AN-NUUR
Na.153 Safar 1419, Juni 12-18, 1998
 
Home 

Links 

Islam Tanzania 

Matoleo ya nyuma 
 
 

Mashairi

Salam kwa John Mtaki

Nimeishika kalamu, kwa uwezo wa Rabuka 
Naandika ya muhimu, Mola asiye na shaka 
Apendalo litatimu, pweke hana mshirika 
Hizi zangu salam, zifike kwa muhisika. 

Ewe John Mtaki, jina ulilojitwika 
Kukujibu ninahaki, yale uliyoandika 
Na hayo hatuhusiki, bali umetupachika 
Nakukumbusha ya haki, dini imetakasika 

Waislam rijali, soma yake histori 
Toka enzi za awali, watu hawa ni hatari 
Si dini ya madogoli, usitutie dosari 
Uislam kwa panga, dhamiri ika dhihiri. 

John ninakukosowa, nisikilize makini 
Leo nikuweke sawa, watu hao wabaini 
Wale waingiao mkusanyiko ibadani. 

Niwake kwa wanaume, hawala hawatengani 
Mambo hayo uyapime, hiyo ni ishara gani 
Kwa udani yatazamwe, yana usalama gani 
Magita na matarumbeta, wapigao kina nani. 

Nguo fupi mipasuko, mwaingia Kanisani 
Kwa mitindo ya kileo, kama mwenda dansini 
Ndio yake matokeo, yatendayo ibadani 
Ajabu ya jicho, laona halijioni. 

Hapa mwisho nasimama, mwisho wa utunzi wangu 
Imenibidi kusema, ingawa si nia yangu 
Naona mwatuandama, kwenye hii dini yangu. 

B. Batuli A. Mohamed Al-Amary,S.L.P. 4,Pangani - Tanga.  
 

Katiba mmekiuka 

1. Vifo Kimara Baruti, watu nane mwajutia 
Mwembechai mauti, dola mmeshangilia 
Eti mmewadhibiti, imani kali sawia 
Katiba mmekiuka, kuzuia mihadhara. 

2. Kuzuia mihadhara, Katiba mmekiuka 
Ni nani mwenye khasara, mmevuna mifaraka 
Tuliwapigia kura, kaitiba kkuwa mipaka 
Katiba mmekiuka, kuzia mihadhara. 

3. Yalotufika Muheza, vifo vya watu mtoni 
Sabini na sita kwanza, kutoweka duniani 
Jambo hili mlianza, Mwembechai wahuni 
KLatiba mmekiuka, kuzuia mihadhara. 

4. Gari moshi la Mpanda, Tabora lilipinduka 
Basi huku likienda, Iringa likaanguka 
Hayo nani iametenda, bado hamjazinduka 
Kaitiba mmekiuka, kuzuia mihadhara. 

5. Mvua ziliponyesha, mlidhania baraka 
Daraja ikazirusha, mwisho iikaja gharika 
Watu wanyama wakesha, mito iilipofurika 
Kaitiba mmekiuka, kuzuia mihadhara. 

6. Ela haikuwa mvua, ila jeshi la Rabuka 
Sasa inakuja njaa, janga hili kutufika 
Kama hamajarejea, bure mnahangaika 
Katiba mmekiuka, kuzuia mihadhara. 

7. Senene qwele sawia, shambani wameanguka 
Kipi mwakitegemea, miiko mmekiuka 
Nini walichokosea, Islam Tanganyika 
Katiba mmekiuka, kuzuia mihadhara. 

8. Ilani twakuhusia, Benjamini Wamkapa 
Musa alipopitia, Firauni kenda kapa 
Kura tulokupatia, tunajutia kkukupa 
Kaitiba mmekiuka, kuzuia mihadhara. 

Shaboki S.R.Babati  
 
 

 
 

YALIYOMO

TAHARIRI  

Uvamizi wa Polisi Mwembe Chai:  Mwanafunzi aliyepigwa risasi apooza Muhimbili   

Maoni yetu: Vipi watu wafurahie mateso ya wengine?  

Wanawake wakutana na kudai:  Gewe, Makamba wajiuzulu    
  
Maelezo ya Mjumbe wa Kisarawe katika mkutano wa kina mama   

Waraka wa Baraza Kuu kwa Mh. Rais   

BARUA ZA WASOMAJI  

Mmiliki wa Biblia na mbinu za kuhubiri   

MAONI YA WASHAIRI  

MAKALA:   
KAMATI YA KINA MAMA WA KIISLAMU - TAARIFA YA MATUKIO JUU YA UNYANYASAJI WA POLISI DHIDI YA WANAWAME WA KIISLAMU   

MAKALA MAALUM   
Waziri Dossa Azizi: Shujaa aliyesahaulika - Na. Mohammed Said  

Mdahalo juu ya kudhulumiwa Waislamu: Tuache hisia na kejeli, tutoe hoja  

TAMKO LA WANAWAKE WA KIISLAMU DHIDI YA MAUAJI YA WAISLAMU MWEMBECHAI NA KUDHALILISHWA WANAWAKE WAISLAMU MAHABUSU   

Hali ilivyokuwa kwenye shule za Misheni   

Makala: Baada ya miaka 34 Zanzibar yakosa Majaji - na S. Mzee   

Bakwata ithamini juhudi za wengine  

Masheih Arusha wamuunga mkono K.K.   
Na Mwandishi Wetu Arusha  

Makamba aliongezea  AN-NUUR 'Mashitaka'  

MSAUD wafikisha suala la Chuki AMNESTY  
  
Wazee Handeni wakwamisha mhadhara 

 
 Maoni yoyote kuhusu ukarasa huu yapelekwe kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
An-nuur Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita