|
Na. 065 Jumatano Septemba 13 - 19, 2000 |
|
|
|
|
|
S.L.P. 72045, Dar es Salaam Tume, kauli ipi sawa? Hivi karibuni imeripotiwa katika vyombo vya habari, kauli za baadhi ya viongozi wa juu wa Chama Tawala ambazo tunadhani zinadhalilisha katiba ya nchi na demokrasia. Kauli za kwamba, wakishinda hatuwachii. Kauli kwamba, magari ya kivita yameandaliwa kupambana na wapizani. Au kauli za majigambo kwamba wananchi wapige kura wasipige kura chama tawala kitashinda. Nchi yetu ni huru. Haiko chini ya utawala wa Kikoloni wala wa kijeshi ni nchi inayoongozwa na katiba; katiba inayoashiria kuwepo kwa serikali iliyoingia madarakani kwa ridhaa ya wananchi. Ni kwa mujibu wa katiba hiyo, leo tuna vyama vingi, vyama ambavyo ni vya wananchi na vyote vina haki na hadhi sawa mbele ya katiba. Hivi sasa tupo kwenye kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika mwisho wa mwezi ujao kwa mujibu wa katiba ya nchi. Uchaguzi mkuu ni fursa ya wananchi kuchagua viongozi wa chama kitakachounda serikali waitakayo. Serikali gani itakayochaguliwa ni siri ya wananchi itakayojulikana baada ya Oktoba 29 mwaka huu. Na ili hilo litimie hapana budi katiba ya nchi iheshimiwe, na sheria zilizounda tume ya uchaguzi, na zile zinazosimamia taratibu za uchaguzi pia ziheshimiwe. Wenye wajibu wa kuhakikisha yote hayo ni tume ya uchaguzi. Hivyo Tume ya Uchaguzi ina wajibu wa kuweka mazingira muafaka ambayo yatahakikisha kuwepo kwa haki na uhuru kwa mwananchi kujiandaa hivi sasa na kupiga kura tarehe 29 Oktoba pasipo vitisho, hadaa,kejeli au kebehi. Hivyo tunaposikia kauli kama hizo zilizotolewa na viongozi wa chama tawala siku kadhaa zilizopita, na tume kukaa kimya hatuna budi kujiuliza kama ambavyo wananchi wengi wamekuwa wakijiuliza, je, kauli hizo ni sahihi? Kauli za kwamba wakishinda hatuwaachii, haziendi kinyume na katiba? Na zile za kuwatangazia wananchi vitisho vya magari ya jeshi vinakubalika? Au zile za kuwaambia wananchi "watake wasitake, mpige kura msipige tutashinda", zinaashiria nini? Hivyo ni tegemeo letu kwamba tume haitoendelea kuzinyamazia kauli hizo maana itakuwa ni sawa na kuwaachia wananchi wachukue hatua zifaazo. Hatuamini kwamba hiyo ndiyo nia ya tume. Bado tuna imani na matarajio mema kwa Tume kutimiza wajibu wake. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Wazanzibar
wawaambia Dk. Omar na Karume:
CCM ni nguruwe aliyenona - Mtopea Kabobe asisitiza uchaguzi huru Mkapa aomba kura kwa hoja ya uzawa Vifaa vya uchaguzi vimeanza kusambazwa Mizengwe yatupwa,wagombea upinzani wapeta USHAURI NASAHA
MAKALA
Kampeni za uchaguzi Zanzibar zimetosha kumvua chui ngozi ya mwana kondoo MPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MAKALA
CUF Tanga wamsihi Mufti wa BAKWATA aachane na siasa Kodi ya Maendeleo haitaondolewa -Mkapa |
|
|
|
|