AN-NUUR
Na.153 Safar 1419, Juni 12-18, 1998
 
Home 

Links 

Islam Tanzania 

Matoleo ya nyuma 
 
 

Maelezo ya Mjumbe wa Kisarawe katika mkutano wa kina mama

Mimi natoka Kisarawe lakini nimepata uchungu baada ya kusikia hapa Dar es Salaam, tunanyanyasika wanawake, mpaka kufika kupigwa na kuvuliwa nguo na kuadhiriwa hadharani. 

Kinachonitia uchungu sana ndugu zangu wanawake wa Kiislamu, Uhuru (umeletwa) na Babu zangu. Mpaka uhuru unapatikana. Babu zetu walipata taabu kuchangishwa sumni sumni ili uhuru upatikane. Lau kama babu zangu wapo mbele ya haki, siwataji kwa majina kwasababu Yaa Rabbi; Bwana Julius Nyerere Kambarage kusikia haya majina atasikitika sana. Kutunyanyasa sisi Waislamu waliokwenda kuomba uhuru na kumpa yeye madaraka.(Leo tunanyanyaswa sisi) hasa Waislamu wa Kisarawe, Msanga, Visiga, Mwanarumango.Wazazi wetu walipata taabu sana nikifikiria natamani kulia. Tumesoma sisi kwa taabu sana.Yaa Rabbil-Alamina Mwenyezi Mungu leo tumeletewa madhara, mtu huyo kwa babu zetu taabu waliyopata kuleta uhuru. Uhuru wamepata Wakristo sie Waislamu hatuna.

Wanawake wamevulia nguo, Ya Rabbi Mungu; kitu kinaniuma sana hasa mimi Mwislamu kutoka Kisarawe.

Najisikia uchungu sana. Mimi najua mwanzo mpaka mwisho (Tulivyopata uhuru).Kitu kinaniuma sana leo mmetugeukia; mmetugeukia wewe (Mhe. Mwalimu Nyerere). Sisi hatusemi wengine.

Ninachosema mimi Yaa Rabbil Alamina Mwenyezi Mungu atupe salama na amani Uislamu wetu uwe juu. Lakini unyonge wetu (kudhalilishwa kwetu) tutalipwa na Allah Subhana Wataala. 

Yaani sisi tumeomba uhuru wa kuja kuteseka. 

Mimi nataka nielewe, kama wapo hapa wanasikia wende wakaniulizie suala hili. Uhuru huu wa wanawake wa Kikristo au wa wanawake wa KiislamuMababu zetu walipata taabu sana kuomba uhuru huu. Wengine walisoma misahafu (Qur'an) kwa ajili ya uhuru huu. Leo uhuru umekuwa taabu (balaa) kwetu sisi wanawake wa Kiislamu ndio hatusemi. Imekuwa sisi tunavuliwa nguo hadharani. 

Serikali gani ya kuwavua nguo wanawake wa Kiislamu. Wavuliwa nguo na wanaume wasio kuwa waume zao. 

Jamani Yaa Rabbil Alamina. Jamani Yaa Rabbil Alamina muogopeni Subhana wa Taala.Au kumbukeni mlipata wapi uhuru huu. Kumbukeni nani alikusaidieni (alileta) uhuru huu!(Walileta) Waislamu hasa wanawake wa Kiislamu mama zetu walikuwa wanakwenda; Bwana Julius Kambarage unarudi (UNO) wamekuimbia "Sasa hata kabwela UNO". Sasa UNO imekuwa taabu kwetu sisi.

Kumbe "hata kabwela UNO" itakuwa hata kabwela UNO yenu nyinyi Wakristo sio sie Waislamu.Assalaam alaikum warahmatullah Waabarakatuh. Nasikia uchungu sana.. 

 
 

YALIYOMO

TAHARIRI  

Uvamizi wa Polisi Mwembe Chai:  Mwanafunzi aliyepigwa risasi apooza Muhimbili   

Maoni yetu: Vipi watu wafurahie mateso ya wengine?  

Wanawake wakutana na kudai:  Gewe, Makamba wajiuzulu    
  
Maelezo ya Mjumbe wa Kisarawe katika mkutano wa kina mama   

Waraka wa Baraza Kuu kwa Mh. Rais   

BARUA ZA WASOMAJI  

Mmiliki wa Biblia na mbinu za kuhubiri   

MAONI YA WASHAIRI  

MAKALA:   
KAMATI YA KINA MAMA WA KIISLAMU - TAARIFA YA MATUKIO JUU YA UNYANYASAJI WA POLISI DHIDI YA WANAWAME WA KIISLAMU   

MAKALA MAALUM   
Waziri Dossa Azizi: Shujaa aliyesahaulika - Na. Mohammed Said  

Mdahalo juu ya kudhulumiwa Waislamu: Tuache hisia na kejeli, tutoe hoja  

TAMKO LA WANAWAKE WA KIISLAMU DHIDI YA MAUAJI YA WAISLAMU MWEMBECHAI NA KUDHALILISHWA WANAWAKE WAISLAMU MAHABUSU   

Hali ilivyokuwa kwenye shule za Misheni   

Makala: Baada ya miaka 34 Zanzibar yakosa Majaji - na S. Mzee   

Bakwata ithamini juhudi za wengine  

Masheih Arusha wamuunga mkono K.K.   
Na Mwandishi Wetu Arusha  

Makamba aliongezea  AN-NUUR 'Mashitaka'  

MSAUD wafikisha suala la Chuki AMNESTY  
  
Wazee Handeni wakwamisha mhadhara 

 
 
Maoni yoyote kuhusu ukarasa huu yapelekwe kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
An-nuur Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita