|
Na. 082 Jumatano Januari 10 - 16, 2001 |
|
|
|
|
|
Mapinduzi Zanzibar:
Na Mosi Suleiman IJUMAA wiki hii, Januari 12, 2001, Zanzibar itatimiza miaka 37 tangu kufanyika kwa mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Sultan Jamhsid Abdullah El-Busaidy tarehe kama hiyo mwaka 1964. Katika mapinduzi hayo yaliyopelekea damu kumwagika, 'Wazanzibar' walishika 'mashoka na mapanga' kumng'oa Sultan huyo baada ya Wazanzibario hao wakiongozwa na Marehemu Abeid Karume, "kunyimwa haki ya kuingoza Zanzibar kupitia chaguzi mbalimbali zilizofanyika Visiwani humo tangu kujipatia uhuru wake mwaka 1962. Lengo la Mainduzi yale, ilikuwa kuondoa dhuluma dhidi ya wananchi iliyodaiwa kuwepo wakati wa utawala wa Sultan Jamshid. "Waikisumwa' na silka ya kibinadamu ya kutokubali kudhulumiwa japo u-dhaifu, wananchi hao walitia nia moyoni: "kufa na kupona," dhuluma iondoke. Wananchi hao hawakuechelea nguvu ya kijeshi alizokuwa nazo Sultan Jamshid wala 'sapoti' yake toka Mataifa ya Ulaya. Walimvaa Sultan 'kichwa kichwa' ambaye hakuwa na jinsi ila kuwapisha wananchi. Ninadhani Wazanzibari wale hawakufanya mapinduzi yale eti kwa sababu Sultan alikuwa ni Mwarabu, bali kwa sababu kiongozi yule wa dola ya Zanzibar alikuwa akiwafanyia dhuluma. Tanganyika (sasa Tanzania Bara) iliyaunga mkono Mapindizi yale na bila kuchelewa ikatangaza kuitambua serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyoundwa chini ya Marehemu Abeid Karume. Lakini tusidhani kama Tanganyika iliyaunga mkono mapinduzi yale kwa vile aliyeng'olewa alikuwa ni Mwarabu, bali tunadhani ni kwa sababu iliaminika Sultani Jamshid hakuwa akiwatendea haki wananchi walio wengi. Lakini hali ya mambo ilivyo Visiwani Zanzibar hivi sasa inasikitisha na kutisha, na wala haitoi picha ya makusudio ya mapinduzi hayo kama tulivyoeleza hapo juu kwamba tunadhani hivyo. Kadhallika msimamo wa Tanzania Bara juu ya Siasaza Zanzibar hauoneshi kukubaliana na jinsi tulivyoeleza tunavyodhani hapo juu. Hivi kweli Mzanzibari leo hii yuko huru na salama kama alivyotarajia mwaka ule 1964 alipojitolea 'kufa au kupona' akiamini anaondoa dhuluma Visiwani mwake? Hivi sasa, mahali popote, unapozungumza demokrasia, ni muhimu ukatofautisha "demokrasia" na "demokrasia ya kweli". Hivi ni kwa kiasigani "demokrasioa ya kweli" imeruhusiwa kukua Visiwani humo? Je Wazanzibari wenyewe wanapata mwanya wa kuwachagua viongozi wawatakao? Wazanzibari wamekuwa wakilalamika kwamba viongozi wao hawatokani na ridhaa yao bali "huchaguliwa Chimwanga, Dodoma." Je haya ndiyo matunda ya mapinduzi waliyoyafanya mwaka 1964 walipojitolea muhanga roho na mali zao? Mzee Aboud Jumbe alishika wadhifa wa Rais wa Zanzibar kwa mara yamwisho kwa kipindi kilichoanzia 1980 ambapo aliingia madarakani kwa kuchaguliwa na Wazanzibari. Lakini aling'olewa madarakani Dodoma, kabla ya muda wake kwisha! Vipi chaguao la Wazanzibari halikuheshimiwa?! Katika uchaguzi wa mwaka 2000, CCM Zanzibar ilimpendekeza Dk. Mohammed Bilali kumpa kugombea urais wa Zanzibar, lakini kikao cha Dodoma 'kikampitisha' Amani Karume ambayeWazanzibari hawakumpa japo nafasi ya pili! Vipi chaguo za Wazanzibar hazikuheshimiwa?! Wakati wa kampeni za uchaguzi huo huo wa 2000 ni kwa kaisi gani Wazanzibari walikuwa huru kuhudhuria mikutano ya vyama halali vya siasa, mbali ya chama tawala, bila kubughundhiwa na polisi, kutishwa na hata kupewa mkong'oto? Magari ya dereya yalisafirishwa toka Tanzania Bara kwenda Viiwani 'kukuza' hofu miongoni mwa Wazanzibari. Je ni kwa kiasi gani sheria za uchaguzi ziliheshimiwa: Je masanduku ya kura hayakuporwa toka vituoni kabla ya kura hazijahesabiwa jambo ambalo ni kinyume chasheria hizo? Na leo hii rais aliyeko Madarakani, ushindi wake umepatikana kufuatia hali hiyo ya ukiukwajiwa sheria za uchaguzi. Je Mapinduzi ya Zanzibar 1964 ndio yalilenga kuleta hali ihiyo? Lakini hali mbaya si ya kisiasa tu bali pia kijamii. Haikuwa desturi kwa Wazanzibari kunywa pombe au kubwiya unga, haikuwa desturi kwa hinti wa Kizanzibari kutokeza hadharani akiwa amevaa 'pensi', 'mini sketi', 'skin tight' (nguo za kubana mwili) au singlet (kiblauzi chenye kuacha wazi sehemu ya mgongo na kifua cha binti). Lakini leo hii, baada ya watawala wa mapinduzi kuingia 'usharika' na Wataliano wafungue na kuendesha biashara ya utalii Visiwani humo, desturi ya Mzanzibari kila siku inapoteza uungwana na, badala yake 'mapambiko' kwa ubaradhuli. Si jambo geni tena kumwona binti wa Kizanzibari - Azma, Bishara, Khadija, Salma, Mwanahamis, Mwanakombo -akiongozana na boyfriend kwenda beach au hotelini (au nyumba ya wageni 'kupumzika'). Hivi ni kweli Wazanzibari mwaka ule wa 1964 walitoa muhanga mali zao na maisha yao ili kuleta hali hiyo isiyomithilika - wananchi wanabambikwa kesi za kutunga, na kusota rumande wengine wanapigwa; hawapo huru kuwachagua viongozi wanaowapenda; mabinti wanatembea uchi, vijana wabobea kwenye ulevi na mengine ambayo tunayahifadhi. Bila shaka Wazanzibari wanaendelea kudhulumiwa, na mlolongo wa mambo. Baadhi ya Wazanzibari wamefikia kusema "heri ya utawala wa Sultani". Ikiwa ni kweli utawala wa kisultani ndio uliokuwa ukifanya dhuluma iliyopelekea kufanywa mapinduzi ya 1964, basi yawezekano mapinduzi hayo hayakuung'oa "utawala wa kisultani" bali yalimng'oa Sultani Jamshid, na nafasi yake kuchukuliwa au kupewa Waswahili. Nimependa kutoa wito kwa Watanzania wote - Wazanzibari
(waliofanya mapinduzi) na Watanzania Bara ambao wao serikali yao wakati
huo iliyaunga mkono mapinduzi hayo - kulitafakari jambo hili. Ijumaa, Januari
12, 2001 au utakuwa ni njiani kweda au kutoka msikitini kuhudhuria sala
ya pamoja ya kila wiki (sala ya jumaa), jaribu kuvuta fikra ya nini hatma
ya hali hiyo.
|
YALIYOMO
MAONI
YETU
Wananchi
wamwambia Mkapa:
Waislamu watakiwa kuwa watekelezaji wa maamuzi ‘Hajj Trust’ yaongeza huduma kwa mahujaji MAKALA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
Mwenye Macho……
|
|
|
|
|