|
Na. 082 Jumatano Januari 10 - 16, 2001 |
|
|
|
|
|
Msimamo wa Pengo haushangazi Na Rajab Kanyama Wiki moja kabla ya uchaguzi Mkuu, askofu Pengo aliwanasihi viongozi wa Chama cha Mapinduzi na serikali yake kwamba, ni vema wakakubali matokeo ya uchaguzi kwa vyovyote yatakavyokuwa. Katika kusherehesha kauli hiyo akasema, ni dhana potofu kuamini kwamba ni lazima chama tawala kishinde katika kila uchaguzi unaofanyika nchini. Cha kushangaza sasa, ni hizi kauli zake mpya alizozitoa siku ya mkesha wa Krismasi za kuwataka wananchi wa Tanzania kuyakubali matokeo ya uchaguzi mkuu , uliofanyika Oktoba 2000, bila ya kujali kwamba uchaguzi huo ulijaa hila na udhalimu wa kupindukia. Hata hivyo, wanaofahamu hawakushangazwa, hasa kwa vile vile historia inaonyesha kwamba kuanzia karne za kati (Middle Ages) huko viongozi wa kanisa Katoliki wakishirikiana na watawala mbali mbali, wamekuwa wakihusika kikamilifu katika vitendo vya ukandamizaji dhidi ya wananchi na wakati mwingine kufanya mauaji hasa dhidi ya watu wanaopingana na misimamo ya kanisa au maslahi yake. Wakati huo, ufisadi uliosababishwa na Mapapa ulishamiri mno katika kanisa Katoliki mpaka wananchi wengi wakaamka na kupinga madai ya uongo na haramu ya Mapapa. Watu hao wakaitwa "wapinga mafunzo halali." (heretics) ambao waliteswa vibaya na kanisa Katoliki la Roma. Moja ya nyaraka zilizoamuru mateso hayo ni ule waraka wa kinyama wa "Ad exstirpanda: uliotolewa na Papa Innocent IV mnamo mwaka 1252 ambao uliamuru kwamba "wapinga imani iliyokubalika (heretics) wapondwe na kusagwa kama nyoka wenye sumu kali." Waraka huu uliendelea kutiliwa nguvu na Papa Alexander IV (1254-61), Papa Clement IV (1265-68), Nicholas IV (1288-92), Bonifa VIII (1294-1303) rejea "The Catholic Encyclopedia, Vol. 8, Uk. 34. Galileo Galilei ni mwanasayansi mkubwa wa karne hizo, aliyeuawa kinyama kwa hukumu ya Inquisition ya Kanisa Katoliki kwa kosa la kufundisha watu kwamba dunia ni mfano wa yai, badala ya kuwa tambarare kama ilivyokuwa inafundishwa na viongozi wa kanisa Katoliki. Huyu ni mwanasayansi mmoja tu tuliyemtaja, kati ya wengi waliouawa na kanisa Katoliki kwa kufundisha tofauti na mafundisho ya kanisa. Kanisa halikuwa likifanya mauaji ya watu mmoja mmoja peke yake, lakini historia inaonyesha pia kwamba kanisa Katoliki lilihusika kikamilifu katika mauaji ya halaiki ya Wayahudi zaidi ya milioni sita, wakati wa vita vya pili vya dunia. Katika siku za hivi karibuni, kanisa Katoliki limetajwa kuhusika na mauaji ya halaiki yaliyofanywa na wauaji wa Interahamwe nchini Rwanda kwa sababu ya chuki za kikabila. Kwa ajili ya uchungu, na kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya vitendo vya kinyama vya kanisa katoliki nchini Rwanda, serikali ya nchi hiyo imeamua kuacha mafuruna mifupa ya watu waliouawa ndani ya kanisa ili iwe kumbukumbu ya kudumu kwa ajili ya vizazi vijavyo. Watu hao walikimbilia katika kanisa hilo wakiamini kwamba wangesalimika. Haya tuliyotaja ni miongoni mwa matokeo yaliyomfanya Papa John Paul wa sasa, kutokea hadharani mwishoni mwa mwaka jana na kuomba radhi kwa makosa ambayo kanisa Katoliki limeyafanya dhidi ya walimwengu. Japo kuwa Papa hakueleza bayana makosa hayo, lakini zipo kumbukumbu za kutosha ambazo zinataja baadhi ya maovu ya Mapapa wenzake waliomtangulia, ambayo waliyafanya dhidi ya wananchi, waumini wa kanisa lao. Katika kitabu " The story of Civilization: The Ages of Faith." Mwandishi Durant anaeleza kwamba, katika karne za kati, Ofisi za Kanisa Katoliki popote zilipokuwa, zilifanya kazi ya kuuza masalia matakatifu, kama vile sanda ya Yesu, na kazi ya kuuza misamaha ya dhambi, na kufanya kuwa biashara kubwa, iliyolikusanyia kanisa mapesa mengi. Mwaka 1300, Papa Bonifa VIII alitangaza sikukuu ya ukumbusho, Jubilei na akatoa zawadi ya misamaha ya dhambi, kwa wale ambao watakwenda kuzuru katika kanisa la mtakatifu Petro, huko Roma. Watu wengi walikwenda kuzuru, na kuweka mali nyingi. Nyingi ya pesa hizo zilitumiwa na Papa mwenyewe na ndugu zake wa ukoo wa Gaetani, ambao walinunua majumba ya ngome, na mashamba mengi huko Latium. Jambo hili liliwaudhi sana wananchi wakazi wa Roma. Mpaka kufikia wakati wa Constantino, kanisa likaendelea kuongeza utajiri wake bila kificho, mpaka kufikia hatua ya kanisa kuwa linadhibiti nchi nyingi, pamoja na maekari ya ardhi waliyonunua, na kwa hivyo wananchi waliokuwa wakiishi katika nchi za kikatoliki, walizimishwa kulipa kodi kwa kanisa, wakati mwingine - kwa hila, kupitia mikataba ya makubaliano kati ya Serikali na Kanisa. Hapa nchini, Kanisa Katoliki linamkataba maalum na Serikali unaoitwa "Memorundum of understanding", uliotiwa sahihi mwaka 1992, ambamo serikali ya Tamhuri ya Tanzania inawajibishwa kutumikia makanisa nchini kupitia kwenye ushirikiano wake wa mashrika ya dini na serikali za nchi za nje. Katika karne za nyuma huko, ni watu wachache tu ndio waliokuwa wanajua kusoma na kuandika, kwa hivyo Mapadri walihusishwa kikamilifu katika kuandika wasia za watu mbali mbali. Mwaka 1170, Papa Alexander III alitoa amri rasmi kwamba, hakuna wasia utakaokubalika kuwa ni halali bila ya kumhusisha Padri. Kwa vile mara nyingi, na hali hii ingalipo hadi hivi leo, Padri ndiye anayekuwa mtu wa mwisho kuonana na mtu anaekaribia kukata roho ili kumpa sala na toba za mwisho, mipango kama hiyo, ilihakikisha kwamba kanisa linakumbukwa ipasavyo, katika wasia wa mtu husika. Kwa ufupi, kanisa Katoliki lina historia ndefu iliyojaa matendo ya kidhalimu, katika nchi mbali mbali ulimwenguni. Kwa mfano, tunaweza tukataja Ireland ya Kaskazini ambako Wakatoliki wamekuwa wakifanya mauaji ya kinyama dhidi ya Waprotestanti, kwa zaidi ya miongo mitatu sasa. Hapa kwetu Afrika mashariki, tunasikia tayari wamekwisha kuunda tume ya majeshi, na hapa nchini, inadaiwa pia kuwa wana viwanja vya ndege ambavyo ndege hutua na kuondoka bila ukaguzi wa vyombo vya serikali vinavyohusika. Kwa matamshi yake, Askofu Pengo anajifanya haelewi kwamba dhana inayopewa nguvu katika utawala wa kidemokrasia kikatiba, ni imani kwamba nchi ni mali ya wananchi na kwa hiyo, ni haki ya wananchi peke yake kuchagua watu wa kuunda Serikali au kuiondoa madarakani. Kutumia mbinu, hila au njama za aina yoyote ili
kuhujumu matakwa ya wananchi ya kuchagua watu wanaowataka kuwapa madaraka
ya kuongoza serikali ni ukandamizaji na hatimaye hupelekea machafuko na
mauaji katika nchi. Hatutarajii kwamba Pengo angependa kuona haya yanatokea.
|
YALIYOMO
MAONI
YETU
Wananchi
wamwambia Mkapa:
Waislamu watakiwa kuwa watekelezaji wa maamuzi ‘Hajj Trust’ yaongeza huduma kwa mahujaji MAKALA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
Mwenye Macho……
|
|
|
|
|