AN-NUUR
Na.153 Safar 1419, Juni 12-18, 1998
 
Home 

Links 

Islam Tanzania 

Matoleo ya nyuma 
 
 

TAMKO LA WANAWAKE WA KIISLAMU DHIDI YA MAUAJI YA WAISLAMU MWEMBECHAI NA KUDHALILISHWA WANAWAKE WAISLAMU MAHABUSU

Sisi Wanawake wa Kiislamu, tumesikitishwa na kufadhaishwa sana na hatua ya jeshi la polisi kuingia msikitini kuwapiga, kuwadhalilisha na kisha kuwaweka rumande akina mama wa msikiti wa Mwembechai mnamo tarehe 12/02/1998. Pia, tumestushwa na kuhuzunishwa na hatua ya polisi kutumia risasi za moto ambazo zilisababisha vifo vya Waislamu wanne na wengine kadhaa kujeruhiwa akiwemo mwanafunzi Chuki Athuman ambaye yuko Hospitali ya Muhimbili hadi sasa na huenda asirejee tena katika hali yake ya kawaida.

Halikadhalika, tumesikitishwa sana na jinsi Serikali ilivyolichukulia suala hilo, hivyo;. Kwanza, kwa pamoja, tunalaani udhalilishaji na mauaji yaliyofanywa na polisi.. Pili, tunaitaka Serikali iache propaganda na ubabaishaji kuhusiana na suala hili, bali;

(a) Iunde tume huru kuchunguza kadhia nzima hii.

(b) Iwachukulie hatua za kisheria wote waliohusika na mauaji ambao baadhi yao walionekana hadharani wakifanya unyama huo, na

(c) Iwaombe radhi kina mama wa Kiislamu waliodhalilishwa na chombo chake cha "Usalama".Tatu, tumesikitishwa na kimya kilichoonyeshwa na jumuiya zinazoitwa za kutetea haki za binaadamu hususan Wanawake, hivyo;

(a) Sisi wanawake wa Kiislamu tumeingiwa na wasiwasi mkubwa iwapo jumuiya hizo ziko kwa lengo hilo.

(b) Hatudhani kuwa vyombo hivi vinawaona Waislamu kuwa ni wanaadamu wenye kustahiki haki za msingi za kila mwanaadamu.Nne, kwa kuwa vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kutengeneza au kuharibu haiba na murua wa jamii na kwamba vinawajibu kuripoti tukio kwa usahihi na kama lilivyotokea (objectively), tunasikitishwa na baadhi ya vyombo vya habari namna vinavyoripoti matukio ya yanayowahusu Waislamu na hasa suala hili la Mwembechai, hivyo;

(a) tunaviomba viripoti habari kwa usahihi na vichukue muelekeo wa kati na kati (Impartiality).

(b) Vilevile tunawasihi waandishi na wahariri wajiepushe na chuki na wazingatie maadili (ethics) ya taaluma yao hasa katika kipengele cha "Balance and fairness".Tano, kwa kuwa uhuru wa kuabudu na suala la dhamana ni haki za kikatiba za kila raia na kwa kuwa sera ya nchi katika utendaji wa vyombo vyake ni ile ya kutokuwa na dini (secular), hivyo tunaitaka Serikali;

(a) Idhibiti watendaji wake wenye muelekeo wa udini katika utekelezaji wao wa majukumu.

(b) Ifute kesi ya kashfa iwapo dai lenyewe ni kule kusema Yesu sio Mungu au Mwana wa Mungu na kwamba hakusulubiwa wala hakufa Msalabani, na 

(c) Watuhumiwa wote wa kesi ya Mwembechai wapewe dhamana. 

Wabillah Tawfiiq,Wanawake wa Kiislamu. 

 
 

YALIYOMO

TAHARIRI  

Uvamizi wa Polisi Mwembe Chai:  Mwanafunzi aliyepigwa risasi apooza Muhimbili   

Maoni yetu: Vipi watu wafurahie mateso ya wengine?  

Wanawake wakutana na kudai:  Gewe, Makamba wajiuzulu    
  
Maelezo ya Mjumbe wa Kisarawe katika mkutano wa kina mama   

Waraka wa Baraza Kuu kwa Mh. Rais   

BARUA ZA WASOMAJI  

Mmiliki wa Biblia na mbinu za kuhubiri   

MAONI YA WASHAIRI  

MAKALA:   
KAMATI YA KINA MAMA WA KIISLAMU - TAARIFA YA MATUKIO JUU YA UNYANYASAJI WA POLISI DHIDI YA WANAWAME WA KIISLAMU   

MAKALA MAALUM   
Waziri Dossa Azizi: Shujaa aliyesahaulika - Na. Mohammed Said  

Mdahalo juu ya kudhulumiwa Waislamu: Tuache hisia na kejeli, tutoe hoja  

TAMKO LA WANAWAKE WA KIISLAMU DHIDI YA MAUAJI YA WAISLAMU MWEMBECHAI NA KUDHALILISHWA WANAWAKE WAISLAMU MAHABUSU   

Hali ilivyokuwa kwenye shule za Misheni   

Makala: Baada ya miaka 34 Zanzibar yakosa Majaji - na S. Mzee   

Bakwata ithamini juhudi za wengine  

Masheih Arusha wamuunga mkono K.K.   
Na Mwandishi Wetu Arusha  

Makamba aliongezea  AN-NUUR 'Mashitaka'  

MSAUD wafikisha suala la Chuki AMNESTY  
  
Wazee Handeni wakwamisha mhadhara 

 
 Maoni yoyote kuhusu ukarasa huu yapelekwe kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
An-nuur Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita