|
Na. 065 Jumatano Septemba 13 - 19, 2000 |
|
|
|
|
|
Kabobe asisitiza uchaguzi huru
MKUU wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Askofu Mkuu Zakaria Kakobe, ameendelea kuitaka serikali kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka huu unakuwa huru na haki ili kuepusha vurugu. Kwa mujibu wa gazeti moja la kila siku, Askofu Kakobe ametahadharisha kuwa endapo haki haitotendeka, wananchi hawatokubali kudhulumiwa na hivyo wanaweza kudai haki yao kwa nguvu, jambo linaloweza kupelekea kuvunjika kwa amani nchini. Ameikumbusha serikali na vyombo vyake kutoa haki sawa kwa vyama vyote , kwani alisema kiongozi huyo wa dini, amani ya kweli haipatikani paliposhamiri dhuluma. Askofu Kakobe mara kadhaa amekuwa akiikosoa CCM
na serikali yake hadharani, jambo ambalo liliwahi kupelekea kutupiana maneno
kati yake na viongozi hao wa chama tawala. Mathalani,aliwahi kuwataka wananchi
kuihoji CCM kile ilichowafanyia kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita kabla
ya kuipa tena ridhaa ya kuongoza kipindi kingine cha miaka mitano.
Na Mwandishi Wetu MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ndie rais anaemaliza muda wake Oktoba, Mhe.Benjamin Mkapa amewataka wananchi wa Mtwara wamchague kwa sababu amezaliwa mkoa huo. Akinukuliwa na gazeti moja la Jumapili iliyopia (Na. 018729)Rais Mkapa aliwataka wananchi hao wampigie kura kwa wingi kwa sababu amezaliwa katika mkoa wa Mtwara. Mhe. Mkapa ni mzaliwa waMasasi mkoani humo. Hata hivyo, gazeti hilo limemripoti Rais Mkapa
katika ziara yake ya kampeni mkoani Mtwara akiwataka wananchi wasivichague
vyama vya upinzani kwa sababu sera zao ni za ubaguzi wa kikabila,jino kwa
jino,udini na jinsia.
Na Mwandishi Wetu VIFAA kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu vimeanza kusambazwa sehemu mbali mbali nchini, imefahamika. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini jana, vifaa hivyo vimeanza kusambazwa jana kwa lengo la kuepuka matatizo yaliyojitokeza katika uchaguzi wa 1995. Aidha Tume hiyo ya uchaguzi imesema haina nguvu ya kisheria kuwadhibiti wanasiasa wanaofanya vurugu na kutumia udini katika kampeni. Mwanzoni mwa wiki hii, imeripotiwa kuwa baadhi
ya wagombea ubunge waliripotiwa kupigiwa debe makanisani huko mkoani Kilimanjaro.
Na Mwandishi Wetu MIZENGWE iliyodaiwa kuwekwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Liwale dhidi ya wagombea udiwani wa upinzani, hatimaye imetupwa na tume ya taifa ya uchaguzi na wagombea hao kuruhusiwa kuendelea na kampeni. Mizengwe hiyo iliyodumu kwa takriban siku 20 imekwisha kufuatia juhudi kubwa zilizofanywa na Katibu wa CUF wilaya ya Liwale Bw. Ahmed Mmou na Tume ya Uchaguzi ya Taifa ya chama hicho. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Bw. Mmou alisema kuwa pamoja na kuchelewa kwa makusudi kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo kutoa fomu kwa ajili ya madiwani, alitangaza kubadilika kwa picha kutoka zile za rangi na kuwa za kawaida (Blackand White) Aogist 14. Wagombea wa upinzani waliwasiliana na mpiga picha ambaye alipiga picha na kwenda kusafisha picha hizo Nachingwea akiahidi kurudisha picha hizo Agosti 17, lakini mpaka Agost 18 siku ya mwisho ambayo maelezo na picha za wagombea zilitakiwa kubandikwa kwenye ubao wa matangazo, mpiga picha huyo alikuwa hajarejea. Bw. Mmou alidai kuwa walimsihi msimamizi huyo kuwa aruhusu kubandikwa kwa picha za rangi ambazo zilikuwa zimeshaambatanishwa na maelezo mpaka zitakapoletwa picha nyeusi kutoka Nachingwea .Msimamizi huyo alikataa katakata, huku akiwatuhumu kuwa ni wazembe. Ilipofika saa 11.30 jioni ya siku hiyo baadaya kwisha muda, mpiga picha huyo alirejea jambo ambalo alidai Bw. Mmou liliwajengea dhana kuwa kuna mchezo umefanyika wa kuwahujumu. Baada ya hapo ulianza msururu wa mawasiliano ya barua kati ya viongozi wa upinzani jimboni humo na msimamizi huyo,lakini haikusaidia. Ndipo Bw. Mmou alipoamua kuja moja kwa moja hapa jijini kuwasiliana na tume ya Taifa ya uchaguzi ambayo, baada ya kukaa kikao chake maalum kwa ajili hiyo, wagombea hao waliruhusiwa kuendelea na kampeni zao. Mratibu wa uchaguzi wa Kanda ya Kusini alitarajiwa kuondoka jana kwenda Liwale kupelekea barua kwa wagombea hao na kwa msimamizi wa uchaguzi jimboni humo. Majina yawagombea udiwani haowa upinzani navyama vyao ni kama ifuatavyo:- Hassan Mkupeta,Saidi Abdallah (NCCR-Mageuzi) naJaphet AliKumbinga (CHADEMA). Kutoka CUF wapo Ahmad Nakwenda, AliLigai, Abdallah Ngatomela na Hemed Rashid. Wengine ni Abdallah Ngalemba, Kasim Kikowela, Ahmed A. Mmou na Abdallah Makere. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Wazanzibar
wawaambia Dk. Omar na Karume:
CCM ni nguruwe aliyenona - Mtopea Kabobe asisitiza uchaguzi huru Mkapa aomba kura kwa hoja ya uzawa Vifaa vya uchaguzi vimeanza kusambazwa Mizengwe yatupwa,wagombea upinzani wapeta USHAURI NASAHA
MAKALA
Kampeni za uchaguzi Zanzibar zimetosha kumvua chui ngozi ya mwana kondoo MPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MAKALA
CUF Tanga wamsihi Mufti wa BAKWATA aachane na siasa Kodi ya Maendeleo haitaondolewa -Mkapa |
|
|
|
|