AN-NUUR 
Na.180 Shaaban 28 - Ramadhan 1419, Desemba 18 - 24, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Mlo wa Daku 

Na Mujahid Mwinyimvua 

KATIKA makala ya chakula na lishe ya wiki iliyopita tulitoa somo maalum (futari ya tende) kwa ajili ya wasomaji wetu Waislamu wanaotarajia kuanza funga ya mwezi wa Ramadhani siku chache zijazo. 

Kwa muhtasari tulisema kwamba Waislamu na wanadamu wote kwa ujumla wanahimizwa na Qur’an kufanya uchaguzi wa vyakula wanavyokula (tazama Qur’an 2:168, 2:178, 5:88). Sababu ya uchaguzi huo ni kwamba Mwenyezi Mungu katika kuumba kwake vyakula vingine anavifanya bora kwa kula (ladha, virutubisho n.k.) kuliko vingine (tazama Qur’an 13:4). 

Vile vile tulisema kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.) amewahimiza sana Waislamu kufuturu kwa tende. Pamoja na vitu vingine, tende ina sukari (glucose) ambayo inaweza kuyeyuka kwa haraka tumboni na hivyo kuweza kutumika na mwili kwa muda mfupi na hivyo kuweza kuupa mwili nguvu (nishati). Jambo hili ni muhimu sana kwa mtu aliyefunga. 

Pia tulisema kwamba, kwa kuzingatia virutubisho vinavyopatikana katika tende, futari yoyote ile lazima itengenezwe kwa kutumia vyakula vyenye sukari na pia vyakula futari hivyo visiwe na mafuta mengi. 

Makala yetu ya wiki hii mwendelezo wa kusudio la makala ya wiki iliyopita. Somo tuliloliwakilisha wiki hii ni mlo wa daku. 

Katika makala hii neno daku ni chakula kinacholiwa usiku wa manane kwa ajili ya kujiandaa kufunga siku inayofuata. 

Kula daku ni sunnah aliyoikokoteza sana Mtume (s.a.w.) kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo: 

"Anas (r.a.) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Kula daku kabla ya alfajiri kwa sababu katika daku kuna baraka". (Abu Daud). 

Mlo wa daku unaweza kuwa mlo wowote ule hata kama maji ya kunywa kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo: 

Amesema Abu Said Khudri (r.a.) kwamba: "Daku ni baraka kwa hiyo msiliache japokuwa kwa tunda la maji. Maana Mwenyezi Mungu na Malaika wake huwarehemu wanaokula daku". (Ahmad) 

Hata hivyo, ni vyema ikakumbukwa kwamba kusudio kubwa la daku ni kumpa nguvu mfungaji na ndiyo maana Mtume (s.a.w.) alihimiza watu kula daku karibu na alfajiri. Mtu asidhani kuwa kula daku mapema kuwa ndiyo ucha Mungu. Ibada ya funga (na nyinginezo) haikukusudiwa kuwatesa wafungaji. 

Mlo wa daku lazima uwe mlo kamili (balanced diet) hasa kama mtu hakupata mlo mwingine baada ya kufuturu. Kitendo cha kuchelewesha mlo wa daku na kuwahi kufuturu (mambo ambayo yanasisitizwa na Uislamu) maana yake ni kuwa muda wa mwili kukosa chakula unapungua. Hivyo basi afya ya mfungaji haiathiriki. 

Mtume (s.a.w.) kama alivyosisitiza kufuturu kwa tende pia amehimiza daku ya tende. Haya tunayapata katika Hadith ifuatayo: 

Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Ni uzuri ulioje kwa muumini kula daku ya tende kabla ya alfajiri". (Abu Daud) 

Katika toleo lililopita katika mfululizo huu, kimakosa tulichapisha kuwa futari iwe na mafuta mengi, lakini usahihi ni kwamba futari isiwe na mafuta mengi. Tunawaomba radhi mwandishi na wasomaji wetu.  

- Mhariri 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri
Umaskini unachafua mazingira!

Mauaji ya Mwembechai: Spika wa Bunge aombwa atoe gharama za kuunda Tume

UWAWARU yafa Rufiji

UN yaidhinisha udhalimu wa Marekani

Qur’an yachomwa moto Shinyanga

Marekani yadhihirisha Ubeberu wake

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: SEXUAL SADISM
Na. Abu Halima Sachangwa

Kitengo cha Zaka chazinduliwa Dar

Tume ya Jiji kubomoa Msikiti wa vipofu

Akheri ya zamani
Na Alhaj Yusuf Kalala, Washington DC. USA

UWAWARU yaleta nusura Ikwiriri

Tamko la Masjid NNUUR juu ya kuanzishwa kwa UWAWARU

Kuanzishwa kwa UWAWARU

Wasomi Waislamu wawajibike
Na Mwandishi Wetu

Albucasis  936 - 1013 (CE)

Ijue Uhuru madrasa - Morogoro

Madrasa Akhlaqil Islamiya yapiga hatua

MADRASATUL Husseiniyi Shadhily
Na Jamillah Nassoro
 
Hatimaye kesi ya kushambulia kituo nayo yafutwa

Changieni vyombo vya mihadhara - Sheikh Said

Misikiti yakosa maji ya kutawadhia

Bakwata Tanga haifuati katiba yake

Sheikh Mbukuzi ataka Waislamu watafute radhi za Allah

Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? - 3
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache - 3
Na Yasin Valerian Massawe

Sheikh Omar Bashir afikishwa mahakamani

Mufti pekee kuidhinisha watu kufunga

Nguruwe wanaofugwa maeneo wanayoishi watu kusababisha magonjwa ya kuambikiza

200 wamesilimu

Sayansi na Teknolojia 
[Kuiweka Modem kwenye Kompyuta] 
 
Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Mlo wa Daku] 
 
Tangazo 
New Book: The untold story of the Muslim struggle against British Colonialism in Tanganyika. 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita