|
|
|
ABDUL Qasim Al Zahrawi (Albucasis) alikuwa bila shaka yeyote ni Daktari mwenye taaluma kubwa ya (surgery) upasuaji wakati wa zama za kati yaani ‘medieval period’. Yeye ameweza kugundua aina mbalimbali ya tiba na njia za upasuaji na teknolojia ya kutengeneza na kubuni vyombo vya upasuaji (surgical instruments) ambavyo vinakisiwa kutimia mia mbili hivi. Alikamilisha Encyclopaedia ya matibabu na upasuaji ambayo hadi leo imetia fora isiyo kifani katika historia ya fani ya ya surgery na kuweza kutambulikana kama ‘The Father of modern surgery’ yaani baba wa fani ya upasuaji wa kisasa. Elimu yake hiyo aliipata katika mji wa Qurtuba, ambao ulikuwa ni mji mkuu wa Ukhalifa wa Kiislamu wa Spain na kujiendeleza katika Chuo cha Utabibu kilichokuwepo katika Falme ya Kiislamu iliyopo Baghdad, mji mkuu wa Iraq. Aliwahi kupata wadhifa wa Daktari wa Mfalme Al Hakam II wa Spain. Katika uhai wake mji wa Qurtuba ulikuwa ni maarufu sana kwa upokeaji Rufaa za upasuaji kutoka Ulaya na Asia. Katika kitabu cha ‘History of Arab Medicine’ kilichoandikwa na Dk. Campbell alitaja ‘Al Zahrawi’s principles of medical services surpassed those of Galen in the European medical curriculum’ yaani misingi ya sayansi ya utatibu Al Zahrawi yamevuka kikubwa sana mitaala ya fani hiyo ya Galen katika utabibu wa Ulaya. Encyclopaedia inayosifika zaidi ni ile ya Juzuu thelathini inayoitwa Al- Tasrif Li man ajaz an-il-talif ‘yaani kitabu kinachomwezesha asieweza kusoma vitabu vikubwa kuelewa taaluma’ ambayo imefafanua elimu ya upasuaji, zana za upasuaji na michoro ya kueleza namna ya upasuaji wa maumbile ya ndani ya mwili "Anatomy". Taaluma hii ya Udaktari ilizama zaidi katika fani za matibabu ya macho, masikio, koo, uzazi, utoaji wa mawe katika kibofu cha mkojo na upasuaji katika sehemu za mifupa na viungo. Yeye alikuwa ni wa mwanzo kutumia nyuzi za hariri katika ushonaji unaoutumika baada ya upasuaji. Katika fani ya utabibu wa meno "Dentistry" alianzisha uwekaji meno bandia na kusahihisha fizi zilizokaa upande. Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha za Latin, Kiingereza, Kifaransa na Kihibrania. Mmoja kati ya Daktari mashuhuri wa Kifaransa aitwaye Guy de Chaulic (1300 - 1368) alinakili: ufundishaji wa Al Zahrawi katika kitabu chake cha upasuaji. Hapa vilifatia vitabu vingi ambavyo vilichapishwa Venice (1541) Basel (1541) na Oxford (1778) ambavyo vimenakili na kufafanua mafundisho ya Al Zahrawi. Mafundisho haya yamedumu hadi katika karne hii na kutoa ufafanuzi unaondeleza taaluma hii ya surgery. |
YALIYOMO
Tahariri Umaskini unachafua mazingira! Mauaji ya Mwembechai: Spika wa Bunge aombwa atoe gharama za kuunda Tume UN yaidhinisha udhalimu wa Marekani Qur’an yachomwa moto Shinyanga Marekani yadhihirisha Ubeberu wake MARADHI
YA KISAIKOLOJIA: SEXUAL SADISM
Kitengo cha Zaka chazinduliwa Dar Tume ya Jiji kubomoa Msikiti wa vipofu Akheri ya
zamani
UWAWARU yaleta nusura Ikwiriri Tamko la Masjid NNUUR juu ya kuanzishwa kwa UWAWARU Wasomi
Waislamu wawajibike
Madrasa Akhlaqil Islamiya yapiga hatua MADRASATUL
Husseiniyi Shadhily
Changieni vyombo vya mihadhara - Sheikh Said Misikiti yakosa maji ya kutawadhia Bakwata Tanga haifuati katiba yake Sheikh Mbukuzi ataka Waislamu watafute radhi za Allah Je,
hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? - 3
Njia
ya uzimani ni nyembamba, waionao ni wachache - 3
Sheikh Omar Bashir afikishwa mahakamani Mufti pekee kuidhinisha watu kufunga Nguruwe wanaofugwa maeneo wanayoishi watu kusababisha magonjwa ya kuambikiza Sayansi
na Teknolojia
Chakula
na lishe
|