea nchi za nje za Ulaya na Marekani. Huko ndiko kupima maendeleo. Profesa anapima maendeleo kwa kuangalia shule za kusoma watoto wa walalahoi, dispensari za kutibiwa makabwela, ajira, milo ya wananchina vitu vya namna hiyo. Hayo ni makosa.Pima maendeleo kwa kuangalia barabara wanazojenga Konoike jijini Dar, na sio madaraja mabovu ya Rufiji. Kuhusu suala la amani. Historia ya nchi ya Tanganyika hadi Tanzania ni ya amani. Hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa kuna kipindi kabla ya uhuru nchi yetu ilikosa amani. Lakini kuna ushahidi wa wazi kabisa kuonyesha namna serikali ya sasa inavyovunja misingi ya amani kwa makusudi. Kuwanyanyasa wananchi, kuwadhulumu, kukashifu dini za wananchi na kuwakashifu viongozi wao na hata kuwatupa gerezani bila makosa ya kisheria. Kwa kumalizia, nasema kuwa Profesa Lipumba anapotoa tathmini za maendeleo ya Tanzania anapaswa kwanza aonane na wataalam wa uchumi na maendeleo waliobobea. Hawa wanapatikana pale Mtaa wa Lumumba. Pale atapata data sahihi na kuzitangaza badala ya kutimia data zake za Kiprofesa ambazo hazikubaliwi Kitaifa na Kimataifa. Kama Profesa nahitaji ushahidi zaidi wa 'maendeleo' kwa kipindi cha utawala wa CCMau kujua 'mema' yaliyoletwa na Azimio la Arusha aseme. Mimi niko tayari kumsaidia. John S. Zingi,
Ndugu Mhariri, MARA nyingi tumekutana na waandishi wa habari kwenye mikutano ya siasa ya vyama vya upinzani. Tumewashuhudia wanavyohangaika kuandika, kunasa sauti, kurekodi picha na kupiga picha. Viongozi wa vyamawanazungumza sera za vyama vyao, namna watakavhoimasisha huduma zajamii, watakavyo kabiliana na umaskini uliokithiri n.k. Yapo mengi yanayosemwa kuikosoaCCM na utawala wake wa miaka 40. Cha kushangaza ni kuwa hatuoni haya kufikishwa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ambayo bila shaka moja na kazi za vyombo hivyo ni kupasha habari. Je huu ni woga kwa CCM na serikali yake? Said M. Buweta,
Ndugu Mhariri, Nimepatwa na mshituko baada ya kuona picha katika gazeti ikimuonesha katibu wa BAKWATA mkoa wa Arusha Alhaj Molel akitoa zawadi katika mashindano ya kumpata Miss Arusha. Ndiyo kusemaBAKWATA mmefika mahali hata Muumba wenu hamumuonei haya tena? Mnafahamu wazi kuwa Mungu wetu (Allah) anakataza wanawake kuwepo katika michanganyiko, anaamrisha wajistiri na mnafahamu wazi kuwa kupinga amri zaMungu ni UKAFIRI sasa tuwaweke kundi gani? Nilitaraji kuwa Bwana Mollel angekuwa ameshachukuliwa hatua za kinidhamu kwa kumtoa katika wadhifa wake. Kimya cha baraza linatufanya tuamini kuwa kweli linaupiga vita Uislamu. Daudi A.Matata,
Ndugu Mhariri, Hivi karibuni makanisa yamekuwa yakipita mashuleni kuwagawia watoto wetu biblia. Zoezi hili limefanyika katika shule nyingi ikiwepo hapa kwetu Mbagala . Nakumbuka mwaka 1986 zoezi hilo lilifanyika hapa Dar es Salaam na lilikuwa la nyumba kwa nyumba. Anwani yao wakati huo ilikuwa 'Dar imrejee Bwana'. Tulipozisoma biblia zile na kuzielewa kisha tukaanza kuzichambua kwenye mihadhara yetu, wagawaji walianza malalamiko eti dini yao inakashifiwa. Ni matumaini yangu kuwa safari hii hapatatokea tena lawama na kuwa wale wanaoona kuwa wana uhuru wa kugawa biblia kwa watoto wetu watahubili pia uhuni wa wengine kuhubiri jinsi walivyosoma na kuzielewa biblia hizo. Abdallah O.Sabaya,
|
YALIYOMO
Tahariri
Kishindo cha CUF chaitikisa Dar Mamia warudisha kadi za CCM Kilwa Chama cha Mugabe chupuchupu Zimbabwe Wasikilizeni wananchi wasemavyo toka kwenye meli mbovu mkabala na Posta ya zamani CCM yakasirishwa kwa kuswaliwa Mtume (S.A.W.) Wanaomzomea Bilal waambiwa Oktoba watakula jeuri yao CCM wapoteza viti 18196; CUF yaongoza kuvinyakua Ushauri Nasaha
MAKALA
MIPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MUANDISHI
MAKALA
Lishe
RIWAYA
Pupe, Mziray wamlia ‘dip’ Shungu - |
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza
hapa
Au
Andika barua kwa: nasaha1420@yahoo.com
|
|
|
|