|
|
|
NIKIWA Mwinjilisti katika Kanisa la Waadventista wa Sabato, mara
nyingi sana nimekumbana na swali hili, tena kwa watu mbalimbali, kwa nafasi
hii naitumia kutoa majibu ya swali hili kwa kirefu. Tafadhali nifuatilie
kwa makini katika sehemu hii ya pili ya majibu yangu. Swali hili limekuwa
kubwa kwa watu mbalimbali, hata limegawa watu katika makundi mawili, wanaokubali
na kushika amri za Mungu. Na wanaokataa kwamba sasa hauna amri, ziliishia
msalabani tena amri zilikuwa za Musa na wana wa Israeli. Kwa makala hii
fuatana ili kupata hatima ya swali hili. Kwanza kabisa kwa msomaji ama
kwa mwenye swali hili apendaye kupata jibu sahihi yampasa amfahamu kwanza
huyo Mungu anayemwabudu kwamba ni Mungu yupi katika sehemu hii ya ya tatu
na ya mwisho.
Haja ya kushika sheria. Je huku kuokolewa kwa neema ni nini? Neema ama rehema ni upendeleo wa bure unaotolewa bila sharti lolote. Na ndipo tunapozungumzia suala la kuokoka yatupasa kuzungumza katika awamu tatu. Awamu ya kwanza ni wokovu kwa ulimwengu wote, yaani wanadamu walipofanya dhambi, Mungu alitayarisha mpango wa wokovu kwa wote kupitia katika Yesu. Na kifo chake pale msalabani kilihitimisha mpango huo. Na kila mmoja wetu duniani akawa ameokolewa na kufanywa mlokole! Hapo ndipo tulipookolewa kwa neema Tito 2:11 "Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa". Awamu ya pili ni pale mmoja wetu duniani anapomkiri na kumpokea Bwana wetu Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wake. Hapo ndipo anaokoka na kuanza safari ya wokovu. Na safari hii huhesabiwa mwishoni jinsi unavyomaliza. Wengi walianza vizuri, wakamaliza vibaya, hivyo wokovu na kuokoka kwao kukawa si chochote si lolote, kama akina Yuda, na wengi wetu leo. Awamu ya tatu na ya mwisho ni hapo atakaporudi mara ya pili Bwana Yesu akukute umelala - mauti ama uhai ukiendelea kuchuchumilia wokovu kwa kuwa na tabia yake ya utakatifu na upendo hapo utaokolewa na kuokoka milele. Mathayo 24:13 "Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka". Hivyo neema ama rehema haitupi hati yoyote ya kuvunja sheria ama kukataa amri, Tito 2:11-12. Maandiko yanazidi kutusisitiza kuheshimu utakatifu wa Mungu kwa kushika sheria zake. Mhubiri 12:13 "Hii ndiyo jumla ya maneno yote yamekwisha sikiwa, mche Mungu nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu".Jumla ya mtu ni kumwabudu na kushika amri zake, na siyo kumwabudu tu. Tena ni kumwabudu kwa kushika amri zote bile marekebisho wala ukarabati. Na tukivunja moja ni sawa na tumevunja zote. Yako 2:10. Na waraka wa kwanza wa Yohana 5:3 "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake wala amri zake si nzito". Kusema kwamba tunampenda Mungu huku tunakataa amri zake, maandiko yanatutia hatiani kwamba sisi tu waongo wala hatuna kweli yoyote (1 Yohana 2:3-4) "Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake". Ndiyo maana tabia ya Walokole (watu wa Mungu) watakaonyanyuliwa na Bwana imetajwa katika Ufunuo 14:12 "Hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao wazishikao amri za Mungu, na Imani ya Yesu". Huo ndio ukweli wa maandiko na jibu la swali letu. Amina. Mtu yeyote aliyesoma yaani anayefahamu mambo hata kama hana dini, hata kama ni Mkristo, lakini anafahamu kuwa Nabii wa Mwisho ni Muhammad. Asiyejua aulize na akitaka atafahamu jinsi Nabii Muhammad alivyotajwa Jina, Heshima yake, Atatokea (upande gani), Atakavyoangamiza sanamu, Atakavyomuondolea Yesu maoni ya uongo, Atakavyonena mambo mazito n.k. Yeyote awe msomi (anayejiona msomi) awe hakusoma, na mwingine awaye yote anayedhani au mwenye hoja kwamba Muhammad si Nabii wa Mwenyezi Mungu, Jawabu ni kwamba "Hajui". Ni nani awezaye kufasiri maandiko (unabii) kama hamjui Mungu? Ni nani mpumbavu kuliko au mjinga kuliko yule aambiwaye kisha badala ya kusikiliza anafunga masikio ili asisikie? Masikio ulipewa ya nini? Hakuna kitu chochote alichosema Yesu Muhammad akapinga wala alichosema Muhammad ambacho Yesu anapinga isipokuwa juu ya Yesu ni sahihi kama Yesu mwenyewe alivyotabiri kwa kusema "...Ataniondolea mimi maoni yote ya uongo...". Kama ni kusoma dini wamesoma wengi, kama ni imani wanayo wengi, lakini waelewa si wengi. Nini maana ya kuelewa? Kuelewa au kujua maana yake ni kuweza kutofautisha ukweli na uongo na ukafuata ukweli. Na iwapo unaujua ukweli lakini hutaki kuufuata maana yake ni kwamba huelewi au bado hujajua vile vile kwa sababu ungejua ungefuata. Hakuna mtu yeyote ambaye anajua kwamba Agano la milele kati ya Mwenyezi Mungu, Ibrahim na mwanawe lilikuwa kwa Ishmael, halafu akaacha kufuata na kutangaza Uislamu. Hakuna mtu yeyote anayejua kuwa Nabii wa mwisho ni Muhammad (s.a.w.) halafu akamkanusha. Kwa hiyo wasiokuwa na dini na Wakristo wote waliosoma na wasio soma hawajui wanachokiabudu. (Maarifa yao yamefichwa). Jina la Muhammad (s.a.w.) lilipaswa liwepo katika Torati na Injili lakini jina hilo hivi sasa halipo. Wako wajuao hivyo na wasiojua lakini wote wanabeba Biblia wanaongozana kwenda makanisani. Lakini Yesu alionya mengi: Mathayo 15:13-14: - "... Kila pando alilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa. Waacheni hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili". Hata hivyo wengi wanajipa moyo kwa kusema "Kama ni makosa hatukuyaanzisha sisi, na vile vile tunatenda mema na kutii amri za Mungu hivyo tuna matumaini mema...". Maneno haya ndiyo kutokuelewa hasa! Kumbuka Yesu kasema nini katika Marko 12:28-34 na uangalie kanuni ya imani (shahada) ya dini yako inasemaje! Maneno ya Yesu katika Marko 12:24-34 na Mathayo 7:24-27 ni mapana na magumu sana na nikisema niyafafanue kwa kuyatolea mifano itakuwa ni kazi ndefu kwa sababu Wakristo wamepoteza ule "moyo" wa mafundisho ya manabii. Sasa iwapo moyo wa kitu haupo, hicho kitu kitakuwa hai? Haiwezekani kiwe hai. "Samaki mmoja akioza ..." Yeremia 32:12 "Wewe urehemuye watu elfu nyingi, uwalipaye baba za watu ouvu wao vifuani mwa watoto wao baada yao, Mungu aliye mkuu, aliye hodari, BWANA wa Majeshi ndilo jina lake". Ewe Mkristo ni kipi kikudanganyacho! Elewa kuwa Mwenyezi Mungu si Yesu wala Yesu si Mungu, bali Yesu ameumbwa na Mungu wa Ibrahim na Uislamu ndiyo mila ya Baba yetu Ibrahim. Uislamu ndiyo dini ya Mitume wote ambayo imekamilishwa na Nabii Muhammad (s.a.w.). Watu wanabishana majukwaani kwa yasiyo na sababu na muda unakatika kama moto unavyokula majani makavu porini. Mauti yatosha kuwa mawaidha Unaonaje kuukataa Unabii wa Muhammad (s.a.w) naye ndiye wa mwisho? Unaonaje kuutetea uongozi wake naye alitumwa na Mungu? Ukikataa kufuata mwongozo wa Muhammad, basi umeshika nini? Una akili gani? Una werevu gani? Unategemea nini? Utajua nini? Iwapo Mwenyezi Mungu ametuumba kwa lengo tu la kumwabudu, basi ni vipi unafuata dini bila makini? Jambo la kheri halipatikani kwa urahisi, hivyo kuelewa usahihi wa dini kunahitaji uangalifu mkubwa kabisa. Mwenyezi Mungu haabudiwi ili mradi tu! Ndiyo maana Wakristo kuisusa Torati kumewapoteza njia na hawajui tofauti kati ya moja (1) na tatu (3) au ufafanuzi wa amri kuu ya Mungu, wala hawaelewi maana ya ubatizo. Ubatizo maana yake ni ushuhuda au ni mfano wa kadi ya kuingilia harusini. Hivyo mtu anapokufa ni lazima awe na kadi hiyo ambayo inatakiwa iwe na anwani sahihi. Sasa je, kadi yako ni ipi? Umejiandaa vipi? Ubatizo wa Wayahudi ulikuwa ni wa kutoswa majini yaani kitendo hicho kinathibitisha kwamba aliyehusika amemkiri BWANA na Nabii anyehusika (aliyepo wakati huo). Ubatizo wa mwisho wa yule abatizaye kwa Roho Mtakatifu ni huu ambao leo unaitwa "kusilimu" yaani kumkiri Mwenyezi Mungu (kama walivyofundisha Manabii wote ya kuwa hana mshirika - Ni mpekee) na kumkiri Muhammad kuwa ni Nabii wake (wa mwisho). Hili ndilo agano ambalo Mwenyezi Mungu alimpa Ibrahim kuhusu kuwabarikia mataifa ili atakayemfuata Muhammad (s.a.w.) asipotee. Nakumbusha tena kwamba wamesoma wengi, wanasali wengi, lakini ni wangapi wajuao siri hii? Biblia imejaa habari za ufunuo kutokea Uarabuni (Hijaz, Parani ..) alikoishi Ishmael, lakini ni wangapi waonao? Qur’an imejaa maneno ya kutetemesha kila kitu, lakini ni wangapi waonao? Qur’an inatoboa siri ya wanavyuoni wa Kiyahudi na Wakristo juu ya kuficha habari za Nabii Muhammad (s.a.w.), lakini ni wangapi waonao? Ukichunguza kila linalotajwa katika Qur’an utakuta ni la kweli, lakini ni wangapi waonao? Imekwishaandikwa ya kwamba wanaotaka dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwao, lakini ni wangapi waonao? Imetahadharishwa ya kwamba Yesu atawakana wanaomtumainia na kwamba usimwombe yeyote (usifanye sala kwa yeyote) isipokuwa Mwenyezi Mungu tu, lakini ni wangapi waonao? Imeandikwa ya kwamba walioficha maneno ya Mwenyezi Mungu na hali yamekwishawadhihirikia kuwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na wanazidi kuyaficha ili wawapoteze watu nanjia ya haki wamekwisha kulaaniwa, lakini ni wangapi waonao? Mwenyezi Mungu kasema: "Nijueni ndipo mniabudu" na hamwongozi mtu asiyetaka kuongozwa, lakini ni wangapi waonao? Mwenyezi Mungu kasema ameuumba moto katika mti mbichi na huo ni katika balaa kubwa alizoumba na kwamba tumkiri yeye kuwa ni Mungu wa haki asiye na mwana wala mshirika yeyote na tunakiri Manabii wake wote na kutii vilivyo amri zake, lakini ni wangapi waonao? Yaliyoandikwa katika Qur’an juu ya Yesu ndiyo ya kweli kabisa, lakini
ni wangapi waonao? Imeandikwa ya kwamba waliojitenga na Qur’an Takatifu
(uongozi ulioachwa na Nabii Muhammad) siku ya kiama amali (wema na) zao
zitaruka patupu kama jivu lililopeperushwa na upepo mkali, lakini ni wangapi
waonao?
|
YALIYOMO
Tahariri Umaskini unachafua mazingira! Mauaji ya Mwembechai: Spika wa Bunge aombwa atoe gharama za kuunda Tume UN yaidhinisha udhalimu wa Marekani Qur’an yachomwa moto Shinyanga Marekani yadhihirisha Ubeberu wake MARADHI
YA KISAIKOLOJIA: SEXUAL SADISM
Kitengo cha Zaka chazinduliwa Dar Tume ya Jiji kubomoa Msikiti wa vipofu Akheri ya
zamani
UWAWARU yaleta nusura Ikwiriri Tamko la Masjid NNUUR juu ya kuanzishwa kwa UWAWARU Wasomi
Waislamu wawajibike
Madrasa Akhlaqil Islamiya yapiga hatua MADRASATUL
Husseiniyi Shadhily
Changieni vyombo vya mihadhara - Sheikh Said Misikiti yakosa maji ya kutawadhia Bakwata Tanga haifuati katiba yake Sheikh Mbukuzi ataka Waislamu watafute radhi za Allah Je,
hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? - 3
Njia
ya uzimani ni nyembamba, waionao ni wachache - 3
Sheikh Omar Bashir afikishwa mahakamani Mufti pekee kuidhinisha watu kufunga Nguruwe wanaofugwa maeneo wanayoishi watu kusababisha magonjwa ya kuambikiza Sayansi
na Teknolojia
Chakula
na lishe
|