AN-NUUR 
Na.180 Shaaban 28 - Ramadhan 1419, Desemba 18 - 24, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Kitengo cha Zaka chazinduliwa Dar 

KITENGO cha Zakat na Sadaqa kinachojulikana kama The Dar es Salaam Yemen Community for Charity & Culture (D.Y.C.C.C) Jumapili ya Desemba 13, mwaka huu kilizinduliwa rasmi katika ukumbi wa Starlight Jijini. 

Katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa mfuko huo wa Zakat na Sadaqa Sheikh Saidi A. Abri alitoa taarifa fupi kuhusiana na kitengo chake na kusema tatizo kubwa linaloikabika jumuiya yake ni uchache wa watoaji wa zakati na sadaqa wakati ambapo wanaohitaji kupewa ni wengi. 

Amewahimiza Waislamu kulipa suala hili uzito unaostahiki kwani ni miongoni mwa nguzo za Uislamu na imepewa msisitizo mkubwa katika Qur’an. 

Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mhe. Iddi Simba Waziri wa Viwanda na Biashara katika nasaha zake kwa Waislamu waliohudhuria uzinduzi huo akiwataka Waislamu kutekeleza nguzo ya Zakat ili kuweza kusaidia katika mambo mbalimbali. 

Zawadi mbalimbali zilitolewa katika uzinduzi huo ambazo zilikabidhiwa kwa baadhi ya wahitaji. 

Akitoa nasaha zake Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Hashim Saggaf katika nasaha zake aliwataka wale wote waliopewa zawadi kuzitumia vizuri na kuwataka wale wenye uwezo wajijengee utamaduni wa kutoa misaada kwa ndugu zao wasiokuwa na uwezo. 



Tume ya Jiji kubomoa Msikiti wa vipofu 
 
  • Wasioona waomba msaada Bakwata
  • Upo shule ya Uhuru
CHAMA cha Waislamu wasioona Tanzania kimeelezea wasiwasi wao kuhusu azma ya Tume ya Jiji kubomoa sehemu ya kuswalia watoto wasioona katika shule ya Uhuru Mchanganyiko. 

Kwa mujibu wa barua iliyoandikiwa Bakwata kuiomba iingilie kati suala hili; kabla ya kuingia kwa Tume ya Jiji watoto hao wasioona walipewa jengo moja walitumie kama Msikiti. 

Jengo hilo lilitumika hadi kufikia Mh. Keenja kuwa Bwana Mkubwa wa Jiji, imesema sehemu ya barua hiyo. 

Ambapo barua hiyo inadai kwamba yeye Mh. Keenja ameona hakuna umuhimu wowote jengo hilo kutumiwa na watoto hao vipofu kumuabudia Mola wao na hivyo yako mbioni kuligeuza litumike kwa shughuli nyingine. 

Barua hiyo No. TABMO/RE/66 ya Desemba 13 iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake Bw. Amiri A.S. Andanenga imemuomba Katibu Mtendaji wa Bakwata afanye hima kuwaokolea wanafunzi Waislamu wasioona sehemu yao muhimu kwa ibada kabla hawajaangukiwa na nyundo ya Tume ya Jiji. 

Juhudi za kumpata Bw. Keenja ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Jiji kuzungumzia suala hili hadi tunakwenda mitamboni hazikuweza kufanikiwa. 

Waislamu wasioona nchini wameunda umoja wao ambao hujulikana kwa jina la "Tanzania Blind Muslims Organisation" (TABMO) na moja ya shughuli zao ni kuwasaidia watoto wasioona walio mashuleni katika jumla ya kuwarahisishia kujua Uislamu wao na kuwajengea mazingira ya kuutekeleza. 

Makao Makuu ya Chama hicho yapo Dar es Salaam yakitumia anuwani P.O. Box 90228. Kwa sasa Katibu Mkuu wake ni Mzee Amiri A.S. Andanenga. 

 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri
Umaskini unachafua mazingira!

Mauaji ya Mwembechai: Spika wa Bunge aombwa atoe gharama za kuunda Tume

UWAWARU yafa Rufiji

UN yaidhinisha udhalimu wa Marekani

Qur’an yachomwa moto Shinyanga

Marekani yadhihirisha Ubeberu wake

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: SEXUAL SADISM
Na. Abu Halima Sachangwa

Kitengo cha Zaka chazinduliwa Dar

Tume ya Jiji kubomoa Msikiti wa vipofu

Akheri ya zamani
Na Alhaj Yusuf Kalala, Washington DC. USA

UWAWARU yaleta nusura Ikwiriri

Tamko la Masjid NNUUR juu ya kuanzishwa kwa UWAWARU

Kuanzishwa kwa UWAWARU

Wasomi Waislamu wawajibike
Na Mwandishi Wetu

Albucasis  936 - 1013 (CE)

Ijue Uhuru madrasa - Morogoro

Madrasa Akhlaqil Islamiya yapiga hatua

MADRASATUL Husseiniyi Shadhily
Na Jamillah Nassoro
 
Hatimaye kesi ya kushambulia kituo nayo yafutwa

Changieni vyombo vya mihadhara - Sheikh Said

Misikiti yakosa maji ya kutawadhia

Bakwata Tanga haifuati katiba yake

Sheikh Mbukuzi ataka Waislamu watafute radhi za Allah

Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? - 3
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache - 3
Na Yasin Valerian Massawe

Sheikh Omar Bashir afikishwa mahakamani

Mufti pekee kuidhinisha watu kufunga

Nguruwe wanaofugwa maeneo wanayoishi watu kusababisha magonjwa ya kuambikiza

200 wamesilimu

Sayansi na Teknolojia 
[Kuiweka Modem kwenye Kompyuta] 
 
Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Mlo wa Daku] 
 
Tangazo 
New Book: The untold story of the Muslim struggle against British Colonialism in Tanganyika. 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita