|
|
| Home |
Masheih Arusha wamuunga mkono K.K.Na Mwandishi Wetu ArushaMASHEIKH kadhaa mkoani Arusha na Kilimanjaro, wameungana na Mbunge wa Kigamboni Mhe. Kitwana Kondo kuiambia Serikali iwape dhamana Waislamu waliopo ndani na kuwafutia mashitaka wale ambao wameshitakiwa kinyume cha katiba na sheria za nchi.Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Sheikh Mohamed Hemed Anzuwani alisema anaungana na Mhe. Kitwana Kondo kuisihi Serikali ama iwaachilie kabisa watuhumiwa wa Mwembechai au iwape dhamana.Alisema ni jukumu la kila Muislamu kuamrisha mema na kukataza mabaya; na hivyo Mhe. Kondo katekeleza wajibu wake kulisemea jambo baya analoona linafanywa na Serikali. Sheikh Anzuwani alisema kama \wakristo wenyewe wanasema hawakukashifiwa; vipi tena Muislamu leo ashitakiwe kwa kosa la kashfa.Naye Sheikh Hashim Juma alitahadharisha kwamba isingekuwa jambo la busara Waislamu kuwekwa katika mazingira ya kujiandaa kuwasomea khitma walioko mikononi mwa Serikali.Sheikh Hashim alionyesha masikitiko yake kutokana na kauli za baadhi ya mabaraza ya dini kwamba hayajaweza kuwasaidia Waislamu kwasababu hayajaombwa. Alitoa wito mafunzo na ujumbe unaopatikana katika Surat Abzab Aya ya 21 mpaka 36 uzingatiwe kwa makini. Naye Sheikh Farijala Hussein akilizungumzia suala hili alisema kwamba imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi kutokana na Serikali kufumbia macho na kujifanya bubu kuhusu suala zima la kuvunjwa kwa haki za binadamu na hasa Waislamu.Sheikh Farijala alisema hivi sasa Waislamu wanakamatwa ovyo, kuwekwa ndani, kupigwa na wengine kuuliwa bila ya haki wala sheria. Katika hali hiyo anasema haungani tu na Mhe. Kitwana Kondo lakini kwa kila mpenda haki na amani. Alisema hakuna amani inayopatikana kwa mabavu wala vitisho, bali kwa kuwapa watu uhuru na haki zao.Sheikh Yusuf Ismail Kimaro ambaye ni Imam wa Msikiti wa Bondeni Wilayani Hai; akiungana na Masheikh wenzake alisema aliyozungumza Mhe. Kitwana Kondo ndiyo yanayotegemewa kwa mtu yeyote mkweli na muadilifu. Kwa ajili hiyo amewataka Waislamu wote kumuunga mkono.Hivi karibuni Mbunge wa Kigamboni Mhe. Kitwana Kondo aliongea na waandishi wa habari ambapo aliishauri Serikali iwape dhamana watuhumiwa wa kesi ya Mwembechai walioko ndani, pamoja na kuiomba iondoe shitaka la kashfa kwa aliyesema Yesu si Mungu. Aidha, Mhe. Kondo katika mkutano huo aliilaumu Serikali kwa kutojali masuala ya Waislamu kiasi cha kuwaruhusu Polisi kuvunja Msikiti na kuingia ndani na viatu. |
Uvamizi wa Polisi Mwembe Chai: Mwanafunzi aliyepigwa risasi apooza Muhimbili Maoni yetu: Vipi watu wafurahie mateso ya wengine? Wanawake wakutana na kudai:
Gewe, Makamba wajiuzulu
Waraka wa Baraza Kuu kwa Mh. Rais Mmiliki wa Biblia na mbinu za kuhubiri MAKALA:
MAKALA MAALUM
Mdahalo juu ya kudhulumiwa Waislamu: Tuache hisia na kejeli, tutoe hoja Hali ilivyokuwa kwenye shule za Misheni Makala: Baada ya miaka 34 Zanzibar yakosa Majaji - na S. Mzee Bakwata ithamini juhudi za wengine Masheih Arusha wamuunga mkono
K.K.
Makamba aliongezea AN-NUUR 'Mashitaka' MSAUD wafikisha suala la Chuki
AMNESTY
|
| An-nuur Home | Links | Islam Tanzania | Matoleo yaliyopita |