|
|
| Home |
Makamba aliongezea AN-NUUR 'Mashitaka'Na Mwandishi WetuMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mheshimiwa Yusuf Rajab Makamba ametoa nyongeza ya madai yake dhidi ya gazeti la AN-NUUR. Katika nyongeza hiyo Mhe. Mkuu wa Mkoa Bw. Makamba amedai kwamba kitendo cha kumuita "Al-Ustaadh Sheikh Makamba" ni kumkejeli na kumdhalilisha.Katika barua yake No. MD/P.10/8/47 ya Juni 6, 1998 kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari, Mheshimiwa Makamba amesema; "Nalalamika kwamba mwandishi wa makala ameniita Al-Ustaadh na Sheikh kwa dhamira ya kunikejeli au kunidhalilisha". Akaongeza kusema "mimi (yeye Mhe. Makamba) sina makamu ya kuitgwa Ustaadh
au Sheikh; mimi ni muuamini wa dini ya Kiislamu na mwanafunzi", ilisema
sehemu ya barua yake.Kwa ajili hiyo Mhe. Yusuf Rajab Makamba anamtaka Mhariri
wa AN-NUUR athibitishe kuwa kwa kumuita Al-Ustaadh na Sheikh hakukusudia
kumnyanyasa.
Sheikh Mohammed Ummy afarikiNa Muhibu SaidMHADHIRI wa Jumuiya ya Wahubiri wa Kiislamu nchini (JUWAKITA), Sheikh Mohamed Athumani A. Ummy, amefariki dunia Jumamosi ya Mei 30, 1998, nyumbani kwa baba yake mdogo, Tandale Uzuri, jijini Dar es Salaam,baada ya kuugua muda mfupi.Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa familia yake, marehemu kabla ya kifo chake alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo na kibofu mbapo aliwahi kulazwa katika Hospitali ya Serikali yaMwananyamala kwa zaidi ya siku kumi na moja bila mafanikio.Aidha kwa mujibu wa msemaji huyo, baadae marehemu alihamishiwa katika hospitali ya T.M.J.iliyopo Kikocheni ambako hadi anafariki ndiko alikokuwa akitibiwa.Marehemu Sheikh Mohamed Ummy atakumbukwa sana na ndugu, jamaa, marafiki, majirani, Waislamu na Wasiokuwa Waislamu hususan wakazi wa mikoa ya Morogoro, Pwani, Dar es Salaam na kwingineko kwa mchango wake mkubwa wa kupigania ili kuuhuisha Uislamu bila woga. Marehemu Sheikh Mohamed Ummy ni miongoni mwa Waislamu waliounda Jumuiya ya kwanza za kuligania Uislamu ijulikanayo kwa kifupi kwa jina la "UWAMDI" mwanzoni mwa miaka ya 1980. Alianza rasmi harakati za kulingania Uislamu mnamo mwaka wa 1979 kwa kufanya mijadala ya Qur'ani Tukufu na tofauti zilizo baina ya Waislamu na Ahmadiyyah na madhehebu mengine ya Kikristo katika shuleya msingi ya Lumumba, Mnazi Mmoja na baadae Sokoni Kriakoo na mikoani alipoitwa kwenda kujibu hoja hizo. Mwaka 1982 alianza kufanya mijadala ya ulinganishi wa vitabu vinne (Torati, Zaburi, Injili na Qur'ani Tukufu) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Saaam na kufundisha elimu hiyo (ya Ulinganishi) katika shule ya Lumumba. Katika kuimarisha kazi hiyo, mnamo mwaka wa 1983, marehemu alishirikiana sambamba na Waislamu wengine waliounda Umoja wa Wahubiri wa Kiislamu wa Mlingano wa Didini (UWAMDI), akiwemo Almarhuman Sheikh Muhdin, Sheikh Khalifa Khamisi Sheikh Sadiki Watuta na wengineo.Katika harakati hizo, mwaka 1984 waliungana na Wahadhiri wengine, akiwemo Al-m arhum Sheikh Ngariba Musa Fundi, ustaadhi Kawemba Mohamed, Sheikh Abubakar
Mwilima na Sheikh Othmani Matata ili kuimarisha UWAMDI.
Wazee Handeni wakwamisha mhadharaNa Abu SaidWAZEE wa Kijiji cha Kwediboma katika Wilaya ya Handeni walikwamisha muhadhara ambao ulikuwa uendeshwe na ustaadh Hamim Ali Boza kuanzia tarehe 6 Juni mpaka tarehe 14 Juni.Kijiji hicho kilioko mwendo wa masaa manne na nusu kwa gari ya abiria, kutoka Handeni mjini, kilikuwa kiwe cha mwanzo kufaidika na kibali cha ruhusa cha mkuu wa Polisi wa Wilaya, chenye kumbukumbu No. HAN/A.25/Vol.V/247 cha tarehe 21 Mei. Tangu ujumbe ulipowasili saa tatu na nusu usiku wa tarehe 6, kulionekana ingia toka isiyo ya kawaida kwenye ofisi ya Katibu Tarafa wa Bakwata. Pirika hizo zilizowahusisha wazee na vijana hatimaye zilikoma baada ya sala ya Alasiri ya siku ya Jumapili. Akitoa ufafanuzi wa kuzuilika kwa muhadhara huo, katibu wa Bakwata Bwana Juma Bakari, alisema yeye kama kiongozi wa Bakwata hakuwa na kikwazo chochote kwa jambo la kheri kama hilo na hasa kwa vile alikwishapata taarifa kabla.Hata hivyo, aliendelea kusema kuwa asingeweza kwenda kinyume na uamuzi wa wazee walioweka pingamizi, ambao ni wajumbe wa kamati ya msikiti,ujumbe wa muhadhara ulipofikia. Ustaadh Hamim aliruhusiwa kutoa mawaidha mafupi ndaniya msikiti, katika
mawaidha hayo aliishukuru nyumba ya wageni ya Bwana Zuberi kwa kutoruhusu
matendo yoyote machafu kutendeka humo pia mkahawa mmoja ambao pia umezuia
ulevi kunywewe humo. Pia aliwahimiza Waislamu kujenga shule na kituo cha
afya.Sehemu nyingine ambazo zilikuwa zifaidike na mihadhara hiyo ni pamoja
na Kilindi, Mgera na Kisangasa.
MSAUD wafikisha suala la Chuki AMNESTYNa Mwandishi WetuWANAFUNZI Waislamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (MSAUD) wameiomba Taasisi za Kutetea Wafungwa (Amnesty International) kumsihi Mhe. Rais Benjamin William Mkapa kumhurumia mwanafunzi Chuki Athumani ambaye alipigwa risasi na Polisi Februari 13.Mwanafunzi huyo yupo hospitalini Muhimbili na anakosa matibabu kwa vile anahesabika kama mhalifu aliye mahabusu. Katika barua yao yenye kumb. Na. MSA/AM/005 wameeleza kwamba tayari walishamuandikia Mhe.Rais kuhusu suala hilo kwa hiyo sasa wanaomba `Amnesty International' iwasaidie juhudi hizo. Tayari zaidi ya robo tatu ya watu waliokuwa rumande wameshaachiwa na
kufutiwa mashitaka.Kwa mara ya mwisho waliachiwa watu 68. Hiyo ilikuwa
jana Alhamis, Juni 11, 1998.
|
Uvamizi wa Polisi Mwembe Chai: Mwanafunzi aliyepigwa risasi apooza Muhimbili Maoni yetu: Vipi watu wafurahie mateso ya wengine? Wanawake wakutana na kudai:
Gewe, Makamba wajiuzulu
Waraka wa Baraza Kuu kwa Mh. Rais Mmiliki wa Biblia na mbinu za kuhubiri MAKALA:
MAKALA MAALUM
Mdahalo juu ya kudhulumiwa Waislamu: Tuache hisia na kejeli, tutoe hoja Hali ilivyokuwa kwenye shule za Misheni Makala: Baada ya miaka 34 Zanzibar yakosa Majaji - na S. Mzee Bakwata ithamini juhudi za wengine Masheih Arusha wamuunga mkono
K.K.
Makamba aliongezea AN-NUUR 'Mashitaka' MSAUD wafikisha suala la Chuki
AMNESTY
|
| An-nuur Home | Links | Islam Tanzania | Matoleo yaliyopita |