|
AN-NUUR
|
| Sheikh Mzonge
awataka Waislamu Moshi wasimamishe swala
Na Ashraf Yussuf, Moshi IMAM wa Msikiti wa Alharamain mjini Moshi, Sheikh Ramadhani Mzonge amesema Waislamu wanapaswa kuipa sala nafasi yake katika Uislamu kinyume na hivi sasa, ili kuimairisha imani zao. Sheikh Mzonge aliyasema hayo katika khutba ya sala ya Ijumaa ya Agosti 21, mwaka huu katika Msikiti wa Alharamain Moshi Majengo. Akizungumzia maana ya sala, Sheikh Mzonge alisema, "Sala ni mazungumzo au mawasiliano baina ya mja na Mola wake, hivyo mja hana budi kunyenyekea kikamilifu awapo katika sala bila kufanya mzaha". Akinukuu baadhi ya aya na hadithi alisema sala ndio nguzo (muhimu) ya pili ya Muislamu baada ya kutoa shahada mbili, na atakayesimamisha sala atakuwa amesimamisha dini na atakae acha atakuwa kaivunja dini. Sheikh Mzonge aliendelea kusema kitu cha kwanza atakachoulizwa Muislamu siku ya Kiama ni sala na iwapo itatimia basi na mambo yake yatakuwa mazuri na iwapo haitatimia, basi nguzo nyingine zote zitachunguzwa. Akisikilizwa na mamia ya waumini, Sheikh Mzonge alisema Waislamu wanapaswa wasali sala kwa wakati wake maalum uliowekwa. Vile vile alisema Mtume (saw) alifaradhishiwa sala katika safari yake tukufu ya mbinguni hivyo alitoa aya kwa kusema "Ole wao wanaosali wasiojali muda wa sala unaotakiwa". Sheikh Mzonge alimalizia kwa kusema, "Sala humuongoza mja au Muislamu katika kheri na mambo mema, hivyo ni muhimu itiliwe mkazo na kupewa umuhimu mkubwa kwani Mwenyezi Mungu anatutahadharisha juu ya kuacha sala kwa kutufahamisha hatima ya wanaopuuza sala kwa kusema: "Ni kipi kilichokupelekeni motoni? Waseme: Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali". "Katika aya nyingine Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika amekwisha faulu aliyejitakasa akakumbuka jina la Mola wake na akasali", alisema Sheikh Mzonge. "Hivyo sala imewekwa kuizunguka siku nzima ili Muislamu akumbuke lengo halisi la kuumbwa na Mola wake na uhai wake ili shughuli anazozifanya zisipelekee aghafilike na lengo hili kuu", alimazilia Sheikh Mzonge. |
YALIYOMO
TAHARIRI Iran ina agenda gani? Mauaji,udhalilishaji Mwembechai: Wanawake
Waislamu waandamana Tabora Na Mwandishi Wetu 'Serikali ieleze hatua iliyochukua
kuhusu mauaji Mwembechai' ‘Musiwasingizie wake zenu maovu’
Barua za wasomaji
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org