AN-NUUR
Na.168 Jamadul Akhir 1419, Septembe 24 - Oktoba 1, 1998

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita

 

Matangazo


Majumuwati Secondary School

NAFASI ZA MASOMO 1999

Mkuu wa Shule anatangaza nafasi za masomo ya Kidato cha Kwanza 1999.

Fomu zinapatikana shuleni Msikitini Temeke Mwisho kila siku kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 7.00 mchana kwa gharama ya shilingi 2,000/- (alfu mbili)

Pia nafasi za kidato cha pili na tatu 1999 zinapatikana.

Usichelewe, wahi nafasi sasa.

Uongozi




Al-Farooq Boys Sec. School

Nafasi za kidato cha kwanza 1999

Form kwa ajili ya nafasi za masomo kidato cha kwanza 1999 zinapatikana sehemu zifuatazo:

1. Ofisi ya Mkuu wa Shule Al-Farooq, Tabata.

2. Ofisi ya gazeti la AN-NUUR Kariakoo mtaa wa

Mahiwa/Livingstone karibu na Msikiti wa Mtoro.

Siku ya mwisho kuchukua na kurudisha form ni tarehe 2/12/1998.

Mtihani wa usaili utafanyika shuleni Tabata tarehe 5/12/1998, saa 2 kamili asubuhi.




MASOMO YA ZIADA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUINGIA FORM I - 1999

Masomo yataanza tarehe 15/10/1998 hadi tarehe 15/1/1999.

Kila mwezi ada ni Tshs 10,000/=.

Masomo yatakayofundishwa ni Hesabu, Kiingereza na maarifa ya Uislamu.

MKUU WA SHULE



Bismillahir Rahmanir Rahiim

Ridhwaa seminary secondary school

NAFASI ZA MASOMO 1999

Shule ya Sekondari ya Kiislamu Ridhwaa iliyoko Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam inatangaza nafasi za masomo kwa Kidato cha kwanza (Form One) kwa mwaka 1999.

Fomu zinaanza kutolewa kuanzia tarehe 28/09/2998. Fomu hutolewa kwa Tshs 4,000/- (Elfu nne tu).

Shule itatoa mafunzo maalum kabla ya mtihani wa kujiunga na Kidato cha kwanza. Kuanzia tarehe 6/10/1998. Watakaopenda kujiunga watatakiwa kulipa Tshs. 7,000/- (Elfu saba tu).

Ni matumaini ya shule kuwa masomo haya yatawawezesha wanafunzi kufaulu mtihani wa kujiunga na Kidato cha Kwanza.

INSHALLAH.

TAFADHALI WAHI FOMU KWA AJILI YA MWANAO

WABILLAH TAWFIQ

MKUU WA SHULE


Vitu mbalimbali vinauzwa

Tunauza bidhaa mbalimbali za nyumbani na zawadi za harusi kwa bei nafuu kabisa.

Huduma za kufunga bure.

Njooni muone Kisakapwike

Mtaa wa Swahili/Narung'ombe,

Simu 180902


Ubungo Islamic High School

Maombi ya kujiunga na Kidato cha Kwanza 1999

Fomu za kujiunga na Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya Kiislamu Ubungo, zinapatikana shuleni Ubungo na katika ofisi ya gazeti la ANNUUR Mtaa wa Mahiwa/Livingstone Kariakoo Dar es Salaam.

Mwisho wa kuchukua fomu na kurejesha fomu ni tarehe 25/11/1998.

Mtihani wa kujiunga (Qualifying test) utafanyika tarehe 28/11/1998 saa 2 asubuhi.

MKUU WA SHULE


SEMINA

Waislamu wa mkoa wa Ruvuma mnaarifiwa semina itakayofanyika Songea Mjini siku ya Jumapili ya tarehe 4/10/1998.

MADA KUU: Nafasi ya Waislamu wa Ruvuma katika maendeleo ya Tanzania.

MUDA: Saa 2.00 asubuhi hadi 12.00 jioni.

UKUMBI: Shule ya sekondari ya Kiislamu ya Msamala.

WALENGWA: Waislamu (wake kwa waume)

WENYEJI: Mfuko wa Maendeleo ya Elimu kwa Waislamu Ruvuma (RUMEDTF)

WAENDESHAJI: Chama cha wanataaluma Waislamu (TAMPRO)

Katibu Mtendaji

TAMPRO MAKAO MAKUU,

Simu: 762144 (off),

DAR ES SALAAM.


MAFUNZO:

Jumuiya ya Wanataaluma wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO) itatoa mafunzo maalum ya Ualimu wa shule za awali.

1. WALENGWA:

a) Wanawake wote wa Kiislamu ambao ni walimu wa vituo vya watoto wadogo (chekechea).

b) Wanawake wote wa Kiislamu ambao wanaokusudia kufanya kazi hiyo ambao wamehitimu kidato cha IV na VI.

2. MUDA WA MAFUNZO:

a) Miezi sita (6), miezi mitatu (3), nadharia na miezi mitatu mazoezi kufundisha.

b) Mafunzo yataanza Inshaallah Novemba 2, 1998, Jumatatu - Ijumaa saa 8 mchana - saa 11 jioni.

3. MASOMO:

- Saikolojia ya watoto

- Mbinu za ufundishaji watoto (Methodology)

- Jinsi ya kutumia vitendo (teaching aids materials)

- Kiingereza

- Elimu ya jamii

- Maarifa ya Kiislamu

-Uongozi.

4. GHARAMA:

Gharama ya masomo ni Tshs 80,000/- kwa miezi sita.

5. MAOMBI:

- Mwisho wa maombi ni tarehe 25/10/1998.

- Usaili (Interview) kufanyika 25/10/1998 katika ofisi ya TAMPRO Masjid Ridhwaa Kinondoni saa 3.00 asubuhi (usaili kwa washiriki wa Dar tu).

- Fomu za kujiandikisha ni Tshs. 1000/- tu.

Fomu zinapatikana (a) Ofisi ya gazeti la ANNUUR

(b) Ofisi ya TAMPRO

Nafasi ni thelathini (30) tu, wahi mapema

Kwa maelezo zaidi piga simu 762144, 181365 na 45125 (usiku) Mobile: 0811 600145.


NAFASI ZA MASOMO KWA

DARASA LA I, 1999 ZINAPATIKANA

Fomu za maombi zinapatikana shuleni kuanzia sasa.

Tarehe ya mwisho kurudisha fomi ni Jumapili 15/11/1998.

Tarehe ya usaili wa wanafunzi ni Jumatano tarehe 18/11/1998.

Na watakaochaguliwa watatangazwa Ijumaa tarehe 20/11/1998.

Kwa maelezo zaidi fika shuleni.

Uongozi wa shule


Bismillahir Rahmanir Rahim

Muhadhara wa wanawake

Wanawake wa Kiislamu wanawaalika wanawake wenzao katika Muhadhara:

Utakaofanyika: Katika Msikiti wa Manyema

Siku: Jumamosi

Tarehe: 26/9/1998

Saa: Kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana

Mada: Haki za mwanamke. Ndoa na talaka, Sababu zinazopelekea ndoa kuvunjika na njia ya kuepusha talaka.

Vile vile kutakuwa na kuchangia mada.

Wabilahi Tawfiq

DA'AWAH GROUP

SALAFIYYA WOMEN


Hafla ya kuchangia kujenga upya Msikiti Ngazija

(Mtaa wa Sewa/India, Dar es Salaam)

Al-Masjid Rahmaan (zamani Makuti)

Box 67619 Manzese Argentina, Dar es Salaam

Waumini wa Msikiti wa Masjid Rahmaan wanaowaomba Waislamu wote na Jumuiya za Kiislamu kuwasaidia katika ujenzi wa Msikiti.

Kuchangia: Mbao, mirunda, cementi, tofari pia fedha kwa ajili ya gharama za mafundi na vifaa vingene.

Akaunti yetu ni 6590890006 Tawi la Ubungo.

Mawasiliano zaidi piga simu 43128 Uongozi wa Msikiti

Simu 180653 Fuad Hassan.

Tunashukuru kwa mshikamano

Wabillah Taufiq


Usiku Adhimu

(Usomaji wa Qur'an Tukufu, Qasida, Maulidi ya Homu, n.k)

Na Chakula cha Usiku

Mahali: Diamond Jubilee

Tarehe: Siku ya Jumamosi 10/10/1998

Wakati: Kuanzia saa 2.30 usiku (baada ya sala)

Kiingilio: Shs 15,000 na 50,000/-

Mgeni wa Heshima: Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi


KUTAKUWA NA MNADA

Bismillahir Rahmanir Rahim

Tanzania Muslim Youth Association (TAYMA)

Temeke Muslim Secondary School

Mandela/Taifa Road Opp. National Stadium

P.O. Box 45245; Tel: 850710,

Dar es Salaam


Bismillahir Rahmanir Rahiym

ORIENTATION COURSE

KUJIANDAA KUINGIA KIDATO CHA I KATIKA SHULE ZA SEKONDARI NA SEMINARI ZA KIISLAMU - 1999

MASOMO: Elimu ya dini ya Kiislamu English, Hisabati, maarifa

KUANZIA: Tarehe 05 Oktoba, 1998

WALIMU: wa Sekondari, wazoefu & Mabingwa

MALIPO: Nafuu sana, fomu ni Tshs. 1,000/- tu

UZOEFU: Tumepasisha 99% 1994 - 1997

Jiandikishe: IEC Centre, Mtaa wa Udoe No. 24 Kariakoo

(Kwa mkata kimeo)

WAHI, TUNAZO NAFASI CHACHE

MKURUGENZI

Islamic Education Consultancy Centre

P.O. Box 72442, Fax 181077, Tel: 181176


Tanzania Universal Qur'anic College

P.O. Box 20486, DAR ES SALAAM

Chuo cha Tanzania Universal Qur'anic College kinatoa nafasi za masomo ya ufundi wa kushona nguo za kiume na za kike.

Mafunzo ni ya kitaalamu na waalimu ni wazoefu.

SIFA:

1. Waliomaliza darasa la 7 na kuendelea.

2. Umri wowote.

Fomu zinapatikana Chuoni.

Mwisho wa kujiandikisha ni tarehe 4/10/1998 na masomo yataanza tarehe 05/10/1998.

Wahi kujiandikisha nafasi ni chache

Chuo kipo barabara ya Kigogo karibu na CCM Ubungo Kisiwani.

MKUU WA SHULE (CHUO)


Jumuiya ya Wanawake Waislamu Sinza, Dar

Mwaliko wa Mhadhara

Umoja wa Wanawake wa Kiislamu wa Masjid Annuur, Sinza una furaha kuwaalika wanawake wote wa Kiislamu wa mkoa wa Dar es Salaam katika muhadhara utakaofanyika Insha Allah siku ya Jumamosi tarehe 10/10/1998 kuanzia saa 2.00 asubuhi hasi saa 6.00 mchana Masjid Annuur, Sinza karibu na kituo cha basi cha hospitali ya Palestina.

Kufika kwenu ni kutekeleza amri ya Allah (sw) ya kuamrishana mema na kukatazana maovu.

MADA: Umoja na Mshikamano kwa Waislamu na madhara ya kutengana

WAHADHIRI: Mada itachangiwa na Wahadhiri mbalimbali kwa mfumo wa mjadala


Nafasi za masomo 1999

Assalaam Alaykum wa Rahmatullah wa Barakaatuh

Wote mnatangaziwa nafasi za masomo ya Kidato cha Kwanza mwaka 1999, kwa vijana waliomaliza darasa la saba.

Fomu za maombi ya masomo zinapatikana:

1. Temeke Muslim Secondary School (Masjidil-Amin - Uwanja wa Taifa).

2. Islamic Education Consultancy - Ust. Fundi.

3. Ofisi ya TAYMA iliyo karibu - Kwa maelezo zaidi.

4. Ofisi ya Gazeti la ANNUUR - Karibu na Msikiti wa Mtoro, Kariakoo.

* Fomu zinapatikana kwa sadaka ya Tshs. 2,500/-

* Kutakuwa na kozi ya "Pre - Form One 99" itakayoanza tarehe 05/10/1998.

* Usaili (Interview) itafanyika tarehe 14/12/1998 -

Interview ni kwa wale watakaoshiriki "Pre - Form Orientation Course" tu.

Wabillahit-Taufiiq

MKUU WA SHULE


Kwa wale watakaobahatika kutoa sadaka zao kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti na Madrasa ya Masjid Nuru Mriti.

Mahitaji muhimu kwa awamu ya kwanza ni kama yafuatavyo:

1. Bati za mita tatu kiasi cha bati 200.

2. Cement kiasi cha mifuko 2000.

3. Misumari ya bati kiasi cha kilo 50

4. Mchanga kiasi cha lori 20

5. Mbao 2"x 4"x9' - mbao 400

2"x3" x9' - mbao 500

Kwa wale walioko mikoa ya Dar na Pwani wanaweza kupitishia michango yao ofisi ya Gazeti la AN-NUUR au kwa pesa taslimu waweza kupeleka moja kwa moja katika Akaunti ya Masjid Nuru iliyoko Benki ya Posta Tawi la Kariakoo Akaunti Na. 10-13893 -7.

Kwa wale walioko mikoa ya Kilimanjaro na Arusha wanaweza kupitisha vifaa vyao ofisi za Shabaha Bus Service au Mwanga au kuwasiliana:

S.L.Posta 7160,

Ugweno.

HABIB A. MCHARO

KATIBU WA KAMATI YA UJENZI KANDA YA DSM

Juu 
 

YALIYOMO  
 
TAHARIRI 
Iran ina agenda gani?

Mauaji,udhalilishaji Mwembechai: Wanawake Waislamu waandamana Tabora Na Mwandishi Wetu

BUCHA YA NYAMA YA NGURUWE KATIKATI YA WAISLAMU
Na Mwandishi Wetu

'Serikali ieleze hatua iliyochukua kuhusu mauaji Mwembechai'
Na Kassim Juma

Vijana wa Kiislamu wajiimarisha Bukoba
Na Nooh Mustafa, Bukoba

Sheikh Mzonge awataka Waislamu Moshi wasimamishe swala
Na Ashraf Yussuf, Moshi

TAMKO LA PAMOJA LA MISIKITI SABA YA MWANZA-KUPINGA OMBI LA BAKWATA KWA SERIKALI LA KUIFUTIA USAJILI WAKE

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 7

MAKALA: Baadhi ya Watanzania wangali wanaishi ‘Tanganyika’
Na Mwandishi Wetu

HOJA BINAFSI: Maendeleo ya Tanzania ni ndoto
Na Fatma Mussa

‘Musiwasingizie wake zenu maovu’
Na Habiba Swedi, Arusha

Wanafunzi Waislamu Songea wapata viongozi
Na Mwandishi Wetu, Songea

Kikundi cha wanawake wa Kiislamu Bi. Khadija – Dodoma
Na Abu Zuberi, Dodoma

Waahidi kutekeleza majukumu kwa jina la Allah
Na Habiba Swedi, Arusha

Arumeru wahitaji Da’awa
Na habiba Swedi, Arusha

Wanawake wa Kiislamu wazungumzia maendeleo yao

Kauli ya wanawake wa Kiislamu Iringa kuhusu kadhia ya Mwembechai

Uislamu ulivyoingia Zanzibar

Wanawake Singida walaani mauaji Mwembechai Wamchangia Mama Chuki 17,000/-
Na Mwandishi Wetu

Sekondari ya Kiislamu kujengwa Maere Tanga
Na Abu Abdullah, Tanga

Sheikh ahimiza Waislamu Lindi wafuate mafunzo ya Uislamu
Na Mohamed Mussa, Lindi

Sheikh Zuberi awataka Waislamu Dodoma kuimarisha Misikiti
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mafundisho ya Quran 
Dhikiri maana yake nini? - 2

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Matatizo ya tumbo yanayosababishwa na utumiaji wa maziwa

Matangazo 

 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org  

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita