|
AN-NUUR
|
| LISHE
Matatizo ya tumbo yanayosababishwa na utumiaji wa maziwa Na Mujahiid Mwinyimvua BAADHI ya watu hupata matatizo ya tumbo mara tu wanapokunywa maziwa. Matatizo hayo ni kama vile kuliona tumbo zito, kujaa gesi (hewa) na wengine hufikia hatua ya kuharisha. Mtu mwenye hali hiyo hujulikana kuwa ana tatizo la tumbo lake kushindwa kusaga chakula cha Laktosi (Lactose). Kwa kimombo hali hiyo hujulikana kama Lactose intolerance. Takriban watu asilimia sabini (70%) duniani wanasumbuliwa na Lactose intolerance. Tatizo hilo linaweza kuleta athari mbaya katika lishe ya binadamu, hivyo basi ni vyema tukaitazama dhana hiyo japo kwa kiasi kidogo. Katika maziwa kuna virutubisho kadhaa, kimojawapo kinaitwa Lactosi (Lactose). Kimaumbile, mwili (utumbo) wa binadamu una vitu vinavyosaga chakula. Vitu hivyo vinaitwa vimeng'enyo (Enzymes). Aina moja ya kimeng'enyo ni Lactase, 'Lactase' husaga chakula kinachoitwa laktosi (ambacho nimekitaja awali) na baada ya kusagwa hutumiwa na mwili. Mtoto anapozaliwa huwa na kimeng'enyo lactase ambacho humwezesha kusaga maziwa anayonyonya kutoka kwa mamake. Mtoto anavyozidi kukua ndivyo idadi ya 'Lactase' inavyopungua. Kwa baadhi ya watu wazima 'Lactase' hupotea kabisa (haizalishwi). Inapotokea hali hiyo, Laktosi ya kwenye maziwa anayonyonya mtu huwa haisagwi kwa njia ya kawaida na yenye manufaa katika mwili. Badala yake, bakteria (vijidudu) waliomo katika utumbo hukisaga chakula hicho (Laktosi) na kutoa hewa/gesi (CO2 na H2). Hewa hiyo hulifanya tumbo kujaa na kwa baadhi hufikia hatua ya kuharisha. Kitendo cha kuharisha ni cha hatari, kwa sababu kinapoteza maji na virutubisho vingine. Baadhi ya watu hasa wafugaji huwa hawana kabisa matatizo ya 'Lactose intolerance'. Sababu ya hali hiyo bado haijawa wazi kwa wanasayansi. Hivyo, elimu ya sayansi inasaidia kwa kiwango kikubwa kukabiliana na tatizo la 'Lactosse Intolerance'. Mbinu ya kwanza ni kuwa, watu wenye matatizo watumie maziwa yaliyochachuka ( mtindi/yoghurt). Mbinu ya pili, ni kunywa maziwa pamoja na kitu kinachoitwa 'Lact-Aid'. Kitu hicho kinafanya kazi kama 'Lactase (kimeng'enyo). 'Lact-Aid hupatikana maduka ya dawa, maduka ya vyakula n.k. Watu wenye matatizo ya 'Lactose Intolerance' wasisuse kutumia maziwa bali wafuate ushauri wa hapo juu. Maziwa ni chakula kizuri na ni chanzo muhimu cha madini ya Kasiam (Calcium). Madini hayo muhimu zaidi kwa kina mama wanaonyonyesha na wale wajawazito. Kwa wale wanaotumia, watumie maziwa yaliyoongezwa vitamini D. Vitamini D ni muhimu pamoja na kazi nyingine kuuwezesha mwili kuweza kuyatumia vizuri madini ya Kasiam. |
YALIYOMO
TAHARIRI Iran ina agenda gani? Mauaji,udhalilishaji Mwembechai: Wanawake
Waislamu waandamana Tabora Na Mwandishi Wetu 'Serikali ieleze hatua iliyochukua
kuhusu mauaji Mwembechai' ‘Musiwasingizie wake zenu maovu’
Barua za wasomaji
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org