AN-NUUR
Na.168 Jamadul Akhir 1419, Septembe 24 - Oktoba 1, 1998

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita

 

BUCHA YA NYAMA YA NGURUWE KATIKATI YA WAISLAMU
  • Mirerani waazimia kuondoa shirki
  • Serikali yaingilia kati
  • Yaahidi kuondoa bucha la nguruwe

Na Mwandishi Wetu

WAISLAMU wa Mirerani wiki iliyopita waliazimia 'kulishughulikia' bucha moja la nyama ya nguruwe mjini hapo baada ya malalamiko yao kutokusikilizwa.

Haikuweza kufahamika mara moja kwamba ni hatua gani wangechukua, lakini Waislamu hao walikuwa wameamua kuswali Ijumaa ya pamoja ambapo baada ya swala wangepeana maelekezo nini cha kufanya. Ijumaa hiyo maalum ilikuwa iswaliwe Septemba 18, mwaka huu.

Hata hivyo, muda mfupi kabla ya Ijumaa hiyo kusimama, uongozi wa serikali ngazi ya kata ulileta barua kwa Waislamu ikieleza kwamba serikali inachukua hatua kuondoa bucha hiyo.

Barua hiyo yenye kumb. Na. WEO/MRN/ML/Vol.11/78 ya Septemba 18 kutoka ofisi ya Mtendaji Kata iliwaarifu Waislamu kwamba bucha hilo la nyama ya nguruwe litahamishiwa sehemu nyingine isiyo na madhara na Waislamu.

Bucha hilo linalomilikiwa na Bw. E. Urio lipo mtaa wa Zaire eneo la Kijiweni ambapo ni eneo la maduka na makazi ya watu.

Awali, Waislamu wa Mirerani waliandika barua serikalini kulalamikia kuwepo kwa bucha hilo ambalo walidai kwamba mara nyingi nyama ya ng'ombe na nguruwe imekuwa ikipimwa kwenye mizani moja.

Juu 
 

YALIYOMO  
 
TAHARIRI 
Iran ina agenda gani?

Mauaji,udhalilishaji Mwembechai: Wanawake Waislamu waandamana Tabora Na Mwandishi Wetu

BUCHA YA NYAMA YA NGURUWE KATIKATI YA WAISLAMU
Na Mwandishi Wetu

'Serikali ieleze hatua iliyochukua kuhusu mauaji Mwembechai'
Na Kassim Juma

Vijana wa Kiislamu wajiimarisha Bukoba
Na Nooh Mustafa, Bukoba

Sheikh Mzonge awataka Waislamu Moshi wasimamishe swala
Na Ashraf Yussuf, Moshi

TAMKO LA PAMOJA LA MISIKITI SABA YA MWANZA-KUPINGA OMBI LA BAKWATA KWA SERIKALI LA KUIFUTIA USAJILI WAKE

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 7

MAKALA: Baadhi ya Watanzania wangali wanaishi ‘Tanganyika’
Na Mwandishi Wetu

HOJA BINAFSI: Maendeleo ya Tanzania ni ndoto
Na Fatma Mussa

‘Musiwasingizie wake zenu maovu’
Na Habiba Swedi, Arusha

Wanafunzi Waislamu Songea wapata viongozi
Na Mwandishi Wetu, Songea

Kikundi cha wanawake wa Kiislamu Bi. Khadija – Dodoma
Na Abu Zuberi, Dodoma

Waahidi kutekeleza majukumu kwa jina la Allah
Na Habiba Swedi, Arusha

Arumeru wahitaji Da’awa
Na habiba Swedi, Arusha

Wanawake wa Kiislamu wazungumzia maendeleo yao

Kauli ya wanawake wa Kiislamu Iringa kuhusu kadhia ya Mwembechai

Uislamu ulivyoingia Zanzibar

Wanawake Singida walaani mauaji Mwembechai Wamchangia Mama Chuki 17,000/-
Na Mwandishi Wetu

Sekondari ya Kiislamu kujengwa Maere Tanga
Na Abu Abdullah, Tanga

Sheikh ahimiza Waislamu Lindi wafuate mafunzo ya Uislamu
Na Mohamed Mussa, Lindi

Sheikh Zuberi awataka Waislamu Dodoma kuimarisha Misikiti
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mafundisho ya Quran 
Dhikiri maana yake nini? - 2

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Matatizo ya tumbo yanayosababishwa na utumiaji wa maziwa

Matangazo 
 

 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org  

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita