|
Na. 065 Jumatano Septemba 13 - 19, 2000 |
|
|
|
|
|
Upinzani washinda Mauritius KUFUATIA ushindi wa muungano wa upinzani nchini Mauritius, Waziri Mkuu Rom Gullam wa nchi hiyo ameahidi kujiuzulu baadaye wiki hii. Ushindi huo wa robo tatu ya viti vyote katika bunge umeifanya upinzani kupata viti 50 kati ya 70. Waziri Mkuu wa nchi hiyo inayotamba barani Afrika kwa kiwango chake cha kukua kwa uchumi kwa mwaka na mfano wa kuigwa kwa demokrasia, ameahidi kujiuzulu pamoja na kuwa ameweza kutetea kiti chake bungeni. Asilimia kuwa ya wakazi wa kisiwa hicho cha Mauritius
ni wa asili ya asia.
SERIKALI ya Burundi imetuhumu Tanzania kwa kuruhusu ardhi yake kutumiwa na waasi wa nchi hiyo ambayo imedai huingia nchini huo kufanya mashambulizi na kurejea Tanzania. Taarifa zilizotolewa kwa waandishi wa habari na Afisa wa jeshi la Burundi mjini Bujumbura. Katika hatua hiyo, majeshi ya Burundi, alisema afisa huyo majeshi yamesogezwa kwenye eneo la kusini mashariki ya mpaka wa nchi hiyo ambayo yanapakana na mkoa wa Kigoma. Aidha, nchi hiyo imeitaka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuhakikisha nchi hizo haziruhusu ardhi zao kutumika na waasi hao ili kusaidia kuwepo kwa amani katika nchi hiyo ndogo ya Afrika ya kati iliyoathiriwa vibaya na vita ya kikabila. Nchi hiyo imependekeza kuwa Tanzania na DRC zishirikishwe kikamilifu katika utafutaji wa amani nchini humo ili kuweza kuwadhibiti waasi. Mara kwa mara serikali ya Burundi imekuwa ikiituhumu
nchi jirani ya Tanzania kwa kuhifadhi waasi na kuwaruhusu kuishambulia
nchi hiyo. Lakini serikali ya Tanzania mara zote imekuwa ikikanusha.
WAPINZANI wa chama cha MLC kinachoendesha mapigano dhidi ya serikai ya Rais Laurent Kabila wa DRC kimetangaza kupata mafanikio baada ya kuuteka mji wa Dongo. Chama hicho chenye kuongozwa na Bw. Jean Pierre Bemba hivi karibuni kilitangaza kuanza kwa mapambano makali ya kuikomboa miji yote iliyotekwa na majeshi ya serikali. Katika mapigano hayo ya siku tatu ya kuuteka mji wa Dongo, Chama hicho kimedai kuwakamata mateka askari 43 wa serikali na kuwakamata wengine 100. Aidha kimedai kuwa wapiganaji wake wanne wameuawa. Mpaka sasas hakuna duru zozote huru zilizokanusha au kuthibitisha taarifa hizo zilizotolewa na katibu mkuu wa MLC. Vyombo vya habari vya serikali vimelaumu kuvunjwa kwa mkataba wa amani wa Lusaka kunakofanywa na MLC ambacho kimepania kumwondoa madarakani kwa njia ya mtutu Rais Laurent Kabila. DRC imekuwa katika kipindi kirefu cha vita vya
ndani tangu kuangushwa kwa utawala wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Mobutu
Seseseko.
WAPIGANAJI wa Kiislamu katika jimbo linalopigania uhuru wa kujiamulia mambo yake kutoka India wamewaua askari wanne wa jeshi la India katika shambulizi la kushutukiza la kujitoa muhanga. Shambulio hilo ambalo lilipelekea mapigano ya masaa sita, liliisha kwa India kushambulia kwa mizinga na maroketi jengo moja ambalo wapiganaji wawili wa Kashmir waliuawa. Katika tukio jingine mwanamke mmoja aliuawa baada ya kutokea mapigano katika eneo la Kashmir linaloshikiliwa kwa pamoja na India na Pakistan ambapo makombora yalitumika. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Wazanzibar
wawaambia Dk. Omar na Karume:
CCM ni nguruwe aliyenona - Mtopea Kabobe asisitiza uchaguzi huru Mkapa aomba kura kwa hoja ya uzawa Vifaa vya uchaguzi vimeanza kusambazwa Mizengwe yatupwa,wagombea upinzani wapeta USHAURI NASAHA
MAKALA
Kampeni za uchaguzi Zanzibar zimetosha kumvua chui ngozi ya mwana kondoo MPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MAKALA
CUF Tanga wamsihi Mufti wa BAKWATA aachane na siasa Kodi ya Maendeleo haitaondolewa -Mkapa |
|
|
|
|