|
Na. 082 Jumatano Januari 10 - 16, 2001 |
|
|
|
|
KUFUATANA na takwimu zilizotolewa na Idar ya Takwimu ya Taifa (National Bureau of Statics) kuwa idadi ya Tanzania wenye kuishi chini ya kiwango cha umasikini imeongezeka kutoka asilimia 48 mwaka 1996 mpaka kufikia 56 mwaka 2000 inaonesha wazi kwamba serikali ya CCM kamwe haiwezi kuondosha umaskini katika nchi hii na badala yake ni kuzidi kuididimiza. Pamoja na kuwa serikali ya Rais Mkapa iliunda kitengo maalum cha kupambana na hatimaye kuutokomeza umasikini kilicho chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, tija ya kitengo hicho imekuwa ni kuongezeka kwa umasikini katika kipindi ambacho serikali hiyo ya Rais Mkapa imekuwepo madarakani. Lakini ifahamike kuwa, kuuondoa umaskini katika jamii hakupimwi kwa kuangaliwa ni idadi gani ya watu umewapa shilingi elfu kumi kumi za miradi ya kuuza magenge au laki laki za miradi ya useremala au miradi mingine yeyote la! Mipango ya kuondoa umaskini huangaliwa kwa kutizama ni kwa kiwango gani umeweza kuongeza ajira katika sekta iliyo rasmi. Pamoja nan kwamba mimi sijakaa darasani nikafundishwa uchumi, lakini kwa akili ya kawaida tu ya mtu mwenye kutafakari na kuwa na mawazo huru, ni ukweli uliowazi kwamba haiwezekani kwa watu kuweza kujiajiri wenyewe, kama hakuna watu waliaoajiriwa katika sekta iliyo rasmi. Hii ni kwa sababu mahitaji mbalimbali ya watu wenye ajira rasmi, ndio hukuza ajira katika sekta isiyo rasmi, sekta binafsi kwa kununua bidhaa au huduma inayotolewa na sekta hiyo. Kwa hivyo basi, ni wazi kwamba kuwapigia kelele wananchi kunakofanywwa na uongozi wa CCM kwamba wananchi wajiajiri wenyewe, bila ya serikali yake kufanya juhudi za kuongeza ajira katika sekta rasmi, ni utapeli wa kisiasa. Kwa hali ilivyo sasa kupungua kwa ajira siku hadi siku na uwezo wa sekta isiyo rasmi kukua nao pia unatoweka. Mtu ataweza kuanzisha biashara ya kuchonga na kuuza vitanda au viti ikiwa wanunuzi hawapo? Mifano ipo mingi lakini hebu na tuangalia ufuatao ambao ni rahisi wa mradi wa chakula. Kuna sehemu, kazi kubwa ya ujenzi inafanyika, hapo utakuta mama lishe (Mama Ntilie) nao wamekwisha fika na wanauza chakula. Wale hawahitaji uwapigie kelele kwamba 'jamaniee nendeni kule mkauze chakula ili mjiajiri. Ninachotaka kukionesha hapa ni kuwa kelele zote zilizokuwa zikipigwa na viongozi wa serikali kuwa wanapambana na umaskini, kama nilivyotarajia zimeanguka patupu kwani aidha hawakuzingatia ukweli au wameshindwa kushauriwa kwa ajili ya kiburi.Kiburi kwasababu ndani ya CCM kuna watalaamu waliobobea katika masuala ya uchumi je wameshindwa kutoa ushauri? Kwamba kupambana kwa kikweli kweli na umasikini kuongeza ajira na wala sio kutoa mikopo ya biashara ndogo ndogo? Tukiachana na hilo la ofisi ya Makamu wa Rais na kitengo chake cha kupambana na umasikini tuangalie hali halisi ya Watanzania kiumasikini huo. Chukua mfano wa jiji la Dar es Salaam ambalo wakaazi wake zaidi ya asilimia 80 wanaishi katika maeneo ambayo hayakupimwa viwanja kwa ajili ya makazi ya watu. Miongoni mwa hawa kwa mujibu wa utafiti wangu binafsi asilimia zaidi ya 70 wanaishi katika vijumba vibovu (slums). Kama unataka kuthibitisha nenda Keko, Magomeni mabondeni, Mchikichini mabondeni, Tandika, Mbagala na kwingi kwingineko, kundi hili pamoja na wale wenye kukaa katika nyumba maarufu kwa jina la National Housing ambazo ziliuziwa wananchi kwa mikopo huko nyuma ambap zipo Magomeni, Temeke, Kinondoni na Tandika wanaishi maisha ambayo ni ya kienyeji zaidi (taditional life style) sawa na yale ya kijijini. Ukiweza kuwabadili watu hawa kutoka kwenye kutumia vibatali mpaka umeme, kutoka jiko la kuni mpaka mkaa, mafuta au umeme, kutoka chumba kimoja kuishi Baba, mama na watoto mpaka watoto wa kike na chumba chao na wa kiume na chumba chao. Kuwawezesha angalau kuepukana na magonjwa ya kipindupindu, kuhara na kuhara damu ambayo hi magonjwa yatokanayo na uchafu, hapo utakuwa umewafanya watu hao au jamii hiyo ya Watanzania kuwa wameendelea na watakuwa wameondokana na umasikini. Lakini ili kufikia hatua hiyo yatakiwa mtu huyo awe na shughuli halali (ajira) ambayo itamfanya ale yeye na familia yake, aitibie familia yake na abakiwe na ziada atakayoitumia kufanya hayo mabadiliko ya msingi, kama kujenga nyumba, kuweka umeme, kununua jiko la mafuta n.k. Sasa kufikiria kuwa umasikini unaondolewa kwa
kutoa mikopo midogo midogo huku ikiwapotezea ajira wananchi wake kwa mamia
kila mwaka ndio maana nikasema mwenzoni kabisa kwamba CCM hawawezi kuondoa
umaskini katika nchi hii na badala yake wataongeza na kufanya ushamiri
kama walivyofanya katika kipindi kilichopita cha miaka mitano.
|
YALIYOMO
MAONI
YETU
Wananchi
wamwambia Mkapa:
Waislamu watakiwa kuwa watekelezaji wa maamuzi ‘Hajj Trust’ yaongeza huduma kwa mahujaji MAKALA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
Mwenye Macho……
|
|
|
|
|