|
MASHAIRI
Kijijini
Kijijini nakupenda, kunamahindi nandizi,
Kunayo mengi matunda, kunde, dengu na mbaazi,
Kuna mtamu mlenda, namkumbuka Shangazi,
Mwenzenu ninakupneda, sana kijijini kwetu.
Jamani babu nabibi, kijijini wamepozi,
Jamani kuku wa bibi, na wale wa babu mbuzi,
Nataka kwenda kwa bibi, kula mihogo na ndizi,
Mwenzunu na kukumbuka, sana kijijini kwetu.
Ifikapo asubuhi, JOGO la babau huwika,
Watu shambani huwahi,ili jembe kulishika,
Ndege nao hufurahi, mitini hufurahika,
Mwenzunu na kukumbuka, sana kijijini kwetu.
Amewaumba billahi, wazuri waloumbika,
Na angani hufurahi, wavutia kwa hakika,
Na Maji nayo Wallahi, TUNGINI yazizimika,
Mwenzetu nakukumbuika, sana kijijini kwetu.
Almasi H. Shemdoe, “
Tunda la Matumaini”,
Dar es Salaam, Tanzania.
Tabia za Watanga
Leo nachukua Tanga, kama fumbo jamiini,
Kuwaeleza Watanga, TABIA zao nchinini,
Tanga watu wa kuringa, hasa kwa kujua dini,
Ukitaka uishi nao, jifunye wewe mjinga.
Tanga bwana kwa mamwinyi, karahaatake nani,
Tanga si kwa bwana Mwinyi, kwangu mwana wa HASANI,
Tanga utaminywa minyi, kwa fani ya ugangani,
Ukitaka ishinao, jifanyewewe mjinga.
Watanga kwa majivuni, hakuna tena nchini,
Hjawachelewi kulani, wakipewa mtihani,
Tanga watu wa kulani, harakati ziko chini,
Ukitaka ishinao, jifanye wewe mjinga.
Tanga kuzuli lakini! Kunapendeza machoni,
Hasa kwetu milimani,kule Lushoto nyumbani,
Tanga mjini jamani, KISIMA cha Qur-ani,
Ukitaka ishi Tanga, jifanye wewe mjinga.
Tanga jama amekeni, wa Tanga badilikeni,
Ngangari wote kueni, ndivyo apenda manani,
Watanga moto washeni, umwinyisasa acheni,
Ukitaka ishi Tanga,jifanye wewe mjinga.
Sita beti nimwishoni, Tanga kwenu ni fumboni,
Ngangari wapojueni, KILIMILE muoneni,
Wakali wa kila fani, Tanga hawakosekani,
Ukitaka ishi Tanga, jiganye wewe mjinga.
Almasi H. Shemdoe,
“Tunda la Matumaini”,
Dar es Saaam.
Bandari Salama
Dar es Salaam yaleo, ndiyo Bandari Salama,
Myaka mingi hadi leo, mji wenye usalama,
Mji wa maendeleo, mji wa walikwa nyama,
Karibuni ni walimwengu, mwone Bandari Salama.
Bandari ya raha leo, jiji maarufu sana,
Bandari yenye vileo, makabila chungu sana,
Taifani tegemeo, viwanda vimejazana,
Karibuni walimwengu, mwone Bandari Salama.
Jiji lawatu kibao, hilo Bandari Salama,
Jamani urithi wao, toka tangu nyingi za miaka
Kutoka kwa Babu zao, akawapa Mola mwema,
Karibuni walimwengu, mwone Bandari Salama.
Bora mawasiliano, Bandari Salama leo,
Bandari ya mapatano, kwa nchi yetu ya leo,
Taifani ni mfano, kwa yetu maendeleo,
Karibuni walimwengu, mwone Bandari Salama.
Baba Bandari Salama,sasa ni Dar es Salaama,
Chetu kivutio chema, Badari ya watu wema,
Wapl.e wasio vuma, wakazi Dar es Salama,
Karibuni walimwengu, mwone Bandari Salama.
Beti sita kaditama, karibu Dar es Salama,
Njoo Bandari Salama, Pwani upate simama,
Upepo Mwanana mwema, ufukwelini unavuma,
Karibuni Walimwengu, mwone Bandari Salama.
Almasi H. Shemdoe
, “Tunda la Matumaini”,
Dar es Salaam, Tanzania.
|
YALIYOMO
MAONI
YETU
Mapinduzi Zanzibar yameleta
kilichokusudiwa?
Wananchi
wamwambia Mkapa:
Mbumbumbu
wa demokrasia waliomo katika chama tawala ni hatari zaidi
Waislamu
watakiwa kuwa watekelezaji wa maamuzi
‘Hajj
Trust’ yaongeza huduma kwa mahujaji
DONDOO
MUHIMU
MAKALA
Jamii
ijihadhari viongozi wasaliti
MAKALA
Msimamo
wa Pengo haushangazi
KALAMU YA MWANDISHI
Kitendawili
cha millenia: Urais bila dola
MAKALA
Dhana
ya kumwabudu Mungu anayeafiki udhalimu lazima tuikatae
MAKALA
Mapinduzi
Zanzibar: Dhuluma bado ipo
MAKALA
CCM
haiwezi kuondosha umasikini Tanzania
MAKALA
Tirivyogo
la sekta ya elimu
Mwenye Macho……
Demokrasia
haiwezi kujengwa kwa kuvunja katiba
HABARI
ZA KIMATAIFA
MASHAIRI
MICHEZO
Baadaya Mkapa kushindwa kusaidia:
Prof. Lipumba aombwa kuiombea Tanzania FIFA
Mtwa aanza kulala mapema
Salvatory aitwa Mtibwa
|