|
Na. 065 Jumatano Septemba 13 - 19, 2000 |
|
|
|
|
|
Yanga watakiona - Kajumulo Na Mwandishi Wetu KLABU ya Kajumulo World Soccer ya Dar es Salaam imesema itafanya kila njia kuhakikisha inaifunga timu ya Yanga ya jijini katika michuano ya Kombe la Muungano katika medani ya soka. Michuano hiyo itakayozishirikisha timu sita, tatu kutoka kila upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu. Kajumulo kupitia kwa kocha wake mkuu, Jamhuri Kihwelo "Julio", imesema ina hakika ya kutimiza azma hiyo kutokana na ubora wa usajili uliofanywa na klabu yake. "Mimi nasema safari hii Yanga watakiona kilichomtoa kanga manyoya kwa sababu tutawafunga mechi zote mbili wakitaka wasitake. Na hii inatokana na ubora wa timu yangu, hasa ukizingatia kwamba tumeongeza wachezaji wengine watano ambao ni wakali", alidai "Julio" jana jijini. Kwa mujibu wa kanuni zinazotawala michuano hiyo timu shiriki zinaruhusiwa kuongeza wachezaji watano kila moja zikipenda. Wachezaji wapya ambao Jamhuri amesema atawatumia kuisambaratisha Yanga ni Edward Kayoza, kutoka Singida United, Mwanamtwa Kihwelo na Mliberia William Fahnbuller kutoka Simba ya Jijini. Kayoza ni miongoni mwa washambuliaji hatari nchini waliotia for a katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyomalizika hivi karibuni na kupelekea timu ya Mtibwa kutwaa ubingwa. Kina Kayoza wanatarajiwa kuungana na wachezaji kama Madaraka Seleman, Idd Kaoneka, Ali Shah, Salvatory Edward, Thomas Kipese na Kalimangonga "Kally" Ongara ambaye anatarajiwa kuwasili wiki ijayo akitokea nchini Uingereza. Pamoja na Kajumulo na Yanga timu zingine zitakazoshiriki ligi hiyo ni Mtibwa Sugar ya Morogoro, Mafunzo, Kipanga na Polisi za Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu KLABU ya Simba ya jijini ni miongoni mwa timu kumi zilizoidhinishwa na chama cha soka nchini (FAT) kushiriki michuano ya kugombea kombe la FAT. Simba imejitosa katika michuano hiyo inayoendeshwa katika mtindo wa mtoano ili kutafuta nafasi ya kuliwakilisha Taifa katika michuano ya kimataifa. Hiyo ni nafasi pekee na muhimu kwa klabu hiyo kongwe nchini kama kweli imedhamiria kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani. Timu zingine zitakazoshiriki michuano hiyo inayotazamiwa kuanza hivi karibuni ni Mtibwa, Ruvu, Tanzania Stars, Coastal, Prisons, JKT Stars, Moro United, Kajumulo na Yetu Afrika ya Dar es Salaam. Hasimu mkubwa wa Simba katika soka Yanga haitoshiriki michuano hiyo baada ya kushindwa kufuata taratibu zinazoongoza michuano hiyo. Washindi wawili katika mashindano hayo wataungana
na washindi wengine wawili wa kombe la Mapinduzi kutoka Zanzibar ambao
kwa ujumla watashiriki kombe la Nyerere ambapo bingwa ataliwakilisha taifa
katika kombe la Washindi barani Afrika.
Na Hamis Kasabe MWENYEKITI wa Kamati ya Muda ya Yanga, Tarimba Abbas Tarimba amesema, yeye sio mbabe na kamwe hatokuwa mbabe. Tarimba maarufu "Thabo Mbeki" amesema hayo juzi katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini katika mazungumzo na waandishi wa habari. Katika mazungumzo hayo, mwandishi mmoja alimwambia Tarimba kuwa yeye ni mbabe kutokana na desturi yake ya kuchagua vyombo vya habari na waandishi katika kutoa habari zinazohusu klabu yake. "Naomba ndugu waandishi mnielewe vizuri, mimi sio mbabe, kwa kweli mimi ni mtu mwenye heshima zangu, kwa hiyo ningependa jamii nielewe hivyo", alisema Tarimba kujibu shutuma hizo. Kadhalika, Tarimba alikanusha kubagua vyombo vya habari na waandishi katika kutoa nyeti za Yanga na akadai kama aliwahi kutokea hivyo basi ilisababishwa na yeye kufuatwa wakati akifanya kazi za Mwajiri wake Bahati Nasibu ya Taifa. Katika kuhakikisha hlo halitokei tena, Tarimba
ameweka utaratibu maalum wa kuongea na waandishi kwa mwezi mara moja ila
kwa dharura.
Na Mwandishi Wetu JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limefanikiwa kuingiza timu mbili kwa mkupuo katika ligi kuu Tanzania Bara kufuatia kumalizika kwa ligi daraja la kwanza nchini. Timu hizo ni Mbozi United ya Mbeya na 977 ya Arusha ambazo zitaungana na timu inayomilikiwa na jeshi la Magereza Prisons ya Mbeya. Timu zingine zilizofanikiwa kucheza ligi kuu bara mwakani ni Eighty two Rangers ya Shinyanga na Nazaret ya Njombe mkoani Mbeya. Cargo ya Dar es Salaam timu ambayo ilikuwa imepewa nafasi kubwa ya kushinda ligi hiyo imeambula nafasi ya tano ambayo haina manufaa. Cargo imeungana na timu zingine katika kufanya vibaya ambazo ni TPC ya Moshi, Ujenzi Rukwa na Wana Kimanumanu African Sports ya Tanga. Wakati huo huo Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka nchini (FAT) Amin Bahroon amesema zawadi kwa wafungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara zitatolewa Septemba 17 mwaka huu. Zawadi pia zitatolewa kwa washindi watatu wa ligi hiyo na kwa timu zilizoonyesha nidhamu ya hali ya juu wakati wote wa mashindano. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Wazanzibar
wawaambia Dk. Omar na Karume:
CCM ni nguruwe aliyenona - Mtopea Kabobe asisitiza uchaguzi huru Mkapa aomba kura kwa hoja ya uzawa Vifaa vya uchaguzi vimeanza kusambazwa Mizengwe yatupwa,wagombea upinzani wapeta USHAURI NASAHA
MAKALA
Kampeni za uchaguzi Zanzibar zimetosha kumvua chui ngozi ya mwana kondoo MPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MAKALA
CUF Tanga wamsihi Mufti wa BAKWATA aachane na siasa Kodi ya Maendeleo haitaondolewa -Mkapa |
|
|
|
|