NASAHA
Na. 065 Jumatano Septemba 13 - 19, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Kampeni za uchaguzi Zanzibar zimetosha kumvua chui ngozi ya mwana kondoo

Na M.M. Mbogo 

KWA mtu yeyote mwenye uelewo wa matatizo ya kisiasa Zanzibar asingesita kukubali kuwa maneno hayo matamu ya Bwana Amani yalikuwa na dawa ndani yake ya ugonjwa sugu wa kisiasa huko Zanzibar. Hapana shaka kwamba uzito wa maneno ya Bwana Karume ndiyo yaliyomfanya Maalim Seifu kumsifia kama mmoja wa vijana wazuri ndani ya CCM. Lakini tofauti na wananchi wengi wasioona upeo mkubwa wa siasa za CCM, Maalimu Seifu aliyatizama maneno ya Amani kwa jicho la shaka kubwa. Yeye kama mwanasiasa mkomavu aliamini kuwa msimamo wa Amani binafsi ulikuwa unapingana vikali na msimamo wa Chama Cha Mapinduzi na serikali yake. Kauli mbalimbali za Maalim Seifu zinaashiria kuwa alikuwa akimuonea huruma Bwana Amani kutamka maneno ambayo kutokana na uchanga wake wa kisiasa na upeo wake mdogo wa kimaono alidhani kuwa yanaweza kutekelezeka ndani ya mashua ya CCM. 

Kwa upande mwingine, Maalim Seifu alituonea huruma Watanzania kwa usahaulifu wetu. Hii ni kweli kwa kuwa tulikuwa tumeusahau usemi tajiri wa mababu zetu wa Kiswahili kwamba mtoto wa simba ni simba.: Tulimtizama Amani katika sura yake binafsi bila kukumbuka kwamba Amani alikuwa sura ndani ya CCM Na kama mmea Amani alikuwa ni kahawa ambayo isingeweza kuzaa mkarafuu. 

Kwa kuwa dalili za mavuno mema huonekana katika kipindi kizima cha ukuaji wa mazao, bila shaka kipindi cha kampeni cha mwezi mmoja kinatosha kutoa dalili ya kuwepo mavuno mema ama kinyume chake. Mdahalo wa kisiasa kati ya Amani na Maalim Seifu ulikuwa na mafundisho makubwa juu ya hatma ya Zanzibar. 

Akijibu swali la nia yake ya serikali ya shirikisho, bwana Amani alilazimika kuufunua ukweli pale aliposema suala hilo linategemea na maamuzi ya vingunge vya CCM Mpaka sasa sera ya CCM imeshasambazwa mikononi mwa wananchi lakini kwa bahati mbaya iko kimya juu ya serikali ya umoja wa kitaifa. 

Kana kwamba haitoshi, katika mikutano yake mbalimbali ya kampeni, Bwana Amani alishatamka wazi kwamba hataunda ya serikali ya umoja wa kitaifa. Kama hili lilitokana na maelekezo toka kwa vingunge wa chama au mawazo yake binasfsi ni suala linalozua utata mkubwa wa kisiasa. Utata huu unaongezeka zaidi tukikumbuka kuwa katika mdahalo, bwana Amani alinukuliwa akikubaliana na Maalim Seifu kwamba suala la muundo gani wa Muungano unatakiwa linategemea maoni yaWazanzibari. Lakini hivi karibuni Bwana Amani ameripotiwa akisema sera ya CCM ni kuudumisha Muungano katika sura tata iliyopo ya serikali mbili. Hatujui kama bwanaKarume aliyasema haya akiwa na kumbukumbu na aliyoyasema huko nyuma. 

Halafu, kuna siku nyingine Bwana Karume alisema atakapoingia madarakani utakuwa ndiyo mwisho wa Chama cha CUF. Kauli hii inampa Bwana Amani sura ya kidikkteta ambayo inapingana vikali na katiba ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar. Hamna njia yoyote anayoweza kuitumia Bwana Karume kukiuwa chama cha CUF zaidi ya njia zilizo kinyume cha katiba, njia ambazo kama zitatumika zitaiweka Zanzibar katika msiba mkubwa kabisa. 

Iwe itakavyokuwa, hali halisi ya siasa ya Zanzibar inahitaji kuwepo kwa serikali ya (shirikisho) umoja wa kitaifa. Mgawanyiko uliyopo kati ya Wapemba naWaunguja ni tatizo la kihistoria ambalo linahitaji hekima na busara kulitatua na siyo jazba za kisiasa. Haitoshi kujaza majeshi na kuzuia uhuru wa wananchi wa kujumuika na wenzao, kwani hiyo inaweza kuleta suluhisho la muda mfupi tu na ambalo baadaye laweza kuwa boma baya la kuwamaliza Wanzazibar. Tusikubaliane na kauli za kichovu kwamba Maalim Seifu au Salmin ndiyo chanzo cha tatizo hilo. Tatizo hilo lilikuwepo isipokuwa tulimekuja kufunuliwa nguo na mfumo wa vyama vingi. 

Kwa wale wote wanaopenda kuiona Zanzibar ikirudia katika amani na utulivu ni lazima tuwatizame wagombea uraisi na vyama vyao kwa jicho la upevu. Tushukuru Mungu kwamba kipindi kifupi cha kampeni ya uchaguzi kimeweza kumvua mwana kondoo ngozi ya chui. Ole wenu mtaokubali kujipeleka wenyewe kwa mwananchi mkizilazimisha fikra zenu na macho yenu kumuona kama kondoo. 

Mungu Ibrariki Tanzania, Mungu Ibariki Zanzibar. Mungu wape mwanga wapiga kura, kura zao zilete amani, haki na usawa. 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Tume, kauli ipi sawa? 

CCM maji shingoni 

Wazanzibar wawaambia Dk. Omar na Karume:
Kura tutawanyima, mtang’oka 

CCM ni nguruwe aliyenona - Mtopea 

Kabobe asisitiza uchaguzi huru 

Mkapa aomba kura kwa hoja ya uzawa 

Vifaa vya uchaguzi vimeanza kusambazwa 

Mizengwe yatupwa,wagombea upinzani wapeta 

HABARI ZA KIMATAIFA

USHAURI NASAHA
Haya ndiyo mambo ya wanawake - 2 

MAKALA
Kura ni silaha 

Kampeni za uchaguzi Zanzibar zimetosha kumvua chui ngozi ya mwana kondoo 

MPASHO NASAHA
BEN NA BULLY 

MAKALA
Wimbo wa Umoja na Amani wa CCM  ni ghilba za kisiasa 

KALAMU YA MWANDISHI
Hojini Ubalozi wa Vatican kwanza 

MAKALA
CCM kushinda uchaguzi bila kupigiwa kura? 

MAKALA
Mwenye macho haambiwi tazama - 4 

CUF Tanga wamsihi Mufti wa BAKWATA aachane na siasa 

Kodi ya Maendeleo haitaondolewa -Mkapa 

Wazee waijibu CCM 

BARUA

MASHAIRI

MICHEZO

  • Yanga watakiona - Kajumulo
  • Simba yajaribu kombe la FAT
  • Tarimba akataa ubabe
  • Jeshi laongeza timu Ligi Kuu

  •  

       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita