AN-NUUR 
Na.180 Shaaban 28 - Ramadhan 1419, Desemba 18 - 24, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Habari
 

UWAWARU yaleta nusura Ikwiriri

KUINGIA kwa UWAWARU imekuwa ni changamoto kubwa kwa Waislamu wa Ikwiriri ambapo wamelazimika kuimarisha madrasa zao na kuanzisha shule za watoto wadogo ili kuepuka kubatizwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikwiriri Waislamu hao wamekuwa wakiagiza na kutembelewa na wanaharakati mbalimbali kutoka Kibiti na Dar es Salaam, jambo ambalo limefufua darsa zilizokuwa zimekufa.

Awali ilidaiwa kwamba baada ya kuingia UWAWARU watoto wengi wa Kiislamu walipelekwa kusoma katika shule za awali za Wakristo ambapo walipewa kila vishawishi kutolewa katika Uislamu.

Imedaidwa kwamba huko darasani watoto hao walikuwa wakipewa makasha (boxes) moja lenye jina la Muhammad na lingine Yesu.

La Yesu lilikuwa na zawadi nzuri ikiwa ni pamoja na pipi na biskuti wakati lile la Muhammad lilijazwa vitu vyenye kutoa harufu mbaya ya uvundo.

Aidha, ilidaiwa kwamba watoto waliosema wanampenda Muhammad walielekezwa wafungue box lake ambapo walikutana na uvundo wakati wale waliosema wanampenda Yesu walikutana na zawadi nzuri.

Kufuatia changamoto hiyo, Waislamu wa Ikwiriri wamezindukana toka usingizini na wameanzisha shule ya watoto wadogo.

Hatua hiyo imeleta ukombozi kwani watoto wote waliokuwa wa chekechea za Kanisa wamerudi kusoma katika chekechea hiyo ya Waislamu.



Tamko la Masjid NNUUR juu ya kuanzishwa kwa UWAWARU
 

SISI Waislamu wa Masjid Nnuur na Utete kwa ujumla tumesikitishwa na kitendo cha Waislamu wa Ikwiriri kuanzisha umoja wa Waislamu na Wakristo Rufiji (UWAWARU). Tunasema kwamba hatuutambui umoja huo na tunalaani kwa shutuma kali.

Tunawataka Waislamu wote waliojiunga na umoja huo kurejea haraka kwa Mola wao. Uislamu utajengwa na Waislamu wenyewe na kamwe hautajengwa na wasiokuwa Waislamu. Waislamu wanaotegemea kuletewa maendeleo ya kidini na kidunia na Wakristo wanazidanganya nafsi zao na hatima yao watanasa kama panya anavyonasa kwenye mtego.

Lengo kuu la Wakristo kwa Waislamu ni kuwabadili Waislamu kutoka kwenye imani yao iliyo sahihi na kuwatukumbukiza kwenye ukafiri. (Rejea Qur’an 2:20) "Wala hawatakuwa radhi Wayahudi na Manaswara mpaka mfuate mila zao..."

Waislamu tuondokane na dhana ya kumpa mchawi alee watoto wetu. Wale wote waliotumbukiza watoto wao katika chekechea za Kikristo ni sawa wamewabatiza watoto wao na siku ya kiyama wataulizwa na Allah (s.w.) juu ya suala hilo.

Waislamu ndiyo waanzishili wa elimu ya chekechea duniani (madrasa). Hivyo basi chekechea za Waislamu ni Madrasa. Madrasa ina mtandao mzuri wa malezi kwa watoto na vijana kiimani na kitabia.

Waislamu wa Rufiji wa leo ni matokeo ya jihadi ya wazee wetu. Rufiji ina mchango mkubwa katika maendeleo ya dini ya Kiislamu Afrika Mashariki na Kati. Historia inashuhudia kuwa Maimamu wengi wa miji ya Zanzibar, Dar es Salaam, Moshi, Dodoma, Nairobi na Mombasa wamezaliwa Rufiji au wana asili ya Rufiji. Sisi Waislamu wa leo hatuna budi kuzienzi juhudi za wazee wetu walioleta mapinduzi ya Kiislamu hapa Afrika Mashariki kwa kuimarisha itikadi za Kiislamu kwa watoto wetu.

Mwisho tunapenda kuwakumbusha viongozi wa Kiislamu waasisi wa umoja huo kwamba kabla ya kuanzisha jambo muangalie athari zake katika Uislamu na sio kufikiria maslahi ya kidunia tu. Mkumbuke kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema katika sura ya 87 aya ya 16 na 17: "Lakini nyinyi mnapenda zaidi maisha ya dunia. Hali ya kuwa Akhera ni bora (zaidi kabisa) na yenye kudumu."

Langalanga lisitufanye tukaipotosha dini ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anatupa mitihani midogo midogo ili kutujaribu imani zetu.

Sheikh Mohammed Lisakile Kitambuli
Katibu Mkuu Masjid Nnuur, Utete


Kuanzishwa kwa UWAWARU

SISI vijana wa Kiislamu wa Masjid Nnuur - Utete, tumezipokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kuanzishwa kwa ushirikiano wa kiimani kati ya Waislamu na Wakristo wa Rufiji (Ikwiriri).

Kwa pamoja tunatamka kwamba umoja huo hatuutambui na wala hautuhusu sisi Waislamu wa Utete. Na pia tunaushutumu vikali muungano huo. Muislamu ndugu yake ni Muislamu mwenzake, hali kadhalika Waislamu wanafungamanishwa kiimani na Waislamu wenzao na wala si watu wa imani nje na Uislamu. Waislamu hatuna chuki na Wakristo bali tunahesabu kama ni jirani zetu na tutashirikiana nao katika nyanja zisizokuwa za kiimani, kama alivyotufundisha Mtume wetu (s.a.w.).

Rufiji kama ilivyo maeneo mengine ya mwambao wa Tanzania, wakazi wake wengi ni Waislamu. Yapata asilimia 99.9 ya wakati wa Rufiji ni Waislamu. Desturi za wananchi wa Rufiji zina asili ya Uislamu. Kwa hiyo sisi Warufiji kamwe hatukubali utamaduni wetu uathiriwe na imani ya Kikristo.

Mwisho tunawataka Waislamu wa Ikwiriri kuupinga UWAWARU kwani ni umoja usioridhiwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Allah anatutadharisha tusiwe na mafungamano au ushirikiano na Wakristo. Katika sura ya 2 aya ya 120 Mwenyezi Mungu (s.w.) anasema: "Wala hawatakuwa radhi Wayahudi na Manaswara mpaka mfuate mila zao...".

Mwenyezi Mungu anatuonya tena kwa kusema: "Enyi mlioamini! Msiwafanye Wayahudi na Manaswara kuwa wapenzi wenu (rafiki zenu) kwani watawarudisheni kwenye ukafiri wenu wa zamani ...". Wakristo siku zote wanataka tufuate mila zao. Ndiyo maana watoto wetu wa kike wanatembea nusu uchi, n.k.

Tunawataka Masheikh na Waislamu waliojiunga na umoja huo kumuomba radhi Mwenyezi Mungu na kuwaomba radhi Waislamu wenzao kwa kuwaundia taasisi wasiyokuwa na radhi nayo, taasisi inayoashiria kuwaangamiza!

Hamza Mohammed Mngage,
Katibu Mkuu
Umoja wa Vijana wa Kiislamu Kamati ya Tarbia Malezi na Taaluma,
Masjid Nnuur - Utete, Rufiji
 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 

Tahariri
Umaskini unachafua mazingira!

Mauaji ya Mwembechai: Spika wa Bunge aombwa atoe gharama za kuunda Tume

UWAWARU yafa Rufiji

UN yaidhinisha udhalimu wa Marekani

Qur’an yachomwa moto Shinyanga

Marekani yadhihirisha Ubeberu wake

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: SEXUAL SADISM
Na. Abu Halima Sachangwa

Kitengo cha Zaka chazinduliwa Dar

Tume ya Jiji kubomoa Msikiti wa vipofu

Akheri ya zamani
Na Alhaj Yusuf Kalala, Washington DC. USA

UWAWARU yaleta nusura Ikwiriri

Tamko la Masjid NNUUR juu ya kuanzishwa kwa UWAWARU

Kuanzishwa kwa UWAWARU

Wasomi Waislamu wawajibike
Na Mwandishi Wetu

Albucasis  936 - 1013 (CE)

Ijue Uhuru madrasa - Morogoro

Madrasa Akhlaqil Islamiya yapiga hatua

MADRASATUL Husseiniyi Shadhily
Na Jamillah Nassoro
 
Hatimaye kesi ya kushambulia kituo nayo yafutwa

Changieni vyombo vya mihadhara - Sheikh Said

Misikiti yakosa maji ya kutawadhia

Bakwata Tanga haifuati katiba yake

Sheikh Mbukuzi ataka Waislamu watafute radhi za Allah

Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? - 3
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache - 3
Na Yasin Valerian Massawe

Sheikh Omar Bashir afikishwa mahakamani

Mufti pekee kuidhinisha watu kufunga

Nguruwe wanaofugwa maeneo wanayoishi watu kusababisha magonjwa ya kuambikiza

200 wamesilimu

Sayansi na Teknolojia 
[Kuiweka Modem kwenye Kompyuta] 
 
Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Mlo wa Daku] 
 
Tangazo 
New Book: The untold story of the Muslim struggle against British Colonialism in Tanganyika. 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita