|
|
| Home |
BARUAMasheikh wa Tunduru tuwaeleweje?Ndugu Mhariri,ALLAH (s.w.t.) ametuambia ndani ya Qur'an kuwa lipatikane kundi miongoni mwenu kulinganiawatu (dini) (Qur 3.107). Aya hii ndio iliowafanya Waislamu wakae chini na kuunda chombo ambacho kitakuwa na kazi hiyo (Al-MALLID) na kilianza kazi hiyo.Hapa Tunduru tangu lilipofunguliwa tawi la Al-MALLID ni takriban miaka miwili na kitu sasa, na vijana wa AL_MALIID walianza kulingania watu hapa mjini na vijijni, kwa kujitolea mali yao na nafsi zao. Mpaka sasa kazi hiyo imepata mafanikio mazuri kama ifuatavyo:- Al-mallid inaendesha madrasa 19 wilayani Tunduru na madrasa hizo zina wanafunzi zaidi ya elfu mbili wanaojifunza.Imefanikiwa kuwaingiza watu 72 kutoka katika dini nyingine na kuingia katika Usilamu.Idadi kubwa yawatu wanahudhuria misikitini kutokana ulinganiaji (daawa) unaofanywa na vijana hao wa AL-MALLID. Lakini jambo la kushangaza na la kusikitisha sana ni kwamba Sheikh Mkuu wa BAKWATA wa Wilaya anapita vijijini na kuwaeleza waumini kwamba vijana hao wa AL-MALLID mkiwaona wakamateni na kuwafungia ghalani kwa madai kwamba, wanakashifu, wanahatarisha amani,hawana hekima, hawana elimu n.k. Wakati taasisi hiyo BAKWATA haijishughulishi na chochote juu ya Waislamu wa Wilaya hii, si kwa kuwalingania watu dini au hata kuendesha madrasa jambo ambalo tulitazamia lingetekelezwa na BAKWATA kama taasisi ya dini. Na matokeo yake ni malumbano katika kugombea madraka kati ya Sheikh mkuu wa BAKWATA NA KATIBU WAKE. Na kama ilivyokawaida yao BAKWATA toka ngazi ya taifa hadi ngazi za wilaya huwa wanaamini kuwa Uislamu ni kurukuu na kusujudu tu, na ukishafanya hivyo unayo tiketi ya kuingia peponi na wamesahau kabisa kuwa Uislamu ni mfumo wa maisha ya mwandamu. Hii inatokana na ukweli kuwa Waislamu wenzetu wa Mwembechai walipouawa na polisi tulitoa maoni kwamba kama tumeshindwa kutoa michango ya rambirambi kwa ndugu wa waliouawa na familia za wale waliowekwa ndani (rumande), basi tuwaombee dua kama tunavyowaombea marehemu wengine, lakini hilo kwa Masheikh wetu likawa ni gumu, eti wanaogopa Serikali yasije yakawakuta yaliyowakuta waumini wa Mwembechai. Bali kwa kuwaombea dua watu ambao walikuwa hawaswali hilo kwao ni sawa na litaendelea kudumishwa. Hivyo mnafikiri matatizo ya Mwembechai ni yao peke yao? Tafadhalini Masheikh rudini kwa Mola wenu. Wakereketwa wa dini,TUNDURU.
CCM isiombe kura za WaislamuNdugu MhaririSERIKALI ya CCM imepeleka askari wakiwa na viatu ndani ya Msikiti wa Morogoro na Mwembechai, na inajisifia kuwa ilikuwa lazima ifanye vile kwa kupambana na wahalifu.Je, jeshi la polisi, makachero na helikopta ziliwezaje kuulinda Msikiti wa Mwembechai na maeneo yanayouzunguka kwa karibu mwezi mzima, lakini ikashindwa kusubiri angalao kwa usiku mmoja kungoja waumini walioko Msikitini hapo watoke wenyewe. Lakini kwa dharau, serikali ikaamrisha askari wavunje milango na kuingia ndani ya Msikiti wakiwa wamevaa viatu. Dharau hii, Waislamu hatutaisahau, na ni dhambi kubwa sana kama mtakuja kutuomba kura katika chaguzi zozote za CCM. A. Mbaga,Dar es Salaam.
Waislamu mlio TAMWA jiondoeni ili mpate radhi ya Mola wenuNdugu MhaririHII ni kwa sababu nilivyochunguza chama hiki kina agenda ya siri ya kupinga mafundisho ya Qur'an na Sunnah.Kwa mfano wa karibu ni kwamba chama hiki kimeweza kutetea Changudoa aliyehukumiwa kifungo ilihali kinajua Changudoa huyo kazi yake ni zinaa na wizi.Wanawake Waislamu wameteswa na kudhalilishwa wamekaa kimya. Ally Marijani,Dar es Salaam.
Hakuna amani TanzaniaNdugu MhaririNAPENDA kujitokeza katika gazeti lako kupinga habari zinazovuma sana katika vyombo vya habari kwamba Tanzania ina amani.Mimi siafiki. Wanatuambia tuna amani, amani ipi ikiwa vyombo vya amani vinavurugwa? Hayo yote yanafanyika hali ya kuwa wao hawajui. Mambo mazito kama vile bomoa bomoa zisizo na mpango, kupunguza wafanyakazi, Wamachinga kufukuzwa ovyo, matibabu hakuna, maji hakuna, barabara hakuna (kusini), pesa hakuna eti yanalipwa madeni! Polisi kuua watu ovyo, polisi kuwakandamiza watu kwa kuwaomba rushwa, wafungwa kunyimwa dhamana na kuteswa. Hayo yote yanapoteza amani kwa hiyo kwa vile yanafanyika, tunasema amani hakuna.Ikiwa leo wanashikiliwa watu bila makosa, pia kuteswa kabla ya hukumu hiyo ndiyo amani. Tunapenda kuiambia serikali yetu kwamba inatupa taabu hata sisi raia tusio na uwezo, kwa sababu sisi tunaokaa katika nyumba za Kiislamu tunafukuzwa kwa sababu Waislamu wana uchungu na ndugu zao Waislamu ambao hawapewi dhamana na wanaonewa. Tunaomba serikali iwafikirie Waislamu. Rose Lukasi,Iringa.
Wanafunzi tukusanyike kupinga mwenzetu Chuki kupigwa risasi Ndugu MhaririTENDO lililofanywa na polisi wa serikali ya awamu ya tatu kumfyatulia risasi na kumjeruhi mwanafunzi mwenzetu Chuki Athumani bila kosa ni la uonevu na ukiukwaji wa haki za binadamu. Kwa vile aliyejeruhiwa hivyo ni Muislamu, serikali haikutoa tamko lolote kwa aliyejeruhiwa wala pole kwa ndugu na wanafunzi wenzake, kama hiyo haitoshi wanafunzi tunazuiwa kwenda kukmuona mwenzetu hospitalini. Wanafunzi takae tukijua kwamba Chuki Athumani anawakilisha wanafunzi
wa Kiislamu hapa Tanzania walioko Serikondari na vyuo, hivyo yaliyomkuta
Chuki yaweza kukukuta wewe au mimi.
Chilyunga M.H.Al-Haramain,Dar es Salaam.
Matamshi ya Mh. K.K. (MB) kuhusu Waislamu walionyimwa dhamanaNdugu MhaririNamuunga mkono Mh. K.K. kwa malalamiko yake kuhusu serikali kuwanyima ndugu zetu waliorundikwa ndani ya mahabusu kwa kile wanachodaiwa kufanya vurugu Mwembechai. Tukitizama kesi yenyewe sio nzito ya kuwanyima dhamana. Kesi yenyewe ni ya vurugu za Mwembechai.Lakini kwa kuwa serikali hii inawachukia Waislamu na Uislamu, imeona hii ndio njia pekee iliyopatikana ya kukandamiza Uislamu na Waislamu wenyewe. Tangu serikali ilipoanzisha Bakwata kinyume na matakwa ya Waislamu na kufuta (EAMWS) bila ya kutoa sababu ilikuwa na lengo moja tu kuzima speed (kasi) za Uislamu uliokuwa wakati huo unaenea hadi ndani ya vitongoji nchini kote. Licha ya jitihada hiyo ya serikali kuzima speed (kasi) hiyo ya kuenea kwa Uislamu, siku hizi chombo cha serikali yaani Bakwata pamoja na Masheikh wake wanashangaa kusikia kwamba wachunga ng'ombe wote wanaingia dini hii ya Mwenyezi Mungu kwa kasi sana. Bakwata inaelewa kwamba Waislamu kote nchini hawaitaki pamoja na viongozi wake. Bakwata imo njiani kufa kifo baridi, dalili zake ni hizi; majengo yake mengi mikoani yamekuwa magofu, kama vile Mkoa wa Iringa, madarasa hakuna, magari yamekufa, mengine yameuzwa, sekondari ya Kiislamu Bakwata imekabidhi Kanisa baada ya kushindwa kuiendesha. Naomba Waislamu wote tumuunge mkono Mh. K.K. aendelee mbele kuutetea Uislamu. Sheikh Msabi Abdallah bin Mrimi,S.L.P. 462,Tarime,Mara.
Bakwata kummaliza Kitwana Kondo!Ndugu MhaririNinapenda nitoe dukuduku langu juu ya majibu yaliyotolewa na Bakwata kwa Mh. Kitwana Kondo na Waislamu wenye msimamo kama wake, kwamba ni mchochezi na anatafuta umaarufu.Kutangaza kwamba KK ni mchochezi, unaweza ukatoa ushahidi ni vipi alichochea au anachochea mambo katika jamii yetu, au kwa sababu tu, amesema kuwa Waislamu wapewe haki yao ambayo iko wazi katika Katiba yetu ya nchi. Kuutafuta umaarufu sio kweli anatafuta umaarufu katika nchi hii au nje ya nchi, kwa sababu ukitoa nafasi nyingine alizofanyia kazi katika serikali zote zilizopita ya awamu ya kwanza, ya pili na sasa ya tatu kuanzia udiwani, umeya na sasa ubunge, vyote vinamfanya awe maarufu kuanzia shina mpaka taifa. Hakuna asiyemfahamu sasa basi kama chombo cha Waislamu kama Bakwata kutangaza kuwa kimemmaliza Muislamu asiwatetee Waislamu wenzake walio jela hamuoni kuwa mnajimaliza wenyewe? Kuwadhibiti Waislamu sio suluhu ya matatizo yaliyopo ila muache mambo ya kidunia na mfuate haki ndipo amani itakapokua ya uhakika katika nchi yetu na dunia nzima. Mpenda Haki,Abdallah Salehe,Dar es Salaam.
Waislamu tumo hasaraniNdugu MhaririNAOMBA nafasi katika gazeti lako ili niweze kutoa zangu nasaha kwa Waislamu wote wa Tanzania.Kutokana na hali halisi ya mgandamizo mkubwa ambao tunaupata sisi Waislamu wa Tanzania kutoka katika serikali ambayo ni ya CCM mimi binafsi nisingependa ifikapo Oktoba, 2000 likafanywa kosa ambalo limefanywa mwaka 1995. Iwapo kosa lile tutalirudia tena, basi tuelewe wazi wote Waislamu wa Tanzania tumo hasarani na itatulazimu tutafute majibu ya kwenda kumjibu Muumba wetu hapo kesho akhera. Hamis Muhammad Choga, Kilwa - Pande.
Serikali inapigania dini gani? Ndugu MhaririNATOA malalamiko yangu kupitia kwenye gazeti lako kuhusiana udhalimu mkubwa unaofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka kuzima Uislamu kwa vinywa vyao. Udhalimu na uadui unaingia pale ambapo baadhi ya Waislamu wamekamatwa wako rumande dhamana hawapewi. Kosa eti wamesema Yesu si Mungu. Tungependa kuona Maaskofu na Mapadri wakifungua kesi hiyo. Lakini mbona wenyewe kimya? Ni wazi kwamba hapa hapana kosa bali ni udhalimu tu wa serikali. Amejisemea K.K. akufukuzaye hakwambii toka. Fauziyat Ahmed Nammanje (Answar)Kigu Kipimi,Box 93,Newala - Mtwara.
|
Uvamizi wa Polisi Mwembe Chai: Mwanafunzi aliyepigwa risasi apooza Muhimbili Maoni yetu: Vipi watu wafurahie mateso ya wengine? Wanawake wakutana na kudai:
Gewe, Makamba wajiuzulu
Waraka wa Baraza Kuu kwa Mh. Rais Mmiliki wa Biblia na mbinu za kuhubiri MAKALA:
MAKALA MAALUM
Mdahalo juu ya kudhulumiwa Waislamu: Tuache hisia na kejeli, tutoe hoja Hali ilivyokuwa kwenye shule za Misheni Makala: Baada ya miaka 34 Zanzibar yakosa Majaji - na S. Mzee Bakwata ithamini juhudi za wengine Masheih Arusha wamuunga mkono
K.K.
Makamba aliongezea AN-NUUR 'Mashitaka' MSAUD wafikisha suala la Chuki
AMNESTY
|
| An-nuur Home | Links | Islam Tanzania | Matoleo yaliyopita |