|
Na. 082 Jumatano Januari 10 - 16, 2001 |
|
|
|
|
|
NUKUU ZA MANENO YA MWALIMU NYERERE KUHUSU MUSTAKABALI WA HALI YA MAISHA YA WANANCHI KATIKA MAZINGIRA YA WACHACHE WANAO NEEMEKA: * Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu? * Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii. * Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi? * Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga. * Wengi katika watu wa nchi zetu ni wajinga ndiyo maana hukubali kutawaliwa hivyo. * Kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ni wajinga tu. * Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira (idiots), kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe.... * Ni ukweli usiopingika kuwa masuala ya maendeleo ni masuala halisi na hayawezi kuwa masuala ya ubabaishaji tu. * Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao (wananchi) na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili. Nukuu hizi zimo katika kitabu kinachoitwa
'Reflections
On Leadership in Africa' VUB University Press, 2000.
|
YALIYOMO
MAONI
YETU
Wananchi
wamwambia Mkapa:
Waislamu watakiwa kuwa watekelezaji wa maamuzi ‘Hajj Trust’ yaongeza huduma kwa mahujaji MAKALA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
Mwenye Macho……
|
|
|
|
|