|
Na. 065 Jumatano Septemba 13 - 19, 2000 |
|
|
|
|
IMEDAIWA kuwa kusitishwa kwa mikutano ya kampeni ya wazi ya wagombea ubunge wa CCM hapa jijini, na kuanzishwa ya ndani kunatokana kukabiliwa na 'hali ngumu', ambapo mikutano yao imekuwa ikihuduriwa na wananchi wachache ikilinganishwa na wale wanaohudhuria ile ya wapinzani hususani Chama cha Wananchi (CUF). Imefahamika kuwa mikutano hiyo ya kampeni imesimamishwa katika majimbo kadhaa ikiwemo Ubungo, Kigamboni, Kinondoni na Kawe. Uchunguzi wa gazeti hili katika jimbo la uchaguzi la Kigamboni umebaini kuwa tangu kufanyika mikutano mitatu ya awali, ambayo mgombea wake ubunge Mzee Kitwana Kondo hakuhudhuria, chama hicho hakijafanya tena mkutano wa hadhara wa kampeni. Toka kuanza kwa kampeni hizo za uchaguzi imekuwa ikiripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa mikutano ya kampeni ya CCM licha ya kuhudhuria na wananchi wachache, imebainika kuwa miongoni mwao wengi huwa ni wanachama wa kambi ya upinzani. Wanachama kadhaa wa CCM hapa jijini wameilaumu hatua hiyo ya chama chao kwa madai kuwa itazidi kukidhoofisha chama hicho na kuwaongezea nguvu wapinzani wapinzani katika kampeni zinazoendelea kwa kuonekana wao (CCM) wameyakimbia majukwaa. Wakati huo huo habari kutoka Moshi zinasema hali si shwari kwa mgombea wa CCM wa ubunge wa Jimbo hilo Bibi Elizabeth Mara Minde. Habari hizo zimeeleza kwamba baada ya CCM kukabwa koo na mgombea wa CUF-CHADEMA, Bw. Philemon Ndesamburo, imeamua kukimbilia kanisani kwenda kuomba kura. Habari hizo zilizo mkariri Bw. Ndesamburo zimedai kuwa mgombea huyo wa CCM amekuwa akipigiwa kampeni makanisani na viongozi wa ngazi za juu wa CCM koani humo. Nao wagombea ubunge wa CCM katika majimbo ya Ubungo na Ukonga, Bw. Charles Keenja na Milton Makongoro,wamedaiwa kufanya kampeni makanisani kufutia hatua yao ya kuchangia kwaya ya Kanisa katika kipindi hiki cha kampeni. Wagombea hao wa ubunge kwa pamoja waliichangia
kwaya ya kanisa la Lutheran Kimanga, hapa jijini hivi karibuni.
Kura tutawanyima, mtang'oka
WANANCHI katika Visiwa vya Zanzibar wamesema hawatishiki na kauli za "kibabe" zinazotolewa na viongozi wa CCM na badala yake watakinyima kura chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao hali ambayo itakifanya chama hicho king'oke madarakani. Wakizungumza katika nyakati tofauti na mwandishi habari hizi Visiwani humo, wananchi hao pia wamesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawahadaa wananchi juu ya muungano kwa vile wana-CCM wenyewe wameonesha kutofautiana juu ya muundo wa muungano. Wakitoa maoni yao juu ya kauli za "kibabe" za CCM wananchi hao wamesema wameshangazwa na kauli ya mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Omar Juma kwamba CCM itashinda tu hata kama wananchi hawataipigia kura. Wameendelea kueleza kwamba wameshanyanyashwa na kauli ya Dk. Omar ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri, aliyoitoa akieleza kwamba majeshi yanaletwa Zanzibar ili kukidhibiti Chama cha Wananchi(CUF). "Kauli hii ya Dk. Omar inaonesha CCM inadharau wananchi kwamba wao ndio wenye uwezo wa kukiweka chama madarakani... na hii ni dalili ya kulewa madaraka", alisema mmoja wa wananchi hao na kasha akaongeza kwamba wao waliitarajia CCM iwaombe kura sio kuwaambia wasipoipigia kura watashinda tu. Mwananchi mwingine, Bw.Abdulhamid Hassan amesema huenda CCM inao mpango wa kuiba kura na ndio sababu wanajihakikishia ushindi. "... huenda wana mpango wa kuiba kura ndio maana wana jeuri kiasi hicho; lakini sisi tunasema kura tutawanyima na watang'oka na tunawaonya kuchezea kura za wananchi", alisema Bw. Abdulhamid. Wakizungumzia majeshi kupelekwa Visiwani kwa ajili ya "kuwadhibiti CUF" wananchi hao wamesema CCM inalitumia visivyo jeshi hilo. "tunavyojua sisi kazi za jeshi ni kulinda usalama wa nchi na sio kupinga chaguo la wananchi", alisema Bw. Mahamound Makame wa mjini Unguja. Katika siku za karibuni, magari kadhaa ya dereya yalipelekwa Zanzibar ambapo Dk. Omar alieleza kuwa hatua hiyo ilifanywa kuwadhibiti wana-CUF. Akielezea zaidi vitisho vya dola dhidi ya wananchi, Bw.Makame alitolea mfano mkutano wa CUF uliovunjwa na polisi. Mwananchi mwingine aliyejitambulisha kama Ali Salim, amesema, Dk. Omar na mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Bwa Amani Karume. Wasiwahadae wananchi juu ya muungano. "Yaelekea Karume hajui sera za chama chake, na yeye hana nguvu yoyote katika CCM.....CCM ilikwishaweka wazi sera yake kuhusu muungano kuwa na serikali mbili kuelekea moja", alisema. Katika moja ya mkutano ya kampeni ya chama chake, Bw.Karume alisema akiingia madarakani ataendeleza muungano wa serikali mbili kwa vile muungano wa serikali moja au tatu muda wake haujafika. Bw.Salim ambaye alidai ni mwana-CCM alisema, "Zanzibar ilikwisha mezwa siku nyingi... tulitaka kubadilisha katiba yetu tukazuiliwa, tulimpendekeza Dk. Bilal agombee urais, wenzetu CCM Bara wakakataa. "Mwaka ule tulijiunga na OIC; Bara wakatuambia tujitoe mara moja, na Rais wetu (wa Zanzibar) sasa wamemvua madaraka yake katika hiyo serikali ya Muungano", alisemana kuongeza kwamba ingawa yeye na CCM lakini anaamini kwamba CUF ndio itakayoweza kuirejesha hadhi ya Zanzibar kama nchi. "CUF nao wanataka serikali tatu, na hali hasa ndio suluhisho la hadhi ya Zanzibar. Mwananchi mwingine, Bi Husma Idd amesema anawashangaa CCM kudai kuwa Bara inaisaidia Zanzibar kulipa mishahara ya wafanyakazi wake. "Sisi hatukuungana eti ili tusaidiwe na huyo Tanzania
Bara, Mzee wetu Karume hakusaini mkataba wa Bara kuisaidia Zanzibar....
Lakini juu ya yote kama Zanzibar kuna hali mbaya ya nchi nani wa kulaumiwa
kama sio hiyo hiyo CCM", alisema Bi. Husna.
Na Mwandishi Wetu Bw. Kassim Mtopea ambaye hivi karibuni aliibuka na kuanza kukipigia debe Chama cha Mpinduzi (CCM) amekifananisha chama hicho tawala na nguruwe aliyenona. Mtopea ambaye CCM wanamwita Sheikh, alikuwa akiongea katika mkutano wa kampeni uliofanyika Yombo,wa kumnadi mgombea ubunge (CCM) wa jimbo la Temeke, Bi Khadija Kusoga alisema CCM ni nguruwe kwa sababu CCM inao viongozi bora, wanaoleta maendeleo. Kauli hiyo ya Mtopea imeungwa mkono na baadhi ya wana-CCM waliohudhuria mkutano huo,ambao wamesema chama chao kimekuwa ni sehemu ya watu wengi kukimbilia huko kwa ajili ya maslahi ya kiuchumi, ambapo watu hao wamekuwa wakihama vyama vyao na kujiunga na CCM kwa matarajio ya kupata riziki zao. Kabla ya kujiunga na CCM, Bw. Mtopea aliwahi kuwa mpiga debe wa NCCR-Mageuzi na baadaye TLP. Hata hivyo baadhi ya wanachama hao wameeleza kuwa kauli hiyo ya mpiga debe huyo wa CCM imekidhalilisha chama chao ambacho ndicho tawala. "Katika jamii yetu, nguruwe ni mnyama mchafu,anakula hovyo na asiyekubalika sana, sasa iweje CCM ifananishwe na kitu kisichokubalika katika jamii", alihoji mwana-CCM mmoja. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Wazanzibar
wawaambia Dk. Omar na Karume:
CCM ni nguruwe aliyenona - Mtopea Kabobe asisitiza uchaguzi huru Mkapa aomba kura kwa hoja ya uzawa Vifaa vya uchaguzi vimeanza kusambazwa Mizengwe yatupwa,wagombea upinzani wapeta USHAURI NASAHA
MAKALA
Kampeni za uchaguzi Zanzibar zimetosha kumvua chui ngozi ya mwana kondoo MPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MAKALA
CUF Tanga wamsihi Mufti wa BAKWATA aachane na siasa Kodi ya Maendeleo haitaondolewa -Mkapa |
|
|
|
|