NASAHA
Na. 082 Jumatano Januari 10 - 16, 2001
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
MICHEZO
 

Baadaya Mkapa kushindwa kusaidia: 
Prof. Lipumba aombwa kuiombea Tanzania FIFA 

  • Simba 'Friends',Yanga bomba wataka anusurusoka nchini 


Na Hamisi Kasabe

KUFUATIA ukimya wa Rais Benjamin Mkapa kuhusu mgogoro wa Tanzania na Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA), wapenzi wa soka nchini wameamua kumuomba Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba kuingilia kati mzozo huo.

Mkapa aliombwa hivi karibuni na Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Ramadhani Balozi kusaidia kutatua mgogoro uliopo baina ya Tanzania na FIFA kufuatia Shirikisho hilo kusimamisha uanachama wa Tanzania, lakini mpaka leo hii hajasema lolote. 

FIFA ilifikia uamuzi huo Oktoba 26 mwaka jana baada ya viongozi wa zamani wa Chama cha Soka Nchini (FAT), Mwenyekiti Muhidin Ndolanga na Katibu wake Ismail Aden Rage kuenguliwa madarakani na serikali. 

Kufuatia adhabu hiyo Tanzania imesimamishwa kushiriki michuano yoyote ya kimataifa pamoja na kutopata misaada ya fedha na kiufundi kutoka shirikisho hilo. 

Wakizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Dar es Salaam baadhi ya wapenzi na wanachama wa Klabu ya Simba, wanaojiita Simba 'friends' (Marafiki wa Simba) wamesema kwa hali ilivyo sasa anayeweza kuutatua mgogoro wa FIFA na Tanzania ni Prof. Lipumba pekee. 

Kwa mantiki hiyo wamemuomba Lipumba kupitia gazeti hili kutumia kukubalika kwake katika Jumuiya ya Kimataifa kumaliza mzozo huo ambao unatishia kuporomoa kabisa soka ya Tanzania. 

Huku wakigoma majina yao, kuandikwa gazetini kwa kuwa siyo wasemaji mahususi wa Simba 'friends; wapenzi hao wamemuomba Lipumba kulinusuru Taifa na janga hilo, bila kujali kuvurugika kwa uchaguzi mkuu uliopita ambao uliwaweka madarakani Ma-Rais Mkapa na Karume. 

NaoYanga bomba ambao wanaaminika kuwa na machungu na klabu yao kama walivyo Simba friends wameonyesha wasiwasi wao kama kweli serikali ya CCM inadhamira ya kuinua soka nchini kutokana na ukimya wake katika suala hilo. 

Kutokana na wasiwasi huo, Iddi Mipata ambaye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa Yanga bomba ameungana na Simba 'friends' kumuomba Lipumba kulishughulikia suala hilo pamoja na chama chake kuporwa ushindi. 


Mtwa aanza kulala mapema 



Na Mwandishi Wetu
 

KIUNGO na mshambuliaji nyota wa mabingwa wa soka Tanzania Yanga Mwanamtwa Kihwelu 'Daly Kimoko' sasa ameanza kulala mapema ili kupumzisha mwili kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jijiniDar es Salaam toka kwa majirani wa mchezaji huyo na kuthibitishwa na Mtwa mwenyewe hivi karibuni, amefikia uamuzi huo kwa kuwa sasa anafanya mazoezi magumu. 

Amesema anafanya hivyo ili kuhakikisha kiwango chake cha usakataji kabumbu kinapanda maradufu na hivyo kuzidi kutisha kisoka. 

Kwa sasa Mtwa ambaye anaishi Magomeni amekuwa gumzo kubwa nchini kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuzifumania nyavu za timu pinzani. 

Kufuatia umahiri huo timu kadhaa za ndani na nje ya nchi zimekuwa zikimuhitaji kwa udi na uvumba ikiwemo timu ya Scouts ya nchini Mauritius. 

Hata hivyo Mtwa ambaye amejiunga naYanga wiki chache zilizopita akitokea timu ya Simba amekataa kuikacha timu yake licha ya klabu hiyo ya Mauritius kumtumia tiketi ya ndege mara mbili. 


Salvatory aitwa Mtibwa

Na Mwandishi Wetu
 

SALVATORY Edward Augustino, kiungo hodari nchini ni miongoni mwa wachezaji 30 wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ambao wameitwa kujiunga na timu hiyo haraka.

Salvatory na mlinzi shupavu Habib Kondo wamesajiliwa na Mtibwa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa wakitokea timu inayouzwa ya Kajumulo World Soccer. 

Kulingana na taarifa iliyotolewa juzi mjini Dar es Salaam na mratibu wa timu ya Mtibwa Jamal Bayser wachezaji wote wanatakiwa kuripoti kambini mjini Turiani leo. 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

MAONI YETU
Mapinduzi Zanzibar yameleta kilichokusudiwa?

Wananchi wamwambia Mkapa:
Mbumbumbu wa demokrasia waliomo katika chama tawala ni hatari zaidi

Waislamu watakiwa kuwa watekelezaji wa maamuzi

‘Hajj Trust’ yaongeza huduma kwa mahujaji

DONDOO MUHIMU

MAKALA
Jamii ijihadhari viongozi wasaliti

MAKALA
Msimamo wa Pengo haushangazi

KALAMU YA MWANDISHI
Kitendawili cha millenia: Urais bila dola

MAKALA
Dhana ya kumwabudu Mungu anayeafiki udhalimu lazima tuikatae

MAKALA
Mapinduzi Zanzibar: Dhuluma bado ipo

MAKALA
CCM haiwezi kuondosha umasikini Tanzania

MAKALA
Tirivyogo la sekta ya elimu

Mwenye Macho……
Demokrasia haiwezi kujengwa kwa kuvunja katiba

HABARI ZA KIMATAIFA

MASHAIRI

MICHEZO

  • Baadaya Mkapa kushindwa kusaidia: Prof. Lipumba aombwa kuiombea Tanzania FIFA
  • Mtwa aanza kulala mapema
  • Salvatory aitwa Mtibwa

  •    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita