|
Na. 065 Jumatano Septemba 13 - 19, 2000 |
|
|
|
|
|
Na Mwandishi Wetu Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Tanga kimemtaka Mufti wa BAKWATA, Sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed aachane na harakati za kisiasa na badala yake atatue matatizo ya BWAKWATA. Wito huo umetolewa na mgombea Ubunge wa Tanga mjini kwa tiketi ya CUF, Bw. Nuru A Diwani, katika waraka wake maalum wa Sept. 9,2000 uliolifikia gazeti la NASAHA. "Halikadhalika tungependa kumnasihi Sheikh Mkuu (Hemed bin Jumaa) kuwa yeye kama kiongozi wa dini ingekuwa bora sana kwake kujishughulisha na maendeleo ya taasi anayoiongoza (BAKWATA) kuliko kujiingiza katika siasa, jambo ambalo hana ujuzi nalo" ilisomeka sehemu ya waraka huo, na kuongeza "tunamkumbusha Sheikh Mkuu kuwa wakati yeye yupo ziarani majibu ya mitihani ya kidato cha sita yalikuwa yametoka na shule ya BAKWATA Al-Haramain imeshika mkia. Waislam na wananci kwa ujumla wanahaki ya kujua kwa nini shule za Mufti ni mabingwa wa kufelisha vijana wetu.Mufti kama kiongozi wa juu wa BAKWATA alistahili kushughulishwa na aibu ya hii na akaachia CCM yenyewe izungumze na Waislam." Nasaha za CUF kwa Mufti wa BAKWATA zinafuatia mkutano wa kiongozi huyo (Sheikh Hemed) alioufanya mjini Tanga, Septemba 1, mwaka huu, katika shule ya Jumuiya, na kuhudhuriwa naWaislam, na viongozi wa CCM na serikali. Lengo la mkutano huo kwa mujibu wa Sheikh Mkuu wa BAKWATA kama ilivyoelezwa katika waraka wa Bw. Diwani,lilikuwa kusahihisha fikra mbovu zinazodai kuwa Sheikh huyo anatembea mikoani ili kuipigia debe CCM. Kiongozi huyo wa BAKWATA alisema kuwa ziara yake mikoani haina uhusiano wowote na kuifanyia kampeni CCM. Hata hivyo,wana-CUF wa Tanga wanahoji kama ziara zakeza mikoani na mkutano wake huo wa September 1, haukuwa na lengo la kuipigia debe CCM, kwanini mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa CCM na serikali, na pia kwanini aliponda hutuba ya Prof. Lipumba, mgombea urais Kwa tiketi ya CUF. Katika ziara ya Mufti wa BWAKWATA na ujumnbe wake
mkoani Iringa iliwahi kuripotiwa kuwa Sheikh mmoja katika msafara huo alisema
ndani ya msikiti "Mkapa Oyee."
Na Mwandishi Wetu MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Rais Benjamin William Mkapa amesema akiingia tena madarakani hafikirii kuondoa, kupunguza au kufuta kodi ya maendeleo kwa sababu huo ndiyo mchango wa raia kwa serikali yao na ustawi wa jamii. Rais Mkapa ambae kipindi chake cha Urais kitakwisha siku chache baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29,mwaka huu, alisema hayo katika mfululizo wa mikutano yake ya kampeni ya Urais mkoani Iringa kwa kupitia CCM. Aidha katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii mjini Mafinga, mgombea huyo wa CCM aliwaahidi wakulima kuwapatia pembejeo za kisasa endapo atachaguliwsa tena kuwa Rais wa Tanzania.
Na Mwandishi Wetu WAZEE waliokuwa wafanyakazi wa jumuiya iliyovunjika ya Afrika Mashariki wamesema wanachotaka ni haki yao kama wafanyakazi wastaafu na sio kusaidiwa na serikali ya CCM. Kauli hiyo ya wazee hao inakuja kufuatia kauli iliyotolewa na Dr. Omar Ali Juma ambaye ni mgombea mwenza wa Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwishoni mwa wiki akiwa mkoani Sindiga. Katika mikutano yake mkoani humo, Dr. Omar ambaye kwa sasa ni makamu wa Rais alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema serikali itatoa sera ya kushughulikia matatizo mbalimbali yanayowakabili wazee, endapo CCM itarudi madarakani. Aidha alisema matatizo ya wazee yameainishwa katika Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka huu ambapo serikali ya CCM itaweka utaratibu ambao utawashirikisha wazee katika uchumi na mambo mengine ya kitaifa. Wakiongea na mwandishi wa habari hizi katika ofisi za gazeti la NASAHA jana, wazee hao waliostaafu walisema, wanasikitishwa na kauli ya CCM ambayo wamedai serikali yake imeshindwa kuwapa haki yao kama wafanyakazi waliostaafu na badala yake inadai inataka kuwasaidia. "Hivi CCM ina nini jamani, kati yetu kuna wazee waliandikiwa cheki ya shilingi 10 (kumi)kama malipo ya mtu aliyestaafu, halafu leo wananadi wana mipango ya kutusaidia, huu ni uongo mtupu", alisema mzee mmoja kwa uchungu ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini. Mzee mwingine ambaye naye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema kama CCM haina sera ya kuwavutia wananchi wasitumie mgongo wa wazee. "CCM ni chama kikongwe kama kimeishiwa sera iwaachie wengine watawale wasitumie mgongo wetu", alisema mzee huyo na kuongeza "haya tuliyofanyiwa na serikali ya CCM hatutayasahau mpaka kufa kwetu". |
YALIYOMO
TAHARIRI
Wazanzibar
wawaambia Dk. Omar na Karume:
CCM ni nguruwe aliyenona - Mtopea Kabobe asisitiza uchaguzi huru Mkapa aomba kura kwa hoja ya uzawa Vifaa vya uchaguzi vimeanza kusambazwa Mizengwe yatupwa,wagombea upinzani wapeta USHAURI NASAHA
MAKALA
Kampeni za uchaguzi Zanzibar zimetosha kumvua chui ngozi ya mwana kondoo MPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MAKALA
CUF Tanga wamsihi Mufti wa BAKWATA aachane na siasa Kodi ya Maendeleo haitaondolewa -Mkapa |
|
|
|
|