|
AN-NUUR
|
| Mafundisho
ya Qur'an
Dhikiri maana yake nini - 2 KUKEMEA viumbe wenye makosa, kuwaepushia hatari viumbe, kuwaokoa viumbe, kulinda amani na utulivu, kupiga na v ita, kujenga nyumba, kununua samani, kununua gari, kusoma, kuandika, kutoa elimu, kujielimisha, kufagia, kutembea, kuangalia televisheni, kusikiliza redio, kula vizuri, kutoa ushahidi, kushuhudia adhabu, kuepuka zinaa, kuepuka ulevi kutotekeleza nia mbaya, kumpa mtu haki yake, kufanya uchaguzi tuhuma. Kutafakari maumbile, kuzitafakari neema za Allah, kufanya ukarimu n.k. haya yote ni ibada iwapo yatafanywa kama atakavyo Mwenyezi Mungu kwa kuzingatika hadith nasunna za Mtume (s.a.w.). Hiyo ndiyo maana halisi ya kufuata Swira'twa-Mustaqima yaani njia iliyonyooka ambayo, katika kila rakaa ya sala tunamuomba Allah atuoneshe. Ombi hili limo katika surati-fatiha. Mwanzoni mwa sura hii tunahisi kwamba shukurani zote anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliyetupa neema zote (Ar-Rahmani-r-Rahim). Vilevile katika surati Dahr aya ya 3, Allah anasema: .......Hakika sisi tumembainishia (binadamu) njia zote mbili, ya kheri na ya shari. Basi Mwenyewe tena atakuwa mwenye shukurani au awe mwenye kukufuru. Kwanasaba wa aya hiyo, maana halisi ya kumshukuru Allah kwa neema zote alizotupa ni kufuata njia yakeyaani kutekeleza amri au maelekezo yake katika kila jambo tulifanyalo. Kushukuru kwa kutamka tu Al-hamdullillah hakutoshi kwani hata mtu aliyeshiba kwa riziki kya haramu anaweza pia kusema Al-hamduli Llah! Hata watu madhalimu kama Makumba au Amini wanaweza kusema Al-hamdulillah wakishiba. Hii si kshukurani bali ni dhihaka kama vile kusema "asante kMungu kwa kunipa riziki kwa njia za haramu. Kwa hiyo kumshukuru Mungu sio tu kusema Al-hamdul baada kushiba au kufanickiwa kupata neema fulani bali pia kuhakikisha kwamba kile kilichokushibisha kimepatikana na kuliwa kwa mujibu wa muongozo wa huyo tunayemshukuru (Allah). Viv yo hivyo, kutamka tu bismillah bila kuhakikisha kama lile tulifanyalo linaridhiwa na Allah au la ni kumfanyia masihara Mwenyezi Mungu - Astaghafirullah. Ni hatia kulitaja jina la Allah katika jambo lililo kinyume na muongozo wake isip;okuwa kwa kulazimika kama v ile kula nyama ya nguruwe kwa shurutisho la njaa jambo ambalo pia ni ibada. Mifano yote hiyo yadhihirisha jinsi ibada inavyowachunga Waislamu wasitoke nje ya utaratibu wa maisha wa Kiislamu na hii ndiyo tafrsi sahihi ya neno dini.Hivyo, maana ya ibada saio kuachana na dunia na badala yake kujibanza upwekeni au misikitini. Bali ibada, kama tulivyoona, ni kufanya shughuli zote na mambo yote kwa kuzingatia maelekezo ya Allah. La muhimu ni kurfejea katika Qur'an na Sunna za Mtume (s.a.w.) ili mtu aweze kujua namna gani akiendee kila kipengele cha maisha yake ya kila siku. Umuhimu wa dhikiri Tumeona kwamba ibada humfanya mtu asitoke nje ya utaratibu wa maisha wa Kiislamu. Kwa upande mwingine dhikiri nayo humafanya mtu asitoke nje ya ibada. Dhikiri humsaidia muuminikwa namna mbili. Mosi khumsaidia kuepluka kutenda jambo lolote lililoharamishwa na Allah, na pili humsukuma mtu kuomba toba upesi upesi pale anapotetereka kutokana na udhaifu wa kibinaadamu. Kwa ujumla dhikiri ndio silaha muhimu ya kupambana na matamanio ya nafsi yanayotiwa nguvu na vishawishi vya shetani. Bila kumdhukuru (kumkumbuka) Allah katika kila nukta ya uhai wetu, ni vigumu kujizuia na tamaa mbaya ya nafsi na kumshinda shetani na kwa hali hiyo, ni vigumu kulifikia lengo la maisha yetu na hiv yo hata zile ibada maalumu za kutuandaa kama vile sala zitakuwa hazina faida yoyote. Isitoshe kitendo cha kumsahau Mwenyezi Mungu, humfanya malaika aandikaye mema awe mapumzikoni na yule aandikaye maovu awe na kazi kubwa. Kwa hiyo basi, dhikiri ndio msingi imara wa uadilifu kwani mtu amkumbukae Allah muda wote huweza kuepuka uovu hata kama yukjo peke yake faraghani, gizani, chumbani, uchoochoroni, kichakani, darini, uvunguni, pangoni, msituni na kwingineko. Lengo la Swala Tumeona kuwa dhikiri ndiyo inayomfanya mtu asitoke nje ya ibada. Kwa upande wake, sala nayo humfanya mtu asiondokwe na dhikiri. Kimaumbile, kumkumbuka Allah muda wote sio kazi nyepesi kwa sababu ndani ya nafsi zetu kuna shetani ambaye daima hutushawishi tumfuate yeye na pia kuna mashetani wengine wengi wa nje ambao kwa mbinu mbali mbali hutuchochea tuwafuate. Ndijo maana Allah (s.w.)ametuwekea sala ili itudumishie utumaduni wa kumkumbuka yeye muda wote. Mara tu tuamkapo asubuhi tunasali alfajiri ili kukumbushwa wajibuy wetu. Na wakati tuko katika shughuli zetu saka ubatwita tena mara tatu zaidi, dhuhuri, Alasiri na Magharibi, lengo likiwa ni lilelile la kutukumbusha tusighafirike na ule wajibu wetu wa kuishi na kufanya shughuli zetu kwa kuzingatia mipaka ya Allah: "Na itakapokwisha sala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu na mkumbukeni Mwenyezi Mungbu kwa wingi (ilimsipatge kufanya mabaya), ili mpate kufaulu.(61:10). Na hatimaye, kabla ya kwenda kulala tunakumbushwa tena wajibu wetu katika sala ya Isha. Hasara ya kutomkumbula Allah Basi siku hiyo italetwa jahanamu. Siku hiyo mwanaadamu atakumbuka, lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? (89:23). Kulingana na aya hii, Salama ya bindamu siku ya Kiama itapatikana iwapo aliishi maisha yake ya duniani kwa kumbukumbuka Mola wsake.Lakini kama ameishi duniani bila kukumbuka wajibu wake wa kumtii Allah katika kila jambo alilofan ya, kisha aje akumbuke wajibu huo siku ya Kiama wakati atakapouona moto, dhikiri au kumbukumbu hiyo haitomsaidia chochote. Itakuwa sawa na mtu aliyekumbuka jawabu la Swali baada ya kutoka katika chumba cha mtihani. |
YALIYOMO
TAHARIRI Iran ina agenda gani? Mauaji,udhalilishaji Mwembechai: Wanawake
Waislamu waandamana Tabora Na Mwandishi Wetu 'Serikali ieleze hatua iliyochukua
kuhusu mauaji Mwembechai' ‘Musiwasingizie wake zenu maovu’
Barua za wasomaji
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org