AN-NUUR
Na.153 Safar 1419, Juni 12-18, 1998
 
Home 

Links 

Islam Tanzania 

Matoleo ya nyuma 
 
 

Makala

Baada ya miaka 34:

Zanzibar yakosa majaji

Na S. Mzee
Zanzibar ni miongozi mwa nchi chache barani Afrika ambazo zilipata tawala zake zilizopo sasa kwa njia ya Mapinduzi ya umwagaji damu. 

Kwa mujibu wa wanasheria Mapinduzi hayo ya Januari 1964 ambayo sasa yana miaka 34 yaligharimu maisha ya watu kadhaa, wengi wao wakiwa ni wale wenye asili ya kiarabu.

Mara baada ya Mapinduzi hayo wasomi kadhaa walianza kuikimbia Zanzibar na wimbi hilo liliongezeka mnamo miaka ya1967 na pia 72 mwaka ambao muasisi wa Mapinduzi hayo Abeid A. Karume aliuawa. Hakuna sababa hasa iliyotolewa hadi sasa juu ya ukimbiaji wa wanataaluma hao lakini kuna tetesi kwamba wengi wa waliokimbia, walikimbia kufuatia chuki za Karume dhidi ya wasomi. Inasemekana kwamba Karume aliwahi kutamka hadharani kwamba msomi umkimbie maili mia moja. Wasomi hao wengi walikimbilia katika nchi za ghuba na wachache wengine katika nchi za ulaya na marekani. 

Kwa mujibu wa wanahistoria mashuhuri duniani hadi kufikia mwaka 1965 Zanzibar mbali ya kuwa ni nchi ya pili kwa utajiri kaitika Afrika iikitanguliwa na Ghana tu, ilikuwa ikiongoza kwa idadi ya wasomi wa kila fani.Prof. Babu yeye anasema hadi muda huo Zanzibar hakukuwa na mtaalamu yoyote toke nje na shughuli zote zilikuwa zikifanywa na Wazanzibari wenyewe tena kwa ufanisi mkubwa. Babu anadai kwamba hadi mwaka huo Zanzibar ilikuwa na madaktari bingwa arobaini na tano (45) wakaiti jamii ya Wazanzibari iilikuwa haizidi watu laki tatu (300,000) wastani wa watu 6500 kwa kila daktari.Lengo kuu la Mapinduzi ya 1964 kwa mujibu wa Karume na wenzake ni kuyafanya maisha ya Mwafrika wa Zanzibar yawe bora kulinganisha na yalivyokuwa wakati wa utawala wa Waarabu. Leo baada ya miaka 34 lengo hilo inaonyesha limeshindwa kufikiwa. Zanzibar imekosa wataalamu wa kkila fani kuanzia madaktari, wahandisi, walimu na wengine kadhaa. Kuthibitisha hoja ya hapo juu Rais wa Zanzibar Dk. Salmin Amour hivi karibuni aliwaapisha majaji watatu na wanasheria wengine kadhaa kutoka Nigeria kufanya kazi zao Zanzibar.

Walioapishwa ni pamoja na Naibu jaji mkuu mmoja, majaji watatu wa mahakama kuu, wanasheria watatu wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar na washauri wake binafsi kuhusu mambo ya sheria watatu.Wachunguzi wa masuala ya siasa tayari wameanza kudai kwamba lengo la Dk.Salmin Amour ni kuteua majaji ambao ataweza kuwatumia atakavyo ukichukulia kwamba hivi sasa kuna kesi ya uhaini inayowahusisha viongozi kadhaa wa juu wa chama cha upinzani CUF. 

Wadadisi wanadai kwamba kama hiyo sio sababu ni kwa nini basi Dk. Salmin ateue wanasheria kutoka Nigeria ambao wataigharimu Serikali ya Zanzibar fedha nyingi zikiwemo za kigeni wakati tayari kuna tume ya siri iiliyounda kuchunguza ukubwa wa Serikali yake, tume ambayo inawasilisha ripoti yake hivi karibuni na kumtaka Dk. Salmin apunguze ukubwa wa Serikali yake. 

Katika kutetea uteuzi wa wanasheria hao kutoka Nigeria Waziri wa Nchi kaitika Ofisi ya Waziri Kiongozi (Sheria na Katiba) Bw. Iddi Pandu Hassan katika taarifa yake iliyotolewa na shirika la habari la BBC mnamo mei 27, 1998 alisema kwamba sababu kubwa ya Dk. Salmin kuteua wanasheria hao ni kutokana na majaji waliopo Zanzibar hivi sasa wanamaliza muda wao na hhakuna wanasheria wenye uzoefu wa kutosha kushika nafasi zao. Bw. Pandu alidai kwamba jaji Dahoma atastaafu Septemba 1998, jaji Wolfgang Dourado atastaafu wakati wowote toka sasa na jaji Kanyonyele atarejea kwao (Bara). Ni suala ambalo haliingii akilini kwamba Zanzibar ambayo ilifanya Mapinduzi 1964 kwa lengo la kuyafanya maisha ya Wazanzibari yawe bora imeshindwa kupata majaji baada ya miaka 34.

Hatuna haja ya kuliingia suala hili kwa undani, lakini inaelekea itafikia wakati tutakosa hata mtu mwenye sifa ya kuongoza nchi na hivyo tutalazimika kuagiza kiongozi huyo toka nchi za nje. Inaweza ikaonekana kwamba ni jambo la dhihaka lakini hii ndiyo hali halisi tunayoielekea. Kama tumeshindwa kupata wanasheria kwa kipindi chote hicho ni kwa nini iwe ajabu kukosa kiongozi wa juu wa kutuongoza. Pengine jambo ambalo linatia mashaka makubwa ni kweli Zanzibar hakuna wanasheria wenye uzoefu au waliopo wanakosa sifa nyengine za ziada ambazo hazikuainishwa. Tayari kuna tetesi kwamba wanasheria wengi waliopo Zanzibar hivi sasa ni wenye asili ya Pemba ambao wamekuwa wakiogopwa kupewa madaraka kwa hoja kwamba watawapendelea wanachama wa CUF, kaitika hukumu mbali mbali. 

Ni vipi mtu ambaye ana shahada ya pili ya sheria na ameshafanya kazi ya uhakimu kwa muda wa miaka zaidi ya kumi na tatu tuambiwe hajawa na uzoefu wa kuwa jaji. Katika hali hii sidhani kama itafika wakati tutakuwa na watu wenye uzoefu katika fani yoyote ile.

Ikiwa maelezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Iddi Pandu ni ya kweli basi kuna haja kubwa ya kuyaangalia Mapinduzi ya Januari 1964 na kuyafanyia tathmini ili tuweze kujua ni kwa kiasi gani yametunufaisha. 
 

 
 

YALIYOMO

TAHARIRI  

Uvamizi wa Polisi Mwembe Chai:  Mwanafunzi aliyepigwa risasi apooza Muhimbili   

Maoni yetu: Vipi watu wafurahie mateso ya wengine?  

Wanawake wakutana na kudai:  Gewe, Makamba wajiuzulu    
  
Maelezo ya Mjumbe wa Kisarawe katika mkutano wa kina mama   

Waraka wa Baraza Kuu kwa Mh. Rais   

BARUA ZA WASOMAJI  

Mmiliki wa Biblia na mbinu za kuhubiri   

MAONI YA WASHAIRI  

MAKALA:   
KAMATI YA KINA MAMA WA KIISLAMU - TAARIFA YA MATUKIO JUU YA UNYANYASAJI WA POLISI DHIDI YA WANAWAME WA KIISLAMU   

MAKALA MAALUM   
Waziri Dossa Azizi: Shujaa aliyesahaulika - Na. Mohammed Said  

Mdahalo juu ya kudhulumiwa Waislamu: Tuache hisia na kejeli, tutoe hoja  

TAMKO LA WANAWAKE WA KIISLAMU DHIDI YA MAUAJI YA WAISLAMU MWEMBECHAI NA KUDHALILISHWA WANAWAKE WAISLAMU MAHABUSU   

Hali ilivyokuwa kwenye shule za Misheni   

Makala: Baada ya miaka 34 Zanzibar yakosa Majaji - na S. Mzee   

Bakwata ithamini juhudi za wengine  

Masheih Arusha wamuunga mkono K.K.   
Na Mwandishi Wetu Arusha  

Makamba aliongezea  AN-NUUR 'Mashitaka'  

MSAUD wafikisha suala la Chuki AMNESTY  
  
Wazee Handeni wakwamisha mhadhara 

 
 Maoni yoyote kuhusu ukarasa huu yapelekwe kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
An-nuur Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita