AN-NUUR
Na.168 Jamadul Akhir 1419, Septembe 24 - Oktoba 1, 1998

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita

 

Makala ya Mtangazaji

Na Nooh Mustafa, Bukoba

Bismillahir Rahmaani Rahiym

KAMATI MAALUM YA UMOJA WA MISIKITI SABA MWANZA

S.L.P. 2353, MWANZA

TAMKO LA PAMOJA LA MISIKITI SABA YA MWANZA-KUPINGA OMBI LA BAKWATA KWA SERIKALI LA KUIFUTIA USAJILI WAKE

PRFESS RELEASE

UTANGULIZI

Waumini wa misikiti saba ya Mwanza inayotakiwa na Bakwata ifutwe wameshtushwa sana na tamko la hivi karibuni la Bakwata kupitia gazeti la Majira Na. 1719 la Alhamisi, Septemba, 17, 1998 la kuiomba Serikali ifute usajili wa misikiti hiyo ambayo ni Masjid Luqman (Mkuyuni), Masjid Tawfiq (Igogo); Masjid Taqwa (Nyamanoro); Masjid Raudhwa (Lumumba); Masjid Islamiyyah (Nyakato), Masjid Safina (Mecco) na Masjid Arafa (Mabatini).

USHAHIDI WA KAULI HII YA BAKWATA

Kwa mujibu wa gazeti hilo la majira, barua mbili za Bakwata zimenukuliwa:

(i) Barua kumb. Na. BKT/MZ/96/20 ya Oktoba 20, 1996 iliyoandikwa na Katibu wa Bakwata Mkoa wa Mwanza na

(ii) Barua Na. R/009/II/IV/115 ya Agosti 26, 1998 iliyoandikwa na Katibu mtendaji wa Bakwata, Taifa Sheikh Rajab Kundya kwenda kwa Kabidhi Wasii wa Serikali.

SABABU ZA BAKWATA KUOMBA KUFUTIWA USAJILI MISIKITI HII SABA NA MAJIBU YETU:

1.0 MISIKITI ILISAJILIWA KIMAKOSA NA SERIKALI:

1.1 Tumeshangazwa sana kuona Serikali inakosea katika kusajili misikiti yote saba na kwa wanasheria wa Bakwata wakaona makosa haya ya Serikali.

1.2 Lakini Bakwata haikuisaidia Serikali kuikumbusha ni kifungu namba ngapi cha sheria ama za usajili kimekiukwa au hata cha Katiba ya Bakwata au hata Qur'ani tukufu au Hadithi za Mtume (S.A.W.).

1.3 Aidha ni tokana na chuki, uongo na uzushi wa Bakwata kuingiza hata ile misikiti ambayo hapo tarehe 20 Oktoba, 1996 ilikuwa haijasajiliwa na mingine bado kabisa haijasajiliwa hadi leo kama ifuatavyo:-

(i) Masjid - Islamiyyah - Nyakato - ulisajiliwa 1997

(ii) Masjid - Taqwa - Nyamanoro - ulisajiliwa 1998

(iii) Masjid - Luqman - Mkuyuni - uilisajiliwa 1997

(iv) Masjid Arafa - Mabatini - ulisajiliwa 1997

(v) Masjid - Safina - Mecco - bado haujasajiliwa hadi leo.

Kwa Bakwata kutotoa hoja zenye nguvu, tunasema bado Serikali iliisajili misikiti kihalali na kwa mujibu wa Sheria.

2.0 MISIKITI ILIYOSAJILIWA HAIKUPATA BARAKA ZA BAKWATA

2.1 Ni ajabu kusikia Bakwata nayo sasa inatoa baraka wakati mtoaji baraka wa dunia nzima ni Mwenyezi Mungu (S.W.) pekee.

2.2 Lakini hata kama ni kweli misikiti hiyo ingelihitaji BARAKA ZA BAKWATA KWANZA, basi tayari kuna misikiti kati ya hiyo iliishapata baraka hizo kwa mfano:- Masjid - Raudhwa ilipoanza kushughulikia idhini ya kusajiliwa mwaka 1995, ilianza kwa kupeleka maombi yake Bakwata - Mkoa - kupitia barua yake kumb. MR/GF/Vol.1/8 ya tarehe 27/11/95 ambayo ilishughulikiwa na Katibu wa Mkoa Bakwata kwenda kwa Katibu Mtendaji Bakwata Taifa - Sheikh Rajab Kunday. Basi kwa nini Bakwata iseme uongo? Ref. yao BKT/MZ/32/95/06 ya 27/11/95.

Huu ni mfano mmoja tu wa kuonyesha namna ambavyo Misikiti yetu imeheshimu Bakwata - ingawa hatudhani ilikuwa ni sharti la kisheria kwanza kupata baraka za Bakwata. Na kama kupata baraka za Bakwata ni miongoni mwa sheria za usajili, Jee Waislamu wa Ithnasheri, Ismailia, Bohora, Ibadhi na Memon walianza kwa kupata baraka za Bakwata kabla ya kusajili?

3.0 VIKUNDI HIVI VILITUMIA JINA LA BAKWATA PASIPO NA IDHINI YAKE

3.1 Kwanza, Bakwata imeridhika kuiita misikiti - kuwa ni vikundi - kauli ambayo ni ya dharau kwa misikiti hii ya Mwenyezi Mungu (S.W.) na wale wote wanaoiongoza na kufanya ibada humo.

3.2 Sio kweli kwamba jina la Bakwata lilitumika bila idhini yao. Rejea sababu ya pili hapo juu ili kuona barua tulizoiandikia Bakwata na wao wakaandika kwenda kwa Katibu Mtendaji, DSM.

4.0 KWAMBA, BAKWATA NDICHO CHOMBO KINACHOUNGANISHA JUMUIYA ZA KIISLAMU TANZANIA.

4.1 Kwa asilimia kubwa, Bakwata imekuwa ni chombo ama cha kuanzisha ama kuchochea chokochoko miongoni mwa Waislamu popote ilipo nchini.

4.2 Sisi, Waislamu wa misikiti saba ya Mwanza, tunaunga mkono kauli ya Baraza la misikiti, Tanzania iliyotolewa kupitia gazeti la Nipashe Na.01310 la Ijumaa Septemba 18, 1998 lililoandika "BARAZA LA MISIKITI LAPINGA BAKWATA". Baraza la misikiti limehofia hatua hiyo ya Bakwata kuwa "Itagawa Waislamu" "Kuzusha fujo" "Itaondoa ushirikiano uliopo" "Itazusha hofu miongoni mwa wafuasi wengi wa dini hiyo", n.k.

4.3 Ikiwa Serikali itaiendekeza Bakwata kwa kulazimisha kuwa Bakwata ni chombo kizuri cha Waislamu wakati kinaendelea kuchochea uvunjikaji wa amani, ipo hatari amani ikaathirika siku moja.

4.4 Inashangaza, badala ya kuunganisha Waislamu, Bakwata imekuwa ikiwashitaki na kuwapeleka mahakamani Waislamu na kudhoofisha au kusimamisha kabisa juhudi zao mb alimbali za maendeleo na Serikali nishaidi juu ya hili. Wamediriki kusimamisha hata ujenzi wa misikiti katika sehemu kadhaa nchini.

5.0 MSIKITI KUTOELEWANA BAKWATA HASA TOKANA NA KUPOKEA MISAADA TOKA NJE BILA KUPITISHIA KWANZA BAKWATA

5.1 Katika kuthibitisha kuwepo uelewano baina ya misikiti na Bakwata. Ofisi ya Bakwata Wilaya ya Mwanza, tangu iundwe Bakwata, imekuwa ikitumia nyumba ya waqfu iliyochini ya msikiti wa Raudhwa kwa zaidi ya miaka ishirini sasa bure, na bila malipo yoyote. Je, huku ni kuelewana au kutoelewana?

5.2 Kuhusu kupokea misaada, Misikiti yote saba inahoji, ni kwa makusudio gani Bakwata itake misaada ya misikiti yote ipitishwe kwake kwanza - kwakati watoaji misaada wanaitoa kwa ajili ya maendeleo ya misikiti wanayokusudia?

5.3 Bakwata wanauthibitisho gani kwamba misikiti hii saba imekuwa ikipokea misaada moja kwa moja kutoka nje? Hata kama itakuwa ni hivyo - jee, ni kosa mtoa sadaka kuielekeza sadaka yake moja kwa moja kwenye misikiti anayokusudia?

5.4 Sisi tunaona, kutoelewana huku kupo ndani ya Bakwata yenyewe kwa sababu muhimu zifuatazo:-

1. Uthibitisho wa kwanza ni toka kwa msemaji mkuu wa Bakwata - Taifa - Sheikh Yahya Hussein - kuwa "kuna migogoro ndani ya Bakwata. Rejea Majira Na. 1719 ya Alhamisi, Septemba 17, 1998 kukurasa wa 3.

2.Anaendelea Sheikh Yahaya na Mufti wa Bakwata katika Majira Na. 1720 ya Ijumaa Septemba 18, 1998 ukurasa wa tatu kuwa "Walisikitishwa na habari (za kufutwa kwa misikiti saba) na wakamshutumu Katibu Mtendaji wa Bakwata........)

3. Vilevile, katika maulidi ya kitaifa iliyofanyika Bagamoyo, Sheikh Omar Bafadhi alitamka wazi

wazi mbele ya Dk. Omar Ali Juma kuhusu chochoko zinazosababishwa na Bakwata nchini.

Hivyo, sio misikiti ila ni Bakwata ambayo haina uelewano si tu na misikiti, lakini na asilimia kubwa ya Waislamu wa Tanzania tokana na tabia yake isiyoridhisha.

6.0 HITIMISHO

6.1 Tunaiomba Serikali na kuwakumbusha Bakwata popote walipo nchini kwamba, wasimamie HAKI katika kudhibiti au kuacha kabisa tabia kama hizi ambazo ni za makusudi kabisa na za mara kwa mara dhidi ya maendeleo ya Uislamu nchini.

6.2 Kwani, bila hata ya kumuogopa Mwenyezi Mungu (S.W.) bado mpaka sasa Bakwata inaendelea kuwashughulisha Waislamu na agenda za mapambano, chuki na kuzidi kuudidimiza Uislamu kinyume kabisa na walivyoapa katika katiba yao pengine kwa sababu zao binafsi.

6.3 Mifano michache ya matendo maovu ya Bakwata dhidi ya Uislamu ni kama ifuatavyo:-

1. Civil Case No. 97 ya 1994 - Secretary General Bakwata vs Masjid Safina (Mecco) - (Rashid Twaha Mvumbo and others) ambapo Bakwata ilishindwa na kuamriwa kulipa gharama zote za kesi ambazo mpaka leo hawajalipa.

2. Civil Case No. 14 The Central Committee of Bakwata vs Masjid Safina (Mecco)of 1995 (Tashid Twaha Mkumbo and others) ambayo kwa mara ya pili tena Bakwata ilishindwa na kuamriwa kulipa gharama zote za kesi ambazo huwajalipa mpaka sasa.

3. Civil Case No. 12/95 Bakwata vs Masjid Tawfiq (Igogo) (Saidi Hussein, Almasi Juakali, Mbaraka Abeid) vile vile hatimaye Bakwata walishindwa katika kesi hii.

Juu 
 

YALIYOMO  
 
TAHARIRI 
Iran ina agenda gani?

Mauaji,udhalilishaji Mwembechai: Wanawake Waislamu waandamana Tabora Na Mwandishi Wetu

BUCHA YA NYAMA YA NGURUWE KATIKATI YA WAISLAMU
Na Mwandishi Wetu

'Serikali ieleze hatua iliyochukua kuhusu mauaji Mwembechai'
Na Kassim Juma

Vijana wa Kiislamu wajiimarisha Bukoba
Na Nooh Mustafa, Bukoba

Sheikh Mzonge awataka Waislamu Moshi wasimamishe swala
Na Ashraf Yussuf, Moshi

TAMKO LA PAMOJA LA MISIKITI SABA YA MWANZA-KUPINGA OMBI LA BAKWATA KWA SERIKALI LA KUIFUTIA USAJILI WAKE

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 7

MAKALA: Baadhi ya Watanzania wangali wanaishi ‘Tanganyika’
Na Mwandishi Wetu

HOJA BINAFSI: Maendeleo ya Tanzania ni ndoto
Na Fatma Mussa

‘Musiwasingizie wake zenu maovu’
Na Habiba Swedi, Arusha

Wanafunzi Waislamu Songea wapata viongozi
Na Mwandishi Wetu, Songea

Kikundi cha wanawake wa Kiislamu Bi. Khadija – Dodoma
Na Abu Zuberi, Dodoma

Waahidi kutekeleza majukumu kwa jina la Allah
Na Habiba Swedi, Arusha

Arumeru wahitaji Da’awa
Na habiba Swedi, Arusha

Wanawake wa Kiislamu wazungumzia maendeleo yao

Kauli ya wanawake wa Kiislamu Iringa kuhusu kadhia ya Mwembechai

Uislamu ulivyoingia Zanzibar

Wanawake Singida walaani mauaji Mwembechai Wamchangia Mama Chuki 17,000/-
Na Mwandishi Wetu

Sekondari ya Kiislamu kujengwa Maere Tanga
Na Abu Abdullah, Tanga

Sheikh ahimiza Waislamu Lindi wafuate mafunzo ya Uislamu
Na Mohamed Mussa, Lindi

Sheikh Zuberi awataka Waislamu Dodoma kuimarisha Misikiti
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mafundisho ya Quran 
Dhikiri maana yake nini? - 2

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Matatizo ya tumbo yanayosababishwa na utumiaji wa maziwa

Matangazo 
 

 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org  

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita